Hiki ni kichekesho cha MMEM!

Mwishoni mwa mwaka jana, Wizara ya elimu iliitia "kash kash" asasi isiyo ya kiserikali iitwayo HakiElimu. asasi hiyo ilikuwa na matangazo mengi katika vyombo ya Habari yakielezea kwa kina hali halisi ya elimu nchini. Msisitizo wao ulikuwa katika kumulika matokeo ya Mpango wa (Maendeleo) ya Elimu ya Msingi, yaani MMEM.
Kwa wengi wetu, matangazo hayo yalikuwa yakiutoboa ukweli wa wazi mkabisa ingawa Sirikali haikuutaka. Ukweli wenyewe ni pamoja na kuwapo kwa ubadhilifu mkubwa wa fedha za Mpango uliofanywa na walimu wakuu wakishirikiana na wakubwa kinyume na malengo husika.
Ushirikishwaji duni wa wananchi katika Mpango mzima lilikuwa ni tatizo lingine lilobainishwa, kutokuwapo kwa kipaumbele cha kujenga shule za wanafunzi wenye ulemavu, mbinu zisizofaa zinazotumiwa na walimu katika ufundishaji na mengine mengi. Hayo yalikuwa kweli tupu, na haikuhitaji shahada ya uzamili kuujua. HakiElimu hata hivyo, walikuwa wamefanya utafiti wa kutosha katika hilo. Sirikali kwa kutumia nguvu zake ikaijia juu HakiElimu kwamba inaongopa. Ikasitisha matangazo hayo.
Kichekesho chenyewe ni kwamba baada ya kuyapiga marufuku matangazo hayo, Wizara ya Elimu sasa inatumia fedha nyingi kubuni na kurusha matangazo mengi yenye maudhui ya ajabu kabisa. Kwamba wanataka wananchi waamini kuwa mpango wa MMEM ulifanikiwa kuliko kawaida! Eti walemavu wamewezeshwa, madarasa bora yamejengwa na mengine mengine sijui nini na nini. Huku ni kujaribu kuwachezea wananchi ambao sirikali inadhani hawaelewi chochote na kwamba wao ni watu wa kuambiwa tu, utafikiri hawaoni.
Leo hii ukitembelea shule zilizojengwa katika mpango huu, hutakosa kubaini kwamba maisha ya madarasa hayo ni mafupi mno na kwamba yalijengwa chini ya kiwango kilichokusudiwa awali. Jambo la kufurahisha ni kwamba walimu wakuu waliokuwa shapu wakati wa mpango huu, wamemalizia nyumba zao na wengine wanamwaga lenta za nyumba zao wanakula kuku kwa mrija saaaafi.
Nafikiri matangazo hayo yalitakiwa kuonyesha mambo hayo na sio kuwadanya wananchi ambao kimsingi wataanza kuumia muda si mrefu, madeni makubwa yatakapoaanza kulipwa. Tutalipa mabilioni wakati waliofaidika ni wachache? Biashara ya namna gani hii? Ni bora tukawa wa kweli kuliko kuwa wakali tunapokosolewa makosa yetu ya makusudi.

Maoni

  1. Bwaya,
    Kwanza niseme ahsante kwa maoni ambayo umeyaacha kwenye uwanja wangu na ahsante kwa kuwa msomaji mzuri wa makala zangu za kila jumapili ndani ya Tanzania Daima.
    Kuhusu hili la elimu mimi nashindwa hata kuelewa nini kinatokea na inakuwaje wananchi waishie kunong'ona tu wakati waathirika ni wao wenyewe na watoto wao.Nadhani lazima tuchukue msimamo thabiti.Masuala muhimu kama haya sio sahihi kabisa kuachiwa wachache,wenye vitambi,ambao watoto wao washamaliza shule siku nyingi sana,kutuamulia.Natumaini JK ameshaanza kulivalia njuga hili kwa sababu nasikia alilisemea hovyo alipozuru wizara ya elimu hivi karibuni.Nadhani tatizo huko nyuma halikuwa aina gani ya masomo yanafundishwa bali nini kinafundishwa;ukoloni mpya?utumwa wa akili?

    JibuFuta
  2. Bwaya hapo ndipo kwenye utata huyu mama wa CCM aliyekuwa chanzo cha kukwamisha madai ya walimu Tanzania sasa ni Waziri wa Wizara hiyo. Amepewa zawadi baada ya kuwaweka kimya walimu kwa miaka. NiMEONA NAYE KAANZA NA LONGO LONGO ZA MUNGAI KUHUSU MICHEZO. Kuna nini hapa nadhani kazi kwetu kuwapasha ukweli maana kuua elimu nchini ni kuwanyima raia wetu haki yao kama binadamu.

    JibuFuta
  3. Leo nimeamua kusema nawe kaka!
    kazi yako nimeona mwanangu,ninachoshukuru hapa ni kuwa yule mama kama alivyosema Bw Jeff pale juu kawekwa katika wizara ileile, lakini ikiwa ni moja kati kumkomesha huyo mama na sio kumpa shukrani katika kile alichowafanyia walimu.
    unajua ni kama Magufuli aliuza nyumba za serikali kwa jeuri na kiburi, JK kamkabidhi rungu linalohusu nyumba huku akimsimanga kuwa hatuuzi nyumba...sasa kazi kwake kumpinga bosi,kwa kufanya mauzo ama kurudisha nyumba na kukoma kucheza mchezo mchafu.

    JibuFuta
  4. Nafurahi kukupa taarifa kuwa nitaanza kusoma huku kwako pia nashukuru kwa kunishtua ndugu yangu,unajua kuna Mtu anakwitwa Makene na mwenzake anakwitwa Mkwinda wamekuwa wananifanyia matendo yasiyo katika tambo zao, hadi nakosa muda wa kutembelea wengine,nitajitahidi kaka!

    JibuFuta
  5. Bwaya yawezekana umesahau kuwa mara nyingi msema kweli huonekana muongo na msema uongo huonekana mkweli midhali ana nguvu za kusemea. Tena akisema kwa Kingereza ndio inaonekana jiniasi kabisa. Hii MMEM mimi nilikuwa naisikia tu kama kitu kingine kama mlio wa mbuzi vile. Lakini matangazo ya HakiElimu nilikuwa nayahusianisha na ukweli ambao nimeuona kwa macho yangu mawili. Lakini ona sasa ukweli umeshafanywa uongo na maisha yanaendelea tu na sisi tuko kimya.

    Lakini haya yote yana mwisho wake.

    JibuFuta
  6. safari bado ni ndefu! si umeona jinsi form four walivyoboronga? inabidi kuchukua jukumu rasmi kufufua elimu yetu kwani na huu utandawizi utatumaliza wajameni!

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?

Tabia za Mtoto wa Miaka 0 – 3 Kimahusiano na Kihisia