Tunawezaje kujinasua na matatizo ya msongo wa mawazo?

Hivi sasa imekuwa ni kawaida kukutana na mtu anayezungumza mwenyewe. Na si tu kuzungumza mwenyewe, bali hata kurusha rusha mikono huku na kule. Waweza kukutana na mtu anayetazama lakini haoni, anayesiki lakini hasikilizi, na anayesema asichojua anachokisema.

Si hivyo tu. Imeanza kuzoeleka kukutana na mtu ofisini mwenye hasira za mafungu dhidi ya kila anayehitaji huduma yake. Hasira zinazoambatana na kufoka, kusema pasi mpangilio, na hata kutukana watu wasio na makosa ya moja kwa moja hovyo hovyo.

Vile vile, ni kawaida kukutana na watu wenye ghadhabu katika sehemu za umma, kama kwenye usafiri wa wote, foleni za benki na kadhalika. Watu wanaonekana kuwa na hasira ambazo kimsingi chanzo chake si hapo alipo.

 Hizi ni dalili za msongo wa mawazo. Na zipo nyingi.

Kuyasema haya hatujaribu kuonyesha kuwa msongo wa mawazo/stress ni kitu kibaya moja kwa moja. Hapana. Kwa hakika kiasi fulani cha stress kinahitajika ili kutufanya tuhimizike kupiga hatua fulani.

Hata hivyo, msongo huu wa mawazo  unapoambana na uendelevu, hali ya kutokufika mwisho, huzaa matatizo. Wengine mpaka wanaathirika afya zao. Wapo ambao shauri ya msongo wa mawazo, hujikuta wakishindwa kumudu mahusiano na watu wengine.

Je, hali hii inatokana na nini? Kwa nini tumeanza kukumbwa na msongo wa mawazo katika siku za leo? Kuna visababishi vipi vinavyosababisha tuwe na msongo wa mawazo? Na kwa nini katika mazingira haya haya wapo watu wasiopatwa na matatizo haya? Kwa nini hakika hali hizi hizi, watu hawa hawa, na maisha haya haya yanayosababisha msongo kwa wengi wetu, yasisababishe msongo kwa watu wengine?

Je, kuna mbinu zozote za kuweza kudhibiti msongo wa mawazo? Je, tunaweza kujilinda na kupatwa na maradhi haya ya kusongwa songwa na mawazo?




Maoni

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?

Tabia za Mtoto wa Miaka 0 – 3 Kimahusiano na Kihisia