Fumbo mfumbie mwerevu

Kwa sasa sipatikaniki vya kutosha kwa sababu ambayo nitaieleza hapa chini kwa maneno matano. Kwa wale wanaopenda chemsha bongo mnaweza kujaribu na kisha kuweka majibu kwenye kisanduku cha maoni ama kuniandikia kupitia sanduku la barua pepe:

Meelekezo: Hizi ni herufi zilizofichwa (codes) ambazo ili kukupa ujumbe, inakubidi kugundua kanuni iliyotumika kuziandika ili kupata maneno matano ya kiswahili fasaha.

OJUBLVXB OB OJUIBOJ KVNB MJKBMP!

Chemsha ubongo kidogo ndugu msomaji.

Maoni

 1. Kaka Bwaya, wewe unafanya kazi usalama wa taifa nini?
  maana lugha kama hizi zinatumika sana katika taaluma hiyo?
  Vinginevyo inabidi nikuogope!!!

  Kaka fumbo limenishinda.

  Ama kweli fumbo mfumbie mwerevu, mjinga atalifumbua, ha ha ha haaaaaaa!!!!

  Nlikuwa naota tu.......

  JibuFuta
 2. Duh! JIELEWE kweli kweli! NAWAZA TU BADO

  JibuFuta
 3. Kuna msomaji kaniandika anaomba dondoo ili asugue kichwa zaidi.

  Basi. Katika kanuni iliyotumika herufi mbili haziwezi kuandikika. Nazo ni A na Z.

  Nafikiri sasa jibu litakuwa nje nje.

  JibuFuta
 4. NITAKUWA NA 'NITHANI' JUMA LIJALO

  JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo ya Kuzingatia Unapoandika Wasifu wa Kazi (Curriculum Vitae)

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3