Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba, 2008

Kwa mabingwa wa Tafsiri fasaha

Kwa wanaopenda kiingereza.Tafadhali naomba tafsiri ya maneno haya kwa kiingereza ambacho hakitabadili maana iliyopo katika kiswahili hiki: "MAMA, HIVI MIMI NI MWANAO WA NGAPI KUZALIWA?" Ukipata tushirikishane.

Unadhani macho yako yanaaminika?

Picha
Nianze kwa kuomba msamaha. Sijakuwepo mtandaoni kwa siku kadhaa. Nikuombeni kutokukata tamaa ya matembezi kibarazani hapa. Leo ningependa tuangalie suala moja. Kwamba mara nyingi tunavyoyaona mambo sivyo yalivyo. Milango ya fahamu zetu haiaminiki. Hebu tazama picha hii hapa chini. Angalia kwa makini kiboksi A na kiboksi B uone unavyodanganywa na macho. Angalia viboksi hivi. Hakuna rangi yoyote kati ya kiboksi kimoja na kingine, japo macho yako yanakuambia kuna rangi ya kijivu. Bonyeza na hapa uone picha hii . Unajifunza nini? Ukweli na uhalisia ni vitu viwili tofauti.

Long live JUMUWATA

Picha
Leo ni siku ya kuadhimisha maendeleo ya blogu Tanzania. Maadhimisho haya yalianza rasmi mwaka juzi, kwa makubaliano ya wanablogu wenyewe walipokutana kwa mkutano mkuu wa kwanza wa mtandaoni. Soma blogu hii hapa kwa maelezo zaidi. Kusema kweli tuna kila sababu ya kufurahia kuanzishwa kwa jumuiya hii muhimu ya kutuunganisha. Siku hii haikupaswa kabisa kuwa hivi ilivyo leo. Kwamba kila mmoja anasherehekea kivyake vyake si jambo la kujivunia sana. Kwa wanablogu wapya, ni vyema kufahamu kuwa tunayo jumuiya yetu yenye viongozi waliochaguliwa kwa kura. Angalia majina yao hapa . Napenda kumpongeza sana Kitururu kwa kazi kubwa aliyoifanya akishirikiana na wenzake. Najua anayo majukumu mengi ya kufanya. Lakini bado hajasita kujitolea kwa faida ya wote. Yupo Da Mija mwamke wa shoka ambaye juhudi zake za kujitolea zimeipeleka mbele jumuiya yetu. Ndesanjo mzee wa kujikomboa. Majukumu nayo bila shaka yamembana. Historia inamkumbuka. Mwenyekiti wetu blogu yake haipatikani. Sijui kilichotoke...

Mchango wa msomaji

Jana kuna mchango wa mawazo niliupata kutoka kwa msomaji Prosper Mwakitalima. Huyu ni mwanafalsafa na rafiki yangu wa siku nyingi. Mjadala wetu ulikuwa katika hoja ya nguvu kuu iliyozungumziwa na Kamala. Anasema: "...Kwamba tunapofikia kuamini kuwa ipo nguvu kuu kwa sababu ya kushindwa kuamini kuwa viumbe vyote na asili yake visingeweza kujiratibu vyenyewe, na hapo hapo tukakubali kuwa nguvu hiyo haina chanzo, na mwisho wake hauelezeki, tunashindwa vipi kuamini kuwa hata viumbe navyo vimekuwapo vyenyewe bila nguvu fulani kuu zaidi? Kwa sababu kama tunaamini kuwa hiyo nguvu haina chanzo, kwa nini tushindwe kukubaliana kuwa hata viumbe navyo vyaweza kuwapo bila chanzo?..." Hiyo ni changamoto nyingine inayohitaji majibu. Najua anachokoza mawazo kwa lengo la kutufikirisha zaidi. Nimetangulia kukujulisheni kuwa yeye ni mwanafalsafa mwenye dini.

Zimebaki siku tano...

Tarehe kumi na nane mwezi huu ni siku ya maadhimisho ya wanablogu. Tukumbushane kushiriki. Mambo kama haya yasionekane madogo kihivyo. Yanatunganisha. Tujiandae.

Kaluse mwanablogu wa utambuzi

Je, unaujua utambuzi? Kama sivyo, basi ujio wa huyu mwanablogu mpya utakupa majibu. Bonyeza hapa umsome . Anazungumzia mambo yanayohusu nafsi zetu. Saikolojia. Binafsi nimependezwa na ujio wa mwanablogu huyu. Naamini utapenda kumsoma na kujadiliana na wasomaji wengine humo.

Hakuna kujifunza bila kutofautiana kimawazo

Ni Jumapili nyingine njema. Hatuna budi kukumbushana kwamba siku ndo zinaenda hivyo. Siku ya tisa leo. Zinaenda. Bado siku chache tuelekee kwenye mwezi wa lala salama. Mwezi wenye sherehe nyingi kuliko utekelezaji wa mipango ya wanajamii. Siku zinakatika. Kwangu Jumapili ni siku ya kupumzika kwa asilimia mia moja. Sababu ni kwamba katika siku sita za juma huwa ninabanwa kisawasawa na dunia. Kwa hiyo Jumapili kwangu ni siku ya kujisomea ninavyovitaka. Kulala. Stori. Kula. Alimuradi tu kufurahia mwisho wa juma. Nimekuwa nikitafakari michango kadhaa ya wachangiaji wa blogu hii hasa kwenye makala za uwapo wa Mungu. Najua kila mtu anao mtazamo wake. Japo najua watu wengi hawajajaliwa kuweka wazi mawazo yao hasa inapokuja suala lenye utata kama hili. Nawashukuru waliomajasiri kujaribu kuchokoza mawazo ya wengine. Kuchokoza mawazo si kazi rahisi. Nilikuwa napitia pitia niliyopata kuyaandika. Basi nikapata makala hii niliyoiandika miaka miwili iliyopita. Ilihusu biblia na imani zetu. Hiy...

Kutoka maktaba: Laana? Ama?

Haya nikurudishe nyuma kidogo. Twende kwenye kumbukumbu zetu. Soma makala hii: Hivi waafrika ni kweli tumelaaniwa? Kumbuka sikuwa nimehitimisha. Nilikuwa katika tafakari tu. Usinielewe vibaya kama baadhi ya watu wengine walivyofikiri. Soma katikati ya mistari.

Tofauti ya Magharibi na Kusini

Natafakari tofauti hasa iliyopo kati ya mataifa ya magharibi na kusini. Wakati Zimbabwe kura zinapigwa na mwezi unakatika ndo matokeo yafahamike...wakati Kenya inachukua majuma kadhaa...wakati Bongo unaelewa mwenyewe...Marikani imechukua masaa kadhaa matokeo yamejulikana. Na si tu masaa hayo, lakini mshindwa anatoa kauli ya moja kwa moja kwamba aliyeshinda kashinda. Anampongeza. Mimi sielewi. Hivi tofauti hii inatokana na nini? Umasikini? Uroho? Ujambazi? Ama ni ujinga flani mukichwa? Sielewi. Hivi sisi ndugu zangu tumepungukiwa nini hasa? Mwenyezi Mungu alitunyima nini sisi wanadamu wa dunia ya sita? Kuna haja ya kujielewa. Ipo haja hiyo.

Je, kuna Mungu? - Mchango wa Nuru Shabani

Kuna wachangiaji wananiandikia kwa barua pepe. Sijui ni kwa nini wanataka tujadiliane sirini. Nadhani tukijadili waziwazi inapendeza zaidi kwa faida ya wasomaji wengine. Hapa ninao mchango wa Nuru Shabani kupitia kisanduku cha maoni. Kwa kuheshimu mchango wa msomaji huyu, naomba niupandishe hapa uusome. "...Ningependa kuungana na Kamala kuwa hakuna kitu kinachoitwa Mungu,kama wengi tulivyoambiwa. Zamani kabla hawajaja wakoloni(wazungu na waarabu) hakukuwa na kitu kinachoitwa Mungu,wao waliamini ktk Nguvu kuu.Ndiyo maana utakuta wengine waliamini ktk miti wengine katika majabali,na kikubwa ndugu zangu ieleweke wengi wa watu wa zamani waliamini zaidi katika kanuni za kimaumbile ndiyo ilikuwa msingi wao. Kwa mtazamo wangu wengi hatumwelewi mungu sana tunachofanya ni kujenga hofu kwa Mungu,linapokuja suala la kutaka kumjua huyo mungu kwa undani utaambiwa unakufuru,sasa mi huwa ninajiuliza iweje utake kujua asili za aliyetuumba uambiwe unakufuru? Haingii akilini umuulize mzazi w...

Je, kuna Mungu? - Mchango wa Kamala

Haya. Nashukuru kwa michango ya wasomaji kuhusu hoja ya uwapo wa Mungu. Ufuatao ni mchango wa Kamala mwanablogu machachari anayepatikana hapa . Yeye anasema: " Kwa vyovyote kuna nguvu inayoendesha haya mambo, kuna nguvu ambayo ni ya ajabu katika hufanyaji kazi wake. nguvu hii wakristo huuita Mungu na waislamu huiita Allah, kila mtu hujiona yuko sahihi lakini wanasayansi ndio basi kwani wao huiita Nguvu tu kama ilivyo. siku zote wanasayansi hukataa kuwepo kwa mtu anayeitwa Mungu lakini hukubali kuwepo kwa nguvu na wanasema kuwa nguvu haiwezi kubadirishwa wala kuharibiwa na wala kupindishwa! uwepo wa nguvu unaonekana tu wenyewe, biblia inasema tumeumbwa kwa mfano wa Mungu kwa hiyo basi na sisi ni nguvu au Roho kama ilivyo hiyo Mungu. sisi kama binadamu mawazo yetu, maneno (kauli) yetu, yananguvu kuliko tunavyofikiri na hubadirisha na kutupangia maisha yetu. kwamfano, Tanzania sio nchi masikini na wala watanzania sio masikini bali ni nguvu ya Hoja ya watu fulani na sisi kuipo...

Je, kuna mungu?

Hakuna mjadala kwamba kila jamii inaamini katika Mungu. Hata kama tafsiri hasa ya mungu huyo hutofautiana kutoka jamii moja hadi nyingine, lakini ukweli unabaki kuwa kila jamii inaamini katika mungu. Ningependa tujipe nafasi ya kujadili dhana ya Mungu katika jamii kwa mtazamo usio wa kigomvi wala kulazimishia majibu kwa kutumia imani tulizonazo. Najua dini zetu zilituzuia kujiuliza maswali ya msingi kama haya. Zinatulazimisha kuamini hata kama hatuelewi. Na tunapojaribu kufanya hivyo, tunaambiwa, tunakufuru. Siamini kuwa kujadili jambo kwa nia ya kulielewa ni kukufuru. Tunaishi katika kizazi kinachotaka ushahidi zaidi kuliko imani. Kwa hiyo hapa ninayo maswali ya kuuliza: 1. Je, Mungu yupo? 2. Na kama yupo, nini kinatufanya tuamini hivyo? 3. Je, ni kweli kwamba sayansi inamkana mungu? Nadhani kujielewa ni pamoja na kupata majibu ya maswali haya kwa ufasaha.

Fahamishwa na nifahamishe.com

Kuna tovuti mpya inatangazwa. Nimeipitia. Ina kiingereza na kiswahili. Kwa mujibu wa waendeshaji wake, tovuti hiyo imebeba mambo mengi ya kukuhabarisha ndugu msomaji. Wanayataja: "Habari mbali mbali za Tanzania na za kimataifa, Habari katika picha na video, Live radio, Online Game, Habari za burudani na wasanii wa bong, Utaweza kusikiliza nifahamishe nonstop bolingo na lingala mix, Kuuza kwa kuweka tangazo lako bure au kununua nyumba, magari, vitu vya electronics na kadhalika, Kushare picha na watanzania duniani na kadhalika". Gonga hapa kuwatembelea ujionee mwenyewe.