Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia 2015

Nilichojifunza Katika Miaka 10 ya Kublogu

Picha
Kwa mara ya kwanza nililisikia neno blogu mwaka 2004. Wakati huo nilikuwa msomaji wa dhati wa safu ya ‘Gumzo la Wiki’ iliyokuwa ikiandikwa na Ndesanjo Macha katika gazeti la Mwananchi. Kwa kufuatilia anuani iliyokuwa ikihitimisha safu hiyo, niligundua kuwa sikuhitaji kusubiri   Jumapili kuweza kulisoma ‘Gumzo’. Anuani hiyo ilikuwa ni ya blogu ya kwanza ya Kiswahili ikiitwa Jikomboe .

Tabora wamemsamehe Lowassa, au ni dalili za kukubalika kwa UKAWA?

Picha
Matokeo ya utafiti mdogo uliofanywa na mwandishi wa makala haya katika mitaa ya mji wa Tabora jioni ya leo, umeonesha kwamba kuna ushindani mkali kati ya Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Ufisadi wa Richmond, Edward Lowassa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dk Wilbroad Slaa, kama uchaguzi mkuu ungefanyika kati ya saa 10 – 12:30 jioni hii. Matokeo hayo yanaonesha kwamba Lowassa ana asilimia 28 na Dk Wilbroad Slaa angepata asilimia 22.

Watoto Waliokosa Masomo Nchini Libya Wafundishwa kwa Njia ya Skype

Picha
Hali tete ya kiusalama nchini Libya imewafanya watoto washindwe kwenda shule tangu mwezi Oktoba. Kwa kuwa watoto hawawezi tena kuhudhuria masomo katika shule zao, El-Zahawi aliwaza ni kwa nini asisogeze madarasa karibu na huko walipo? Na hapa ndipo Shule ya Skype ya Benghazi ilipozaliwa rasmi.

CCM ni maarufu Kigoma kwa 40.2%, ikifuatiwa na CHADEMA kwa 27.2%

Picha
Utafiti huru uliofanywa na mwandishi wa makala haya, umeonesha kwamba mgombea yeyote wa nafasi ya Urais wa Chama cha Mapinduzi angeweza kuchaguliwa na wapiga kura wa Manispaa ya Ujiji/Kigoma kwa asilimia 40.2% ikiwa uchaguzi mkuu ungefanyika kati ya saa 11 mpaka saa 1 na nusu jioni ya leo.

Kujenga Nidhamu kwa Mtoto wa Miaka Miwili hadi Mitatu

Picha
Kiini cha mahusiano ya mzazi na mwanae asiyezidi miaka mitatu, ni upendo. Kupitia upendo mzazi anaweza kufikiri vizuri zaidi kile anachokihitaji mtoto na kukishughulikia ipasavyo. Hata hivyo, si wakati wote mtoto wa umri huu hutaka kilicho sahihi. Wakati mwingine kile kinachoonekana kuwa hitaji la mtoto, kina hatari ndani yake na hakiwezi kuachwa kifanyike kwa kisingizio cha kulinda uhusiano wa mtoto na mzazi. 

Wafilipino Wauliza ‘Rais Yuko Wapi?’ Wakati wa Majanga ya Kitaifa?

Picha
  "TWITI TENA kama unadhani PNoy alipaswa kuhudhuria mapokezi ya heshima badala ya tukio la Kiwanda cha Magari. #NasaanAngPangulo" alitwiti @BobOngWords. Alama habari #NasaanAngPangulo, yenye maana 'Rais yuko wapi' katika lugha ya Kitagalog, ilikuwa mada maarufu zaidi kwenye mtandao wa Twita duniani wakati Wafilipino walipokuwa wakionesha hasira zao kwa Rais Noynoy Aquino kufuatia  kukosekana kwake  kwenye mapokezi ya heshima ya miili ya polisi waliouawa wakiwa kwenye operesheni maalum.

Unavyoweza Kumsaidia Mtoto Kuwa Mkweli

Picha
Bila shaka umewahi kujiuliza kwa nini mtoto amekudanganya kwa jambo dogo ambalo, kwa hali ya kawaida, angeweza kukwambia ukweli na mambo yakaisha. Chukulia kwa mfano, una watoto kadhaa nyumbani. Unagundua kuna kosa limefanyika. Unapowauliza kujua nani aliyehusika, hakuna anayekuwa tayari kukubali. Kama umekuwa ukijiuliza kwa nini watoto hudanganya, usiwe na wasiwasi.  Karibu watoto wote hudanganya katika mazingira fulani fulani. Wanapodanganya, hata hivyo, nia yao huwa ni kulinda uhusiano wao na wewe mzazi kwa kusema kile wanachojua unakitaka.  Tahadhari ni kuwa ikiwa kudanganya kwa nia njema kutaachwa kuendelee, hujenga tabia ya uongo mbeleni.

Wafilipino Walivyomficha Papa Francis Hali Mbaya ya Haki za Kijamii Nchini Humo

Picha
Makundi ya haki za kijamii yalizuiwa na Polisi kukaribia msafara wa Papa Francis. Picha kutoka kwenye ukurasa wa facebook wa Kathy Yamzon

Watoto Wagomvi, Wasumbufu na Wenye Utukutu katika Umri wa Miezi 0 – 36

Picha
Tangu tumeanza mfululizo huu, tumejaribu kuonesha namna tabia za mtoto zinavyohusishwa na malezi ya mzazi kuliko vinasaba. Kwa ujumla tumeona kile anachokifanya mtoto ni matokeo ya kufikiwa au kutokufikiwa kwa matarajio yake . Katika makala haya tunaangalia kundi la watoto wenye tabia za ugomvi, utukutu, ukaidi na usumbufu na kuona namna mazingira ya kimalezi yanavyochangia hali hii.

Watoto Wanaopenda Kucheza Kuliko Kujifunza Katika Umri wa Miezi 0 – 36

Picha
Pamoja na kuwa kucheza ni hitaji la msingi katika kujifunza kwa mtoto, michezo ipaozidi wazazi wengi hupata wasiwasi. Michezo huweza kupoteza muda mwingi sana wa mtoto, muda ambao ungeweza kutumika kwa mambo mengine. Kwa kawaida mtoto anayependa sana michezo ni 'mtu wa watu' na kumtenga na watoto wenzake ni kama adhabu. 

Tabia ya Kukwepa Watu kwa Watoto wa Miezi 0 - 36

Picha
Tuliona namna malezi yanavyosababisha watoto kujiamini nakuthamini wengine . Katika makala haya tutaangalia makosa kadhaa yanayofanywa na wazazi kwa kujua au kutokujua ambayo husababisha mambo yanayoweza kuchukuliwa na wengi kama ‘matatizo ya kitabia’. Hata hivyo, kuna ukweli kwamba kinachoonekana ni tatizo chaweza kuwa fursa katika mazingira mengine. Kwa sababu ya kupunguza urefu wa makala moja katika kueleza makundi yote kwa pamoja, tutaangalia kundi moja kwa makala.

Athari za Matarajio na Malezi ya Mtoto wa Miaka 0-3

Picha
Umewahi kujiuliza kwa nini watoto wengine ni waoga na wenye aibu wanapokuwa na watu wakati wengine wana ujasiri hata kusimama na kuzungumza mbele ya hadhara ya watu wazima? Kwa nini mtoto mwingine huonekana kupenda sana watu lakini huwa mgomvi na mwenye kutatua migogoro kwa kupigana?   Iweje watoto watofautiane tabia katika mazingira ambayo wakati mwingine wanakuwa wamezaliwa katika familia moja? Hilo ndilo tunalolenga kulitazama kwa mhutasari.