Ndivyo walivyoboresha Elimu?
CCM inajigamba sana kwamba imepanua elimu katika nchi yetu. Katika ilani yake ya uchaguzi, CCM inatuambia kwamba shule za Sekondari zimeongezeka kutoka 1745 mwaka 2005 mpaka shule zipatazo 4102 mwaka jana. Kwamba wanafunzi wanaosoma sekondari katika nchi yetu, wameongezeka kutoka 401,598 mwaka 2005 kufikia 1,401,559 hivi sasa! Kwa mtu anayehesabu mafanikio kwa kuangalia vitu na idadi, haya yanaweza kuonekana kuwa ni mafanikio makubwa sana kuwahi kufikiwa katika nchi yetu. Lakini tukitazama aina ya hao wanaoitwa wanafunzi wanaodaiwa kuwa mashuleni kwa wingi, utashangaa! Katika wanafunzi hao ni asilimia 17.8 tu ndio hufaulu kwa daraja la I. II na III. Umati mwingine unaobaki (yaani asilimia 82.2) wanaishia kupata daraja sifuri na lile la IV. Kwa maana nyingine, kwa kila wanafunzi 10 wanaofanya mtihani wa Taifa, ni wanafunzi wawili tu hupata angalau daraja la III. Hiyo ni elimu ya Sekondari hata baada ya Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari. Ukija kwenye elimu ya msingi ambayo n...