Mwanaume anapokimbia 'kelele' nyumbani
Mwanadamu ana uwezo mkubwa wa kuficha tabia. Samahani. Namaaminisha mwanaume. Unajua, katika jamii zetu, ni aibu mwanaume kukiri mahusiano yamekushinda. Kuliko kuitwa kila aina ya majina saa nyingine tunalazimika kujenga taswira ya ukamilifu hata kama kiuhalisia tunaugulia maumivu makali. Jumlisha hapo dini, kwa maana ya hizi itikadi za ufuasi wa halaiki, kiwango cha kuonesha ukamilifu lazima kiwe juu zaidi. Tumeaminishwa ndoa ni kielelezo cha ukamilifu. Hakuna kukosea. Ukishasema una changamoto na mwenzako, watu wanakupiga jicho la dhihaka, “Hukumwomba Mungu akupe mke? Humtegemei Mungu vya kutosha?” Nani yuko tayari kuonekana hana uhusiano mzuri na Mungu? Kwa upande mmoja, ninamuelewa sana Godi. Hofu ya kuchafua jina lake inamfanya aigize amani ya ndoa isiyokuwepo. Swali nililojiuliza, kwa nini sasa Godi amefikia mahali hajali watu wa nyumbani kwake? Kama ana tatizo na mkewe, inakuwaje anashindwa kujali hata watoto? Kila tabia, kwa ...