Dini: Matamanio ya kinadharia

Dini hunadi matamanio na taraji za kinadharia, zisizo halisi. Dini zinatangaza hukumu kwa mambo ya kimaumbile (nature) zikilenga kuwafanya watu kuishi maisha ya kimaigizo, yasiyoyao.

Kwa mfano, zipo dini zinalazimisha 'makada' wake wenye damu kama sisi kutokuoa, ama kuolewa. Ilani hii ya useja, hata ikiwa nzuri vipi, inabaki kuwa mapendekezo mazuri yasiyotekelezeka.

Huwezi kupambana na maumbile na ukanikiwa. Huwezi kuusukuma mwamba na kweli ukasogea ukiona.

Kwa hiyo, matokeo yake unakuta wenye dini wanabaki kuzungumza kitu wasichokifanyia kazi.

Hadharani wanazuia watu kuoa, gizani wanayatenda yayo hayo wanayoyazuia.

Hadharani wana uwezo usioelezeka, sirini ni dhaifu kama wadhaifu wengine.

Nini maana yake? Je, ni kweli dini i zaidi ya uhalisi? Je, miujiza inayonadiwa na dini, ni jambo lililo halisi? Je, dini si jumla ya matamanio hafifu
yenye mipaka ya kibinadamu?

Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Pay $900? I quit blogging

Fumbo mfumbie mwerevu