Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2014

Mambo ya Kufanya Unapotafuta Kazi

Picha
INGAWA inafahamika kuwa wapo wahitimu, tena wengi tu, ambao hufanya maamuzi ya kutumia ujuzi na maarifa waliyoyapata darasani kujiajiri wenyewe, kwa maana ya kubadilisha maarifa na ujuzi walionao kuwa bidhaa pasipo kumtegemea mtu aitwaye mwajiri, bado tunajua kuwa wahitimu wengi, kadhalika, huchagua kutafuta ajira. Kwao, huona ni rahisi kujipatia kipato cha kuendesha maisha yao kwa njia hiyo. Makala haya yanasaili mambo yanayoweza kumsaidia mhitimu anayetafuta ajira kupata taarifa zinazohusiana na namna bora ya kuwasiliana na mwajiri kwa matumaini ya kupata ajira anayoitegemea.

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -2

Tuliona katika makala iliyopita  maana ya saikolojia na kuhitimisha kwamba kinachotazamwa zaidi katika saikolojia ni tabia. Kwa hakika matatizo mengi yanayoikabili jamii yetu chanzo chake ni tabia. Tabia ndio chanzo cha matendo tunayoyaona kama kukosekana kwa uaminifu, ubadhilifu wa mali za umma, ufisadi, migogoro ya ndoa, misuguano ya kijamii, chuki, upendo, ugaidi, unyanyapaa, ubaguzi wa rangi, ubaguzi wa kidini, changamoto za kimalezi na kadhalika. Yote haya yanaweza kuchambuliwa na kupatiwa majibu yake kwa kutumia sayansi ya tabia (saikolojia). Katika makala haya nitatoa mifano mifano kadhaa kuonesha namna sayansi ya tabia, inavyoweza kutumika kutatua matatizo yanayoikabili jamii.

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Picha
SAIKOLOJIA, neno lililotoholewa kutoka neno la kiingereza psychology, si elimu inayoeleweka sana katika jamii yetu. Asili ya 'psychology' ni neno 'psyche' lenye maana ya nafsi. Katika makala haya, tunasaili kwa ufupi maana ya saikolojia kama taaluma na kuonesha nafasi ya taaluma hiyo ngeni katika jamii yetu katika kutatua matatizo ya kijamii na hivyo kuharakisha juhudi za watu kujiletea maendeleo yetu.

Mambo Muhimu ya Kuzingatia Unapoondika Barua ya Kuomba Kazi

Picha
Barua ya kuomba kazi ni waraka ambao mara nyingi husomwa kabla ya waraka mwingine wowote unaoambatanishwa katika kuomba kazi. Ni vyema barua ya kuomba kazi ikaandaliwa kwa umakini, na kujaribu kugusa kwa ufupi mambo yaliyoonekana kwenye wasifu binafsi kumvutia mwajiri mtarajiwa.

Wajibu wa pamoja wa mwajiriwa na mwajiri katika kuziba pengo la ujuzi unaotakiwa kazini

Picha
Katika makala yaliyopita tulisaili kwa uchache kile hasa ambacho waajiri wengi wanahitaji kukiona kwa watu waombao ajira. Kwa kifupi tuliona kwamba pamoja na uwezo wa kutumia nadharia za darasani katika mazingira ya kazi, waajiri wanatafuta kuona ujuzi tuliouita 'rahisi', au kwa kiingereza soft skills. Huu ni ujuzi usiosomewa lakini ndio huwa mithili ya mafuta yalainishayo ngozi iliyofubaa, kwa maana ya kuongeza ufanisi wa ujuzi rasmi wa kazi. Kama tulivyoona, kutokuoana (mismatch) kwa mahitaji ya mwajiri na sifa za mtafuta kazi ni moja wapo ya changamoto kubwa katika ulimwengu wa sasa wa ajira. Kwamba wapo watu wengi wenye kutafuta ajira kwa kuamini kuwa wanazo sifa za kuajiriwa, lakini waajiri wanaotazamiwa kuwapokea watu hao wakiwatilia shaka kuwa hawana uwezo wa kujaza nafasi walizonazo. Ni tatizo la elimu au mtazamo ? Wapo wanaoamini kwamba tatizo ni elimu. Kwamba tunawajaza wanafunzi maarifa ya kinadharia ambayo kwa hali halisi hayahitajiki kwenye soko la ajira....

Waajiri Wanatarajia Nini kwa Waombaji wa Kazi?

Taarifa ya Utafiti wa Ajira na Kipato ya mwaka 2012 , iliyotolewa na Idara ya Takwimu ya Taifa mwezi Julai 2013, inaonyesha kwamba nchi yetu ina waajiriwa rasmi 1,550,018.  Kati yao, asilimia 64.2 wameajiriwa katika sekta binafsi na waliobaki (asilimia 35.8) wameajiriwa katika sekta ya umma. Aidha, taarifa inasema ni asilimia 24.8 pekee ya wafanyakazi hawa, wanapata kipato cha kuanzia Tsh 500,001 kwa mwezi [vipato vya wafanyakazi wengi (asilimia 54.4) ni chini ya Tsh 300,000 kwa mwezi.] Nafasi za kazi zisizojazwa Takwimu za taarifa hiyo zinathibitisha kwamba moja wapo ya changamoto zinazokabili soko la ajira hapa nchini, ni kukosekana kwa waajiriwa wanaokidhi matarajio ya ajira. Kwa mfano, wakati kwa mwaka 2011/12 zilikuwepo nafasi za kazi 126,073 nchini kote, ni wafanyakazi wapya 74,474 tu waliweza kuingia kwenye soko la ajira kwa kipindi hicho. Kadhalika, takwimu hizo hizo zinaonyesha kuwa nafasi za kazi zipatazo 45,388 hazikuweza kujazwa katika kipindi hicho. ...

[VIDEO]: Mazungumzo na Liberatus Mwang'ombe na Solomon Chris baada ya Uchaguzi DMV

Picha
Mubelwa Bandio kati akiwa na aliyekuwa mgombea wa nafasi za Mwenyekiti wa Jumuiya DMV Liberatus Mwang'ombe (L) na mgombea nafasi ya Katibu Msaidizi Solomon Chris (R0 wakati wa mahojiano Agosti 9, 2014, Jumuiya waTanzania waishio Washington DC, Maryland na Virginia nchini Marekani ilifanya uchaguzi wake mkuu. Matokeo yake yamekuwa yakipingwa na waliokuwa wagombea wa uchaguzi huo kutokana na sababu mbalimbali. Wamaketi na Vijimambo Blog na Kwanza Production kueleza sababu hasa za kupinga matokeo hayo siku ya Jumatano ya Agosti 13, 2014. Karibu uungane nasi kusikia wanachopinga

Nilichojifunza katika maonyesho ya tatu ya wanasayansi chipukizi wiki hii

Picha
MAONYESHO ya wanasayansi chipukizi yaliyoandaliwa na T aasisi ya Young Scientists Tanzania yamefikia hatma yake wiki hii. Maonyesho haya ya siku mbili, yaliyofanyika kati ya tarehe 13 na 14 Agosti katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es salaam, yameacha mafunzo makubwa kadhaa. Kwanza, yameweza kufanya ieleweke vizuri zaidi kwamba wanafunzi wanayo hamasa kubwa ya kufanya sayansi ikiwa watawezeshwa, kinyume kabisa na madai ya mara kwa mara kwamba sayansi haipendwi na wala haifanyiki mashuleni. Washindi wa kwanza wakikabidhiwa zawadi na Dk Bilal. Picha: @bwaya Katika muda wa siku mbili hizi, nimeshuhudia namna bongo za wanafunzi wa shule za sekondari, tena nyingi zikiwa zile za kata, zinavyochemka katika kujaribu kutatua changamoto zinazowakabili. Inasisimua kuwaona wanafunzi wakijaribu kutafuta mbinu za kupambana na vyanzo vya magonjwa, uharibifu wa mazingira na kutatua changamoto zinazowakabili watu wetu katika kujiletea maelendeleo kwa ujumla. Hilo limekuwa wazi kupitia maonyes...

Wanafunzi waonyesha namna teknolojia rahisi inavyoweza kurahisisha upigaji kura bila kufika kituoni

Picha
NIMEFIKA hapa Diamond Jubilee kama mwananchi anayetamani kujionea hamasa waliyonayo wanasayansi chipukizi kuonyesha kazi zao nzuri. Ni maonyesho ya tatu ya Sayansi katika ukumbi wa Diamond Jubilee ambayo hatimaye hapo kesho yatawaibua wanafunzi wawili kama washindi wa tatu wa shindano la wanasayansi chipukizi hapa nchini linaloandaliwa na Young Scientists Tanzania. Baadhi ya washiriki kwenye ufunguzi wa maonyesho leo. Picha: @bwaya Kwa hakika hamasa ni kubwa. Wanafunzi wamejawa na msisimko wa aina yake kuonyesha matokeo ya tafiti zao walizozifanya tangu mwanzoni mwa mwaka huu. Wamejawa na matumaini, hasa kwa sababu ya maneno ya ufunguzi yaliyosemwa na Mkurugenzi wa YST, Dk Kamugisha wakati akiwakaribisha asubuhi ya leo. "Tulipata maombi ya kushiriki kutoka shule zaidi ya 200...lakini ni maombi 100 pekee yalifanikiwa kupenya katika mchujo. Mpaka hapo ninyi ni washindi. Kilicho muhimu zaidi, ni kwamba pamoja na kwamba kazi zenu zitapitiwa na watu wanaoelewa vyema zaidi maene...

Young Scientists Tanzania: Kujenga utamaduni wa kutafuta ufumbuzi wa matatizo yetu kisayansi

Picha
YAMEKUWEPO madai ya siku nyingi kwamba elimu yetu haijaweza bado kutufundisha kufikiri sawa sawa. Kwamba tunafundishwa kukariri, kukumbuka na kurudia rudia yale yale tunayofunindishwa madarasani. Hatufundishwi zaidi ya nadharia za mambo yanayojulikana tayari. Hatufundishwi kuyatazama mambo kwa macho ya kutafuta kujua yasiyojulikana. Matokeo yake, tunaambiwa, hata wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu, wamekuwa wakipata taabu kujifunza namna sahihi ya kufanya tafiti kama sehemu ya Shahada zao. Nini sababu ya hali hii? Mwonekano nje ya ukumbi wa Diamond Jubilee jioni hii. Picha: @bwaya Wengine wanasema, hatujaweka msisitizo kwenye sayansi, kwa maana ya kutafiti. Kutafuta majibu ya matatizo yetu kwa njia za kisayansi. Inasemwa, hali iko hivi kwa sababu shule zetu hazijawezeshwa. Resources. Siku zote wimbo umekuwa ni ule ule kwamba "Serikali, serikali, serikali", "Shule zetu hazina maabara...wala vifaa",  "Kukosekana kwa maabara, maana yake ni kupungua kwa...

Unauelezaje utamaduni wa kusainiwa kitabu na mwandishi?

Picha
Profesa Mbele anaeleza vizuri kuhusu utamaduni wa kusainiwa vitabu katika blogu yake:  "...Suala hili la kusaini au kusainiwa vitabu linastahili  kutafakariwa. Naamini lina vipengele kadhaa muhimu, kama vile kiutamaduni, kisoshiolojia, kisaikolojia, na kifalsafa. Hata katika maduka ya vitabu hapa Marekani, aghalabu utaona vimepangwa vitabu vya mwandishi vikiwa na ujumbe "Signed copy." Jambo hili linaisukuma akili yangu kutaka kulielewa zaidi. Ningependa kujifunza zaidi kuhusu suala hili, kwa kusoma maandishi mbali mbali na kufanya tafakari mwenyewe..."  Msomaji wa kitabu cha Profesa Mbele, akifurahia nakala ya kitabu. Picha: @hapakwetu Unaweza kusoma zaidi kwenye blogu yake hapa . Kama mmoja wa wasomaji waliowahi kupata bahati ya kusainiwa kitabu na mwandishi mwenyewe, mmoja wapo akiwa Profesa Mbele, mwandishi wa kitabu kizuri cha " Africans and Americans Embracing Cultural Differences ", nikiri kabisa kwamba suala hili lina muujiza wa aina...

Hotuba ya Mhe Kikwete akizungumza na wa-Tanzania waishio Washington DC

Picha
Karibu kusikiliza hotuba ya Mhe. Dk Jakaya M Kikwete alipozungumza na waTanzania usiku wa Agosti 2, 2014 kwenye hotel ya Marriot, jijini Washington DC nchini Marekani. Kwa hisani ya Mubelwa Bandio.

Namna ya kukopeshwa kirahisi na kuchangiwa michango ya harusi na marafiki

Picha
WALA usishangae hata kidogo. Umesoma vyema kabisa kichwa cha habari. Tunataka kujifunza namna bora kabisa za kuwapiga watu mizinga. Kukopa na kuchangiwa michango ya harusi. Vyote hivi vinafanana kimsingi kwa sababu vyote vinategemea hisani ya watu wanaoitwa ndugu, jamaa na marafiki. Kwako usiyekopa, nikuambie mapema kabisa, hapa si mahali pako. Makala haya ni mahususi kwetu sisi wakopaji maarufu ambao (ni kama vile) haiwezekani kabisa kumalizia mwezi bila kuongezea na za watu. Sasa ili nieleweke nawalenga watu gani, niseme awali kabisa kwamba hatuzungumzii mikopo ya taasisi za fedha kwa ajili ya maendeleo. Nazungumzia mikopo kutoka kwa watu kwa ajili ya kusukuma siku, au misaada ya kufanikisha harusi. Wazo la kuandika mikakati hii madhubuti ya kukopa, nimelipata jana baada ya kusoma taarifa ya google kuhusu kile hasa kilichotafutwa na watumiaji wa mtandao (netzens) kupitia kwenye google, kilichowaongoza na kujikuta wakiwa kwenye blogu yangu. Hapa nanukuu sentensi mbili nilizoziona:...

Mahusiano mazuri na watu hujengwa kwa kutambua na kuheshimu hadhi zao na sio kulinda hadhi yako

Picha
WATAFITI wa saikolojia ya jamii, wanakubaliana kuwa miongoni mwa sababu nyingi zinazosababisha hali ya mitafaruku katika mahusiano ya watu -iwe kazini, nyumbani, na kokote- ni kule kujisikia kushushiwa heshima. Kwa kawaida, binadamu hatupendi kushushiwa hadhi, ego, ambayo ndiyo hutufanya tupambane na yeyote anayetishia kuharibu namna tunavyojiona na pia tunavyoonwa na wengine. Tunaambiwa, watu wenye kuamini kuwa hadhi zao haziko salama , insecure, wenye kujihisi kama watu wenye hitilafu fulani, huwa ni wepesi zaidi kuhisi hadhi zao zinachezewa na hivyo kuhitilafiana na watu kirahisi. Hawa ndio watu ambao, unaweza kuwakosea kwa bahati mbaya huhisi kudharauliwa. "Acha dharau dada!" Ndio kusema hawaamini hadhi zao. Watu secure, wanaoamini kuwa hadhi zao hazitishiwi na wengine, si wepesi kukwaruzana na watu. Sababu ni kwamba hawaoni kirahisi threat ya heshima na hadhi zao, na vile vile wanao uwezo mzuri wa kulinda hadhi na heshima za watu wengine. Migongano ya kimahusiano...