CHANGAMOTO Insha za Jamii - Prof. Mbele



Natamani sana kukisoma kitabu hiki. Ninakitafuta kwa bidii. Unajua kinakopatikana?
Mwandishi Profesa Mbele anasema kakiandika kusahihisha majungu kuhusu Mwalimu Nyerere. Msome hapa halafu uone kama unaweza kujishindia Dola 100!

Waweza pia kusoma majadiliano katika Jamii Forums yanayodurusu ikiwa wanaomkosoa Mwalimu Nyerere wana hoja.

Maoni

  1. Nilishakisoma. Hakuna jipya. Utapoteza pesa zako bure.

    Kuhusu majungu ya Nyerere kuna insha moja tu humo basi.

    Unaweza kusoma makala zote zilizomo humo katika blogu ya kwanzajamii.com.

    Please don't waste your money

    JibuFuta
  2. Ndugu mtoa maoni hapo juu: waweza kunijulisha kinatopatikana kitabu hiki? Kuhusu umuhimu wa yaliyomo humo, nadhani hilo linabaki kuwa MTAZAMO BINAFSI WA AKISOMAYE (na si maoni jumla ya asikiaye maoni ya WALIOKISOMA)!

    JibuFuta
  3. Shukrani ndugu Bwaya, kwa ulizo lako. Kitabu kinapatikana mtandaoni, hapa. Mipango ya kukifanya kipatikane Tanzania ilianza muda kiasi uliopita. Kuna dada mmoja mjasiriamali pale Bagamoyo anauza vitabu vyangu, simu yake ni 0754 445 956, na mwingine yuko Dar es Salaam, simu yake ni 0754 888 647.

    Kwa taarifa ya ziada, ni kuwa nilikiandika hiki kitabu cha CHANGAMOTO ili kiweze kueleweka kwa wananchi na kuwavutia, kuanzia kule kijijini. Nashukuru kuwa vijana wa kijiji cha Msoga (yaani kwa JK) wanakipenda, kwa mujibu wa ujumbe walioniletea. Bora uwasiliane nao kwanza, simu 0715 841 122, usije ukanunua halafu ukakuta ni bidhaa feki :-) teh teh teh teh.

    JibuFuta
  4. Asante sana Profesa kwa maelekezo murua. Kwa apendaye kujifunza zaidi maudhui ya kitabu hicho, sasa anaweza kujua pa kuanzia. Nitafanya utaratibu wa kupata nakala yangu mapema!

    Asante sana kwa mara nyingine.

    JibuFuta
  5. Ni miezi kadhaa na masiku mengi tu sijaonekana katika tasnia hii ya blog.
    leo nimerejea tena. Nawaahidi mambo mazuri, karibuni kibaraza cha Tegelezeni. Tupo Pamoja.

    JibuFuta
  6. Habari za siku.
    Kama mwanablogu kutoka Tanzania,nakuomba kushiriki kuchangia Mchakato wa KUFUFUA JUMUWATA(Jumuiya ya Wanablogu Tanzania).

    Tafadhali naomba ufungue hii kurasa ya
    http://blogutanzania.blogspot.com/
    kisha upendekeze jinsi ya kufufua JUMUWATA.

    Ahsante

    Luiham Ringo.

    JibuFuta
  7. Bwana Bwaya:

    Japo nawe umepotea bila kuaga kama mimi, natumaini kwamba huko uliko ni kwema. Ukiweza RUDI !!!

    Nilikuwa napita hapa kusema kwamba sasa nimerudi tena rasmi. Tupo pamoja !!!

    http://matondo.blogspot.com/2011/12/wanablogu-wenzangu-na-wapenzi-wote-wa.html

    JibuFuta
  8. Profesa Matondo,

    Nimezipokea habari za kurejea kwako wa furaha.

    Nami, bila shaka nitarudi si muda mrefu. Kuna mawili matatu yalichukua sehemu kubwa ya masaa ninayokuwa macho.

    Asante kwa kupitia hapa. Tuko pamoja!

    JibuFuta
  9. Kaka Bwaya upo salama nimekumiss na wengine pia naamini wamekumiss.

    JibuFuta
  10. Anonymous wa kwanza, naona unajikanyaga. Kwanza unakibeza kitabu hiki, na papo hapo unawashauri watu wakasome makala kwenye tovuti ya "Kwanza Jamii." Makala zile ndizo zilizomo katika kitabu, na mwandishi ni mimi. Kama ni kweli kitabu ni duni hivyo, je, unataka watu wakapoteze muda wao kule "Kwanza Jamii"?

    Kama ni suala la kupoteza hela kwa kununua kitabu hiki, kwa nini unawaambia watu wakasome makala kwenye blogu, wakati unajua fika, au unapaswa kujua, kuwa wengi wanaenda "internet cafe" kusoma hizi blogu, na unajua kuwa wanatumia fedha kulipia huko "internet cafe?" Kitabu hiki kina makala nyingi, na kuzisoma huko internet cafe inaweza kugharimu kiasi kinachofanana na bei ya kununua kitabu. Anonymous unajikanyaga.

    Wewe ni msomaji moja, na una haki ya kutoa mawazo yako kuhusu chochote unachosoma. Lakini mimi nawajua pia wasomaji ambao wana mawazo tofauti na yako. Kwa mfano, mwanablogu Freddy Macha ameyapenda mawazo niliyoandika kitabuni mle kuhusu elimu ya kijijini, na kuhusu mwalimu wa shule ya msingi. Ameandika hivyo mitandaoni. Vile vile, ninajua kuwa kitabu kinapendwa na vijana katika kijiji cha Msoga, kule Bagamoyo. Nimeshapata taarifa zao tena na tena, na nimeandika hivyo katika blogu yangu. Kutokana na mawaidha ya wanakijiji wa kijijini kwangu na hao wa Msoga, ningekuwa na uwezo, ningepeleka nakala kwenye vijiji vingine nchini. Insh'Allah, nitafanya hivyo siku za usoni.

    Kwa sababu hujajadili lolote lililomo kitabuni, najiuliza iwapo kweli wewe umekisoma kitabu hiki au kama umeziangalia tu kurasa zake. Kuhusu Mwalimu Nyerere, pamoja na kuwa nimeandika makala moja tu inayomlenga yeye, lakini vile vile nimemnukuu katika makala zingine. Ingekuwa wewe ni mtu makini, ungetambua hilo. Nahisi wewe ni mbambaishaji tu ambaye hata kusoma ni tatizo kwako.

    Kama hata yale niliyoandika kuhusu Shaaban Robert si mapya kwako, basi wewe ni mtaalam na msomaji uliyebobea. Kama hata yale majadiliano yangu na Jeff Msangi ni mambo ya kawaida tu kwako, basi nakuvulia kofia kuwa ni mtu mwenye upeo mpana wa masuala. Lakini, nawajibika kusema kuwa hakuna dalili kuwa wewe ni mtu makini kiasi hicho.

    Ingekuwa wewe umekisoma kitabu hiki, na ni mtu mwenye upeo wa kusoma na kuelewa, angalau ungetambua kuwa nimesema kuwa watu wa kijijini kwangu walivutiwa na yale niliyoandika katika "Kwanza Jamii," wakanihamasisha kuandika zaidi. Kama nilivyoandika katika kitabu hiki, nilikuwa nawawazia watu wa kijijini kwangu. Hata hivyo, kitabu kikishachapishwa, watu wa kila aina wanakuwa na fursa ya kukisoma au kukichungulia, wakiwemo wababaishaji kama wewe anonymous.

    JibuFuta
  11. good sharing information

    JibuFuta
  12. i like it this blog information

    JibuFuta
  13. Thanks you for good information

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?

Pay $900? I quit blogging