Kumwua Muisrael si kuua?

Wengi wetu tunajua zile amri kumi ambazo Musa/Moshe alizipewa na mwenyezi Mungu ili ziwe dira ya maisha ya wana wa Israel wakati na baada ya safari yao ya jangwani. Tunajua kuwa amri hizo zinatuhusu hata sisi wa kizazi hiki tusiokuwa waisraeli.

Katika hizo amri ipo inayosema Usiue. Yaani Mungu akizuia binadamu yeyote kumtoa uhai kwa makusudi binadamu mwenzake.

Ninaweza kuonekana wa ajabu nikiuliza: Hivi amri hii ilimaanisha usimwue nani? Ni kuua tunakokufahamu ama kuna neno linaloendelea ambalo huenda lilihaririwa na Moshe?

Ninasema hivi kwa sababu, baada ya Musa kufia mlimani, na mamlaka ya kuwaongoza wana wa Israeli kushikwa na Yoshua kuna jambo la ajabu lililotokea. Wale jamaa walipokuwa wakiingia kwenye nchi ya ahadi, Kanani, nchi ambayo ilikaliwa na wenyeji wakati wairaeli wakiishi Misri, yalifanyika mauaji makubwa ambayo hayana tofauti na yale ya kimbari. Watu kwa maelfu walipoteza maisha yao. Mauaji haya ninashawishika kuamini kuwa yaliyazidi yale yaliyotokea Rwanda miaka ya tisini.

Ni Yoshua ndiye aliyekuwa kinara wa mauaji haya akijua fika kwamba Mungu alikuwa amekataza kuua. Na inaonekana hata Mungu mwenyewe aliyaunga mkono mauaji hayo maana aliagiza wateketeze kila kilichokutwa katika nchi ile. Kwa maana nyingine pamoja na Mungu wa Israeli kuamrisha kuwa mwanadamu haruhusiwi kuua, yeye mwenyewe aliruhusu uuaji wa kutisha kwa mkono wa Yoshua. Aliruhusu mauaji ya binadamu aliowaumba yeye. Mauaji ya kimbari.

Naomba kuuliza: kuua kunakosemwa na biblia ni kupi? Ni kuua Mwisraeli ndiko kunakokatazwa na kwamba ukiua asiye Mwisraeli unakua hujaua? Naomba ufafanuzi kwa wanaouelewa utata huu.

Maoni

  1. Hili swali gumu. Kwa maana mpaka leo hii Mpalestina akiua Muisraeli mmoja Waisraeli wataua kibao. Cheki hata mambo yaliyotokea Lebanoni baada ya kuteka sijua askari wawili wa Kiisraeli. Hivyo naamini Waisraeli wenyewe huamini kuwa ni zaidi ya mataifa mengine.

    JibuFuta
  2. Iliuweze kuwa muumini muri wa dini fulani hutakiwi kuwa mdadisi kiasi hiki. Ni sawasawa na kumchunguza kuku wa kiswahili, hutamla.

    JibuFuta
  3. Ninakubaliana na wewe Kitururu. Ninatafuata kujua: hivi ni kweli Mungu anawathamini zaidi Waisraeli kuliko viumbe vingine katika sayari hii ama ni mtazamo tu wa wachache wetu?

    Halafu huyu bwana anayeficha jina lake kanifurahisha sana. Kwa nini umle kuku bila kumchunguza? Kwa nini ule utumbo bila maswali?

    Nadhani ni bora usimle kuku kwa sababu umebaini kasoro yake kuliko kumla kwa sababu analiwa na kila mtu wa kabila lako!

    Ukimtafiti ukajua ubora wa nyama yake, utamla kwa furaha na kujiamini. Au sio bwana anonimasi?

    JibuFuta
  4. Kama hujui Mungu aliruhusu kufa kwa Waisraeli zaidi hata ya alivyofanya kwa mataifa mengine. Kila walipokosa aliwaambia kuwa ataweka upanga ila hatawamaliza kabisa. Mungu aliruhusu kufa kwa mataifa mengine na hata kuteketea kabisa lakini si kwa wana wa Israeli. Kwa hiyo si kwamba Mungu amewaruhusu wao tu kuua. Jikumbushe yaliyowakuta kule Ugerumani, na pia soma vizuri kitabu cha Daniel na Ezekieli, na pia malizia kitabu cha nabii Amosi utapata ni nini Mungu amekuwa akiwafanyia Waisraeli. Si mema tu bali hata mabay pindi wanapokosa.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Haiba ni nini?

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Makundi Manne ya Tabia za Watoto Kitabia

Uislamu ulianza lini?