Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari, 2010

Padre Karugendo ndani ya Blogu

Kama ulizoea kusubiri siku ya Jumatano kusoma mawazo ya Padre Karugendo kwenye gazeti la Raia mwema au labda Jumapili kwenye Tanzania Daima, jua enzi hizo zimepita. Sasa utaweza kupata kila unachotaka kwa wakati wowote kupitia blogu yake. Bonyeza hapa kumkaribisha , halafu uendelee kumtembelea. Karibu sana Padre Karugendo. Umechagua fungu jema kufungua blogu.

Tangazo la Mkutano Mkuu wa Uanahabari wa Kiraia wa Global Voices 2010

Picha
Mkutano wa wanablogu wa Global Voices, utafanyika Mjini Santiago mwezi Mei tarehe 6 na 7 mwaka huu. Nimezipata habari hizo kupitia ukurasa wa kiswahili wa mradi wa Lingua Swahili . Nimetamani kama na sisi tungekuwa tunapanga kukutana siku fulani mwaka huu! Inawezekana! Ni muhimu tuanze kufikiri kukutana uso kwa uso hata kama matanga ya ile Jumuiya yetu hajapita bado.

Upweke wa kutokublogu

BAADA ya kimya cha muda mrefu kwa sababu zilizokuwa nje ya uwezo wangu, namshukuru Mungu wa Israeli nimerejea tena. Sijaja na kipya. Ila nimekuja kusoma mengi ya mtandaoni. Ukweli ni kwamba mtandao ni moja ya burudani zangu muhimu sana kama ilivyo mpira kwa wenzangu fulani. Kwa wenzangu na mimi tusiopenda kujua hata matokeo ya mechi za Uefa, wapi zaidi ya kwenye blogu? Nilikosa kusoma posti na maoni ya wanablogu. Nimekuwa kwenye kipindi cha upweke fulani hivi nisioweza kuueleza. Kila siku nijakosa kujiuliza: hivi Baba Mtakatifu Simon kasemaje leo? Da! Watu kama akina Mubelwa, Subira, John Mwaipopo, Yasinta, Maprofesa Mbele (bora hata ninakisoma kitabu chake kwa kukirudia na kukirudia) Matondo, akina Evarist, Kamala, Mbilinyi, Dada Vukani, Kisima, Lundu Nyasa (msee jibu lako nakuja nalo), akina Shabani Kaluse (pole na shule), wazee wa Strictly gospel (hee yale majadiliano nitayarudia mapema sana), na wengine wengi ambao nimebaki nao kichwani mwangu. Nilikosa kusoma mawazo motomo...