kwanza nilidhani dhamira,pili nilidhani ubinadamu,tatu nilidhani nyakati mpya,nne nildhanai ilani ya chama itawekwa kando,tano nilidhani hisia za kweli shauri kaishi mjini.....kumbe ilikuwa kama kawaida wabongo tunavyopenda kusikia neno 'ahadi'. asante kwa kutembelea blogu yangu pia
WANAUME wengi wanaamini wanawake, kwa kawaida, ‘wanapenda hela.’ Kwamba ukiweza kumhakikishia mwanamke 'uhakika wa kiuchumi' unakuwa umemaliza. Ingawa hatuwezi kupuuza ukweli kuwa uhakika wa 'kiuchumi' ni moja wapo ya mahitaji ya mwanamke, lakini si sahihi kuamini kuwa moyo wa mwanamke unaweza kuthamanishwa kwa fedha. Fikra hizi walizonazo wanaume [kuwa anachokihitaji mwanamke ni fedha] zimeleta matatizo mengi katika mahusiano na ndoa. Kwa mfano, wapo wanaume ambao baada ya kuhakikisha wenzi wao wamepata mahitaji ya msingi, basi wanawatelekeza kihisia. Hali hii husababisha upweke mkubwa kwa wanawake hawa wanaojikuta hawana mtu wa karibu kuwasikiliza isipokuwa vitu.
Nimekuwa mfuatiliaji wa karibu wa blogu maarufu ya Strictly Gospel . Tofauti na blogu nyinginezo, wachangiaji wengi wa blogu hii nawafahamu kwa sura ingawa mmiliki wake sijawahi kuonana naye. Japo mara nyingine nashindwa kushiriki mijadala hiyo ya kiimani moja kwa moja kama ambavyo huwa nashindwa kublogu humu ndani, ni karibu kila siku lazima napita pale kuona namna mijadala ya kiimani inavyokwenda. Hapa nimeupata huu hapa mmoja. Bonyeza hapa kuusoma na bila shaka utajifunza mengi. Unayo maoni yoyote? Tembelea blogu nzima hapa .
Kuna wakati unaweza kufikiri unaigiza msimamo na kejeli kwa maumivu ya mtu, unakuwa na maoni yasiyo na haya kwa mateso ya wenzako ukijua unawafurahisha watu fulani lakini hayo maigizo ya kukosa huruma kwa mwenzako yana uwezekano wa kugeuka tabia kweli na ukawa mtu katili kweli kweli. Michezo, dini na siasa visikuchochee kujiona una haki ya kubeza masaibu wanayopitia wenzako kwa sababu mdogo mdogo mizaha hugeuka ukweli. Mwaka 1971, Philip Zimbardo, mshunuzi na mwalimu wa Chuo Kikuu cha Stanford, alifanya utafiti maarufu kama #StanfordPrisonExperiment akilenga kuchunguza nguvu ya mazingira kwenye tabia. Utafiti ulivyofanyika Zimbardo alitengeneza gereza la kuigiza hapo chuoni likiwa na seli, mahali mfungwa angekaa mwenyewe, mahali pa wanyarapa kuishi, mahali wafungwa wangetoka na kuteswa na wanyapara. Washiriki walifanyiwa mchujo wa haiba kuona kama ni watu wenye utimamu wa tabia na hisia. Kwa njia ya nasibu (random assignment) wanafunzi...
Wiki hii mimi na familia yangu tulikuwa na kikao cha ‘halmashauri kuu’ ya mwaka. Kikao chenyewe kililenga kujitathmini sisi kama familia na kujiwekea malengo ya pamoja kwa mwaka 2023. Kikao hiki kinatarajiwa kufuatiwa na kikao cha 'Kamati Kuu.' Maandalizi ya kikao hiki cha 'banguabongo' yalifanyika kwa kupeana dondoo za kufanyia kazi agenda za kikao. Hatimaye siku ikawadia. Jioni ya Jumapili ya Desemba 25, 2022. Tukiwa eneo tulivu mbali nyumbani, baada ya mwenyekiti wa kikao kueleza kwa nini tumekutana, shughuli yenyewe ikaanza. Agenda ya kwanza ilisomwa na mtoto wetu wa kwanza, “Kitu gani ulichofanya mwaka huu kinakufanya ujisikie fahari?” Tukatakiwa kuandika kwenye vikaratasi vidogo tulivyokuwa tumegawiwa tayari. “Tumieni vikaratasi vya kijani. Mambo matano makubwa yaliyokufanya ukajisikia fahari kwa mwaka huu.” Baada ya kila mmoja kuorodhesha mambo yake matano yaliyomwendea vyema mwaka huu, mtoto wa pili akakusanya vikaratasi vyenye majibu na kuvibandika kwenye u...
SAIKOLOJIA, neno lililotoholewa kutoka neno la kiingereza psychology, si elimu inayoeleweka sana katika jamii yetu. Asili ya 'psychology' ni neno 'psyche' lenye maana ya nafsi. Katika makala haya, tunasaili kwa ufupi maana ya saikolojia kama taaluma na kuonesha nafasi ya taaluma hiyo ngeni katika jamii yetu katika kutatua matatizo ya kijamii na hivyo kuharakisha juhudi za watu kujiletea maendeleo yetu.
Katika makala haya, tunatazama kwa ufupi makuzi ya mtoto mwenye umri wa siku moja mpaka miezi 36. Tutaangalia mambo ya msingi yanayonesha ukuaji wa mtoto unavyoendelea katika maeneo makubwa manne; 1) ukuaji wa kimwili 2) kiakili 3) kimahusino na watu wengine na mwisho 4) kihisia. Kwa kawaida maeneo haya manne yanategemeana ili kumwezesha mtoto kukua kwa ujumla. Kwa mfano ili mtoto akue kimwili, anahitaji ukuaji wa akili ipasavyo ambayo nayo itaathiri namna anavyomudu hisia zake na hivyo kuhusiana na watu wengine. Kwa hiyo ni sawa tukisema hakuna ukuaji wa eneo moja usiotegemea eneo jingine.
Dan Brown mwandishi wa kitabu kinachokwenda kwa jina la Da Vinci Code , kafanya kile ambacho binadamu wengine hatuthubutu hata kukijadili. Kaamua kuchokonoa mambo ya kiimani ambayo watu tunakwepa kuyahoji, kwamba hayajadiliki. Ni dogma. Trela ya filamu yake hii hapa . Katika Da Vinci code, Dan Brown anajaribu kuchimbua “kweli” zilizojificha nyuma ya ukristo, “kweli” ambacho zimefunikwa na kanisa ili kuwapumbaza watu waamini kwamba Jeshua alikuwa mwana wa Mungu. Kwa kadiri ya Da Vinci Code, ukweli wenyewe ni kwamba Ukristo ulianzishwa na “nabii wa kawaida” ambaye hastahili kujidai kwamba ana uungu (divinity) wowote. Nabii mwenyewe ni Yesu Kristo. Kwa hakika, alimwoa Mariam Magdalena, ambaye baadaye ndiye aliyemchagua kuliongoza kanisa baada ya kifo chake. Suala hili, kwa mujibu wa Da Vinci Code, liliwakasirisha sana wanafunzi wake na baada ya kusulubishwa kwake, Mariam Magadalena ilibidi atimuliwe, ndipo akakimbilia Ufaransa na mtoto wao waliomzaa na Yeshua “mume” wake. Mwandishi anas...
kwanza nilidhani dhamira,pili nilidhani ubinadamu,tatu nilidhani nyakati mpya,nne nildhanai ilani ya chama itawekwa kando,tano nilidhani hisia za kweli shauri kaishi mjini.....kumbe ilikuwa kama kawaida wabongo tunavyopenda kusikia neno 'ahadi'.
JibuFutaasante kwa kutembelea blogu yangu pia
Karibu mpangala. Nimependa lugha yako.
JibuFuta