Mazoezi ya kusikiliza wanafunzi wangu

Miezi kadhaa nilikuwa nawafundisha (soma kuwasikiliza) wanafunzi fulani. Niliwapenda vijana wale. Kuna siku nitasimilia zaidi habari zao.

Nilibahatika kuwafundisha ile mada katika Biolojia ambayo (ikifundishwa vyema) huwafanya wanafunzi wajifunze kufikiri. Mada yenyewe inaitwa organic evolution. Basi. Mimi ni kati ya wanaoamini kuwa kazi ya mtu aitwaye mwalimu si kufundisha bali kuongoza mijadala.

" Mnafikiri viumbe na kila kilichomo katika dunia pamoja na dunia yenyewe vilitokea wapi?" Niliwauliza. Bila shaka unaweza kuelewa walijibu nini.
" Sasa (Mungu) aliumbaje viumbe?" Nikawauliza.
Mmoja akajibu kwa haraka: " Kwa nguvu zake(Mungu)...maana anao uwezo wote" Maneno mengine siyakumbuki. Kufupisha ilibidi nijie kwa njia hii:
" Kwani huyo mnaye mwita Mungu alitokea wapi?" Wakashangazwa sana na swali la kijinga namna ile. Hawakulitazamia kutoka kwa mtu waliyemheshimu kama mimi. Mwalimu wa mazoezi. Huku nikijua kabisa wanahangaika kunilewa, ikabidi nigeuze kabisa sentensi hiyo kwa kiswahili kamili. (Maana sa nyingine huwa unahisi kabisa hawaelewi ingawa wanatamani kiingereza cha uongo na kweli). Nikarudia: " Mungu mliyeniambia kaumba dunia yeye kaumbwa na nani?"

Mmoja ambaye nilishabaini kwa wiki hizo mbili tangu niwe hapo kwamba ana kichwa kizuri, akanyanyua mkono: " Yeye hakuumbwa. Alitokea tu." Haya.
" Sasa kama yeye katokea tu, nina kosa gani nikisema na viumbe navyo vilitokea tu?...kwa sababu ushahidi wa viumbe kuumbwa ni wa kuaaminika tu...Mnaonaje tukifikiri kuwa na navyo vilitokea tu?"

Ilikuwa kasheshe. Lakini mpaka leo wale vijana wananiandikia. Somo la evolution likawa sababu ya mijadala ambayo huwa siamini kuwa ilitoka kwa wanafunzi. Kumbe yale hayakuwa mazoezi ya kufundisha, bali mazoezi ya kusikiliza. Nilijifunza mengi.

Maoni

  1. Kusikiliza bomba la shule.Tatizo wengi wetu tunafikiria ni ujanja kuwa muongeaji zaidi ya kuwa msikilizaji.

    JibuFuta
  2. Nakubaliana na wewe Simon. Ila kuwa mwalimu msikilizaji ni kazi nzito na ngumu kuliko kuwa mwalimu mzungumzaji.

    JibuFuta
  3. Nikarudia: " Mungu mliyeniambia kaumba dunia yeye kaumbwa na nani?"

    Mmoja ambaye nilishabaini kwa wiki hizo mbili tangu niwe hapo kwamba ana kichwa kizuri, akanyanyua mkono: " Yeye hakuumbwa. Alitokea tu." Haya.
    " Sasa kama yeye katokea tu, nina kosa gani nikisema na viumbe navyo vilitokea tu?...kwa sababu ushahidi wa viumbe kuumbwa ni wa kuaaminika tu...Mnaonaje tukifikiri kuwa na navyo vilitokea tu?"

    Mr., Mungu hakutokea tu. mungu alikuwepo, yupo na atakuwapo milele!

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Haiba ni nini?

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Makundi Manne ya Tabia za Watoto Kitabia

Uislamu ulianza lini?