Inasemekana wasomi wanakimbilia siasa. Wanaowaunga mkono wanasema serikali haijali utaalam wao. Inawakejeli kwa malipo kiduchu. Wao, kwa kuona kuwa siasa zinalipa, wanaamua kuzitelekeza fani zao wanakimbilia majimboni kwa lengo la kupata maslahi manono. Inasemwa pia kuwa siasa nayo inawahitaji wataalam kama Maprofesa, Madaktari wa Falsafa na watu kama hao. Kwamba ubobevu wao unatoa mchango mzuri likija suala la maamuzi. Je, ni kweli wanasaidia katika maamuzi? Je, si kweli kwamba kila aina ya ufisadi tunaousikia leo umefanyika mikononi mwa wasomi? Wamesaidia nini? Wanaowapinga, wanasema kuwa elimu yao ilipaswa kujikita katika kuileta jamii maendeleo kupitia fani walizobobea bila kujali serikali inawajali ama la. Kwamba wangejikita vema katika fani zao, ni lazima wangeyapata mafanikio hayo wanayoyafuata katika siasa. Wanasema, kuna ulazima gani wa kila mtu kukimbilia siasa ili kufanikiwa? Je, siasa ndio kila kitu? Je, kukimbilia siasa si dalili ya ufinyu wa elimu yetu? Wanashin...
Tunasubiri.
JibuFuta@BWAYA: Mkuu salama lakini?
JibuFutaDu, Baba mtakatifu Mkodo salama! Ndo kwanza nimerejea. Mambo vipi?
JibuFutaDa'Mija asante kwa kupiga hodi. Nilifunga nyumba kwa muda, nimerudi. Karibu tupo!