Kosa nambari moja

“Kwa nini uliamua kusoma hayo unayoyasoma?”
“Basi tu napenda, hata sijui kwa nini...ila nahisi ni kwa sababu niliyafaulu vizuri zaidi kwenye mtihani wa kidato cha nne…”

“ Kwani unafikiri kuwa nani baada ya masomo yako?”
“…Hata sijui…mambo yatajipanga yenyewe!...”

“ Yatajipanga yenyewe? Sasa ukijakugundua baadae kwamba unataka kuwa mhasibu, na wewe sasa hivi unasoma Fizikia na Kemia…huoni kwamba utakuwa umepoteza muda wako bure kusoma mambo ambayo utaachana nayo?”

“ Ujue future inajipangaga bila kutegemea umepanga nini. Na isitoshe kubadili fani si jambo la ajabu…”

Kwa hivyo unakuta sababu hasa zinazowafanya wanafunzi kufanya maamuzi ya michepuo yao, haziridhishi. Maamuzi ya nitasoma nini hutegemea zaidi ushauri wa wazazi (wanaoongozwa na kiu ya pesa ambao wao wenyewe wameshindwa kuzipata), mkumbo wa marafiki –rika (wanaoongozwa na hamu ya kujitafutia sifa nyepesi nyepesi kwenye jamii) na sababu nyinginezo.

Ni bahati mbaya sana kwamba katika nchi yetu, pamekuwapo na juhudi ndogo sana ya kuwashauri watoto kujielewa mapema ili waweze kufanya maamuzi yanayohusisha hulka na vipaji vyao kuliko ‘nguvu kutoka nje’. Ni kwa sababu hii unakuta kwamba kiukweli, kule wanakoelekezwa wanafunzi na masomo ‘waliyoyachaguliwa’ na jamii kunatofautiana sana na jinsi wao walivyo.

Kwa mfano. Mtu mwongeaji. Asiweza kufurahi bila kupiga kelele na ‘washika dau’. Mwenye papara. Asiyeweza kumaliza dakika kumi na tano mahali pamoja. Mtu wa namna hii anataka kuwa daktari wa binadamu kwa sababu tu alifaulu vizuri Baolojia.

Ama mtu mkimya. Anayeona raha kuwa pekeyake. Hajisikii ukiwa bila marafiki. Hapendi mabishano/majadiliano na watu. Mtu mrahisi kukerwa na watu. Mwoga wa kusema anachofikiri. Mtu huyu anataka kufanya kazi zitakazomkutanisha na watu kama vile sheria, ualimu na kadhalika.

Hili ni kosa kubwa sana tunalolifanya katika maisha yetu. Kutaka kusoma vitu visivyoendana na tabia/personalities zetu. Tunasoma vitu kwa sabbau tu vitatufanya tuwe na heshima kwenye jamii. Kwa sababu tu tunataka kazi zitakazotulipa kwa haraka.

Kwa kufanya hivyo unakuta tunajidhulumu ridhiko la nafsi zetu ambazo zinatutaka kufanya vitu ambavyo vitakuza vipaji vyetu kwa faida yetu na jamii kwa ujumla.

Itaendelea

Maoni

 1. Walimu wa awali wanajukumu zito sana la kugundua na kutafuta uelekeo wa kila mwanafunzi.

  Kila mtoto ana kipaji chake ambacho wale wanaomkuza wanatakiwa wakigundue na wamuongoze vyema ili baadae aweze kukitumia kipaji hicho vizuri.

  Watoto wanapoingia ktk swala la kusoma,huwa wanakutana na changamoto mbalimbali. Kuna wale ambao kulingana na vipaji vyao wanapenda masomo ya sayansi na wengine ya sanaa.

  Changamoto kubwa wanayokumbana nayo ktk kipindi hiki ni kuanza kufundishwa na walimu ambao hawana uwezo wa kukidhi matakwa yao kulingana na vipaji vyao(to cupture the interests of the learners).walimu kushindwa kuwaelekeza wanafunzi vizuri toka awali kunasabisha wanafunzi kuchukia masomo haya na kuyaona ni magumu hata kama kulingana na vipaji vyao walitakiwa kuyamudu masomo hayo.

  Kwa hali hii wanafunzi wanaanza kuchukua mikondo ambayo wanaona ina ukinzani mdogo,yani upande wa masomo ambayo waalimu wake wanafundisha vizuri na kueleweka.

  Hapa sasa yanaibuka makundi mawili, watoto ambao watafanikiwa kuwapata waalimu ambao wataweza kutimiza matakwa yao kulingana na vipaji vyao na wale ambao wataangalia wapi kuna unafuu ili kurahisisha swala la kusoma.

  Hapa nimegusia tu kwa elimu ya msingi,kwa namna ambavyo huanza kuvificha vipaji na kupoteza dira ya mtoto.

  Kuna mzazi ambaye mtoto wake alikuwa mkorofi sana shuleni,na mara nyingi alikuwa hafiki shuleni,basi siku moja mzazi huyu aliitwa shuleni baada ya ukorofi wa mtoto kukithiri, katika majadiliano, mkuu wa shule alimwuliza ule mzazi,namnukuu "hivi wewe mzazi,ulishawahi kukaa na mtoto wako na kumuuliza kama anapenda kusoma au la? ili usipoteze fedha zako kwa mtu ambaye pengine hapendi kusoma" mwisho wa kumnukuu,sasa sijui ilikuwa ni jazba, au alikuwa na maana gani hasa,namwachia yeye,kwani tafsiri yangu yaweza ikawa tofauti sana na alichokuwa anamaanisha.Sasa,fikiria wewe ndiye mzazi,na umerushiwa swali hili,ungemjibu nini?

  JibuFuta
 2. Kama ulikuwepo. Unataka kuwa nani? Daktari. Umeshakutana na wangapi? Sijawahi hata kuongea na mmoja ila napenda nikilazwa nawaona wanakuja na makoti meupe na vidudu vya kuning'iniza shingoni halafu anaamua nani aende nyumbani. Wanakuwa na akili sana"
  Mmhhhhhh!! Hivi ni makosa yetu ama hatujaandaliwa kujua kuna fani ngapi tuwezazo? Yaani kuambia ukisoma HKL lazima uwe mwandishi, ukisoma PGM utakuwa Injinia ama Nahodha ama Rubani, HGE wewe ni mchumi tuu. Kwani KOSA NAMBA MOJA ni la nani hasa? Msomi, mfumo ama waliotutangulia?
  Na hii itaendelea......

  JibuFuta
 3. Kaka naona Kamjadala kanaendelea.
  Kwa leo sitaweza kuchangia, ngoja niwapishe wenye hoja, maana nimeishiwa na maneno.

  JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Pay $900? I quit blogging

Fumbo mfumbie mwerevu