Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai, 2010

Strictly gospel na mijadala ya kiimani

Nimekuwa mfuatiliaji wa karibu wa blogu maarufu ya Strictly Gospel . Tofauti na blogu nyinginezo, wachangiaji wengi wa blogu hii nawafahamu kwa sura ingawa mmiliki wake sijawahi kuonana naye. Japo mara nyingine nashindwa kushiriki mijadala hiyo ya kiimani moja kwa moja kama ambavyo huwa nashindwa kublogu humu ndani, ni karibu kila siku lazima napita pale kuona namna mijadala ya kiimani inavyokwenda. Hapa nimeupata huu hapa mmoja. Bonyeza hapa kuusoma na bila shaka utajifunza mengi. Unayo maoni yoyote? Tembelea blogu nzima hapa .

Bongo inaumwa kisichoonekana (2)

TUMEKWISHA kuona namna nchi yetu inavyopiga hatua kubwa za kimaendeleo. Na sina shaka kwamba msomaji atakuwa amebaini kwamba hizo zinazoonekana kuwa hatua za kimaendeleo zina walakini. Aidha, tulikuwa tumeishia katika kuyatazama hayo yanayoitwa maendeleo katika sekta ya elimu yanavyolisaidia taifa. Muunganiko wa muhimu ukawa ni kwa vipi rasilimali watu ambayo taifa halikuwa nayo miaka iliyopita, inatusaidia katika kusukuma “maendeleo” mbele? Hapa tungependa kudodosa namna ambavyo ukuaji wa taaluma katika maeneo mbalimbali unavyosukuma mbele maendeleo yetu ili kujaribu kuona ulikolalia ugonjwa wa taifa. ******************************************************* Tumekuwa tukifundisha wanasheria kwa miongo kadhaa sasa. Hawatoshi, lakini wapo na wnafanya kazi zao katika maeneo mbalimbali nchini. Je, watu hawa wametusaidiaje kuondokana na unyanyasaji wa kisheria tunaoupata katika jamii zetu? Taaluma ya sheria imegeuka kuwa mashindano ya kupangilia hoja ili kushinda kesi zisizo na tija....

Bongo inaumwa kisichoonekana

Ni wazi kuwa nchi ya Bongo ya miaka kadhaa iliyopita, si hii ya leo. Mambo mengi ya msingi yanabadilika na kwa kweli yanabadilika kwa kasi kubwa. Hata hivyo, ningependa kuonyesha kwamba tatizo tunalokabiliana nalo katika nchi yetu limejificha katikati ya haya tunayoyaona kama maendeleo. Tatizo hilo haliwezi kutatuliwa kwa kusogeza zaidi maendeleo kwa wananchi wala wala kwa kuanua demokrasia zaidi wala kukusanya kodi zaidi wala kwa kuongeza wasomi zaidi. Tatizo hilo linaweza kutatuliwa kwa kupembua upotofu wa aina ya maendeleo yetu tunayoonekana kuyataka zaidi na tukiyapata tunayatangaza kupitiliza. Tutazame maendeleo katika sekta ya mawasiliano. Nchi hii haijawahi kushuhudia maendeleo yaliyofikiwa hii leo katika teknolojia ya mawasiliano. Tuko juu katika nyaja ya mawasiliano baada ya kuwa tumefungua milango yote miaka ya tisini. Yapo makampuni kibao yenye wateja wanaokaribia milioni ishirini kati ya raia milioni arobaini. Na wote hao wanapigiana simu na kuandikiana ujumbe mfupi wa m...

Kwa nini wewe tena Oktoba hii?

Picha
Unatusumbua! Kadiri siku zinavyosonga wajikomba sa-na Salaamu mpaka unaboa! Eti ‘mmeamkaje wapenzi wangu niwapendao…’ Fataki mkubwa wewe! Ulikuwa wapi siku zote? Kisa cha kumsalimia mtu barabarani? Umejua maana yetu eh? Hivi hukutujua siku za nyuma? Unadhani tumesahau… Sikia, Tunakumbuka nyodo zako mara chache ulizokuja Tunakumbuka kauli zako za maudhi Eti sie wako tu iwe isiwe Tukupe tusikupe haikusumbui Ukasema hata ukiwa kule sie wa hapa ni wako Sasa babu sikiliza Mwaka huu ni wa hapa hapa Wote ‘twajua huna uumini wowote Unatafutaga nini kipindi hiki? Ni hivi hivi tu waja majisidi? Wenzio ‘twaswali weye unadipu Kisa? Eti ule mpango wa mlo huko nje Unachekesha… Yaani mie mwenye njaa nikulishe wewe unayebeua! Yaani unitumie fasta, kama kondomu sina maana tena? Umesahau ulivyotufanyia siku zile? Tumekupa ukala ukaondoka? Shukrani yako sitasahau: vumbi la fo wili mjini Kama hunijui vile… Nashangaa umenirudia...

‘Vijana waache kutumiwa’

Picha
JINA LA KAMALA si geni kwa wanablogu wengi. Yeye ni mwendeshaji wa blogu maarufu inayojadili (pamoja na mambo mengine) masuala ya kiutambuzi. Bonyeza hapa kuitembelea . Ndugu Kamala anajulikana pia kwa namna yake ya utoaji maoni huru katika blogu anazozitembelea ambayo hufikirisha na mara nyingine kuibua mijadala zaidi. Blogu hii ilipata fursa ya kuzungumza naye siku chache zilizopita kuhusu falsafa zake, blogu, dini, siasa na mambo yake binafsi. Karibu kujua zaidi kuhusu mwanablogu huyu anayeblogu kutokea kanda ya ziwa. ________________________________________ Ndugu Kamala, nashukuru kwa kukubali kutumia muda wako ili tuweze kujadiliana masuala mawili matatu. Labda tuanze na falsafa yako binafsi. Unaamini nini katika maisha ambacho ndicho kinachobeba utambulisho wako kama Kamala? Naamini katika utu, ubinadamu, upendo na umoja. Napenda kuelewa vitu na kudadisi na ndio maana natumia majina ya kihaya tu ninayoelewa maana yake na kwa nini yawepo… napenda kuacha maisha yaende na kuf...

Mazungumzo na Kamala Luta

Siku chache zilizopita nilipata bahati ya kufanya mazungumzo mafupi na Bw. Kamala Luta, mwanablogu machachari ambaye si mara moja amewahi kuibua mijadala mizito kupitia maoni yake huru ama makala kwenye blogu yake. Kaa mkao wa kula. Nitayachapisha mazungumzo yake mapema sana namalizia kuweka koma, nukta na funga semi.

Msaada wa msamiati...

Baada ya kimya cha ukumbi huu kwa muda mrefu na mwendo wa 'kuibuka na kuzama' kwa sababu zilizokuwa nje ya uwezo wangu, sasa nimerejea rasmi. Tutaendelea kujadili, kuhoji, kuelimishana na hata kupotoshana inapotulazimu. Kumbuka huwezi kuelimika pasipo kupotosha mtazamo ulionao. Sasa nitangulie kuwaomba misamiati ya maneno haya kwa kiswahili fasaha: ethics, ethos, morality na morals. Nayafahamu maneno haya vizuri lakini sina maneno husika kwa kiswahili fasaha. Sipendi ule mtindo wa kutumia sentensi nzima kuelezea neno moja. Naomba mnisaidie kuongeza msamiati. Nitafurahi kupata majibu hayo hata kwa barua pepe kwa watakaopenda kutumia njia hiyo. Natanguliza shukrani za dhati!