Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari, 2009

Fumbo mfumbie mwerevu

Kwa sasa sipatikaniki vya kutosha kwa sababu ambayo nitaieleza hapa chini kwa maneno matano. Kwa wale wanaopenda chemsha bongo mnaweza kujaribu na kisha kuweka majibu kwenye kisanduku cha maoni ama kuniandikia kupitia sanduku la barua pepe: Meelekezo: Hizi ni herufi zilizofichwa (codes) ambazo ili kukupa ujumbe, inakubidi kugundua kanuni iliyotumika kuziandika ili kupata maneno matano ya kiswahili fasaha. OJUBLVXB OB OJUIBOJ KVNB MJKBMP! Chemsha ubongo kidogo ndugu msomaji.

Kosa nambari moja

“Kwa nini uliamua kusoma hayo unayoyasoma?” “Basi tu napenda, hata sijui kwa nini...ila nahisi ni kwa sababu niliyafaulu vizuri zaidi kwenye mtihani wa kidato cha nne…” “ Kwani unafikiri kuwa nani baada ya masomo yako?” “…Hata sijui…mambo yatajipanga yenyewe!...” “ Yatajipanga yenyewe? Sasa ukijakugundua baadae kwamba unataka kuwa mhasibu, na wewe sasa hivi unasoma Fizikia na Kemia…huoni kwamba utakuwa umepoteza muda wako bure kusoma mambo ambayo utaachana nayo?” “ Ujue future inajipangaga bila kutegemea umepanga nini. Na isitoshe kubadili fani si jambo la ajabu…” Kwa hivyo unakuta sababu hasa zinazowafanya wanafunzi kufanya maamuzi ya michepuo yao, haziridhishi. Maamuzi ya nitasoma nini hutegemea zaidi ushauri wa wazazi (wanaoongozwa na kiu ya pesa ambao wao wenyewe wameshindwa kuzipata), mkumbo wa marafiki –rika (wanaoongozwa na hamu ya kujitafutia sifa nyepesi nyepesi kwenye jamii) na sababu nyinginezo. Ni bahati mbaya sana kwamba katika nchi yetu, pamekuwapo na juhudi ...

Nchi yetu inatengeneza aina gani ya wasomi?

IMEKUWEPO mijadala mingi kuhusu mfumo wetu wa elimu. Mijadala hiyo inatokana na watu wengi kuamini kwamba elimu yetu ina hitilafu kubwa. Elimu yetu ni wazi kuwa bado haijaweza kukidhi vigezo vya haki vya elimu ya kweli. Elimu ya kweli, kwa hakika inabadilisha maisha ya watu wake. Elimu ya kweli haitufanyi tujidharau. Elimu ya kweli haitufanyi tujipuuze sisi wenyewe pamoja na utamaduni wetu. Elimu ya kweli haitufanyi tuwe dumavu, watu wasiofikiri zaidi ya mtihani. Kwa hivyo, kwa wengi wetu mfumo wetu wa elimu, kwa hakika, hauna ubavu wa kutosha kutuletea uhuru wa kweli wa fikra na maendeleo. Mfumo wetu wa elimu unahitaji kubomolewa. Tukiisha kuubomoa, tushiriki kuujenga kwa upya. Tangu awali, mwanafunzi wa ki-Tanzania hajengwi kusoma zaidi ya mitihani. Mwanafunzi wa ki-Tanzania hatengenezwi kuchambua mambo, badala yake anajazwa 'maarifa' kiasi cha kushindwa kuyapambanua. Kwa hiyo unakuta purukushani kubwa madarasani inakuwa ni namna ya kupata alama A ni si vinginevyo. Za...

Kama sio utumwa ni nini hiki?

Habari za siku ndugu msomaji. Binafsi sijambo. Nafurahi kurejea kibarazani baada ya heka heka za huko na huko. Itoshe kuhusu mimi, nikukaribishe tena humu ndani. Leo ningependa kukusimulia kisa kimoja. Nikuase kwanza, kwamba usilazimike kunielewa vibaya. Sijawa na tabia ya kuona makosa zaidi niwapo mahali ama nikutanapo na watu. Maana siamini kwamba binadamu ana kazi ya kushabikia makosa kuliko jema moja. Nisijitetee sana. Jumapili hii nilipata fursa ya kuhudhuria ibada kwenye kanisa la 'kisomi'. Washirika wa kanisa hili, wengi wao ni wale ambao umande haukuwazuia kuhudhuria shule. Wamesoma. Pamoja na ukweli kwamba wote walikuwa weusi kama mimi, lakini ilikuwa bayana kwamba kiingereza kilikuwa 'nguzo' ya ibada hiyo. Hilo halikuwa tatizo kwangu. Maana inaeleweka kwa wengi wetu kwamba, kusoma kunathibitishwa na umahiri wa kusema kiingereza. Nshazoea hili. Pamoja na ukweli kwamba kiuhalisia kiswahili ndicho kinachotawala madarasani lakini watu hatutaki kuukubali ukweli...

Je, majina yetu hayawezi kubeba falsafa zetu?

KUNA hili suala la majina yetu. Inafahamika wazi kwamba tunapozaliwa, mara nyingi shughuli ya kwanza kabisa inayofanywa na wazazi, ni kutupatia majina 'yao' wanayojisikia kuwa yanatufaa. Tunajikuta kama ambavyo tunarithi dini za wazazi wetu bila kuhoji, na majina nayo tunayabeba mazima mazima. Majina haya mara nyingi tunayapewa bila tafakuri ya kina. Wazazi wanaamua tu wengine ni kwa sababu ya matukio ya wakati huo mtoto anazaliwa bila kujali atakavyojisikia mtoto pale atakapojielewa yeye mwenyewe ukubwani. Kwa mfano, mtoto anaitwa Matatizo, au Masumbuko, ama Shida na majina kama hayo. Mtoto huyo anapokuja kubaini kuwa jina alilopewa na wazazi wake halikuwa na nia nzuri ndani yake na hivyo kuleta hisia za ubashiri wa aina ya maisha atakayoishi, hapo ndipo mparaganyiko huanzia. Na wengine hupewa majina mazuri, lakini ni ya kigeni, yasiyo na uhusiano na utamaduni wetu. Ni majina yanayoitwa ya dini, na pengine tunayafurahia lakini kimsingi yakawa kielelezo cha utumwa wa ...

Kuna haja yoyote ya kutokuwa na dini?

Tumekuwa tukijaribu kujadili masuala ya dini. Hili ni jambo jema sana kwa ukombozi wa fikra zetu. Mwaka juzi tulifanya hivyo pale kwa Ndesanjo . Unaweza kubonyeza hapa kuusoma mjadala huo uliohusu dini na imani . Hivi karibuni, Koero aliufungua na kuufunga mjadala wa aina hiyo hiyo. Naomba sasa tujadiliane kwa kina suala hili kwa minajili ya kupeana changamoto pamoja na kuelimishana inapobidi. Je, dini chimbuko lake ni nini? Je, dini inayo uhusiano wowote ule na Mungu? Je, bila dini hatuwezi kumwona Mungu? Na je, kutokuwa na dini kunawezekana? Angalizo: Mipaka ya tafsiri ya Mungu katika mjadala huu, inabaki kuwa maoni ya mchangiaji husika.

Padre Karugendo kakosea kipi hasa?

Picha
Mwandishi machachari na mwanafalsafa anayeheshimika kwa uchambuzi makini, Padre Privatus Karugendo (pichani) amevuliwa daraja la Upadre. Habari hizi si njema na ni za kusikitisha sana. Yeye mwenyewe amenukuliwa akisema kuwa hautambui uamuzi huo ambao anaamini umefanyika kwa misingi ya chuki za watawala wa kanisa hilo. Nimeshtushwa na habari hizi kwa sababu kwanza nimekuwa mfuatiliaji wa makala zake kwa maika mingi tangu enzi za Rai ya zamani, na sasa Raia mwema pamoja na Tanzania Daima . Na kwa majuma kadhaa Padre Karugendo amekuwa akiandika mtazamo wake kuhusu namna kanisa la Katoliki (hasa la Afrika) linavyoendeshwa. Yeye anasema watawala wa Kanisa wanatutawala badala ya kutuongoza . Kama na wewe ni msomaji mzuri wa makala zake utakubaliana nami kuwa Padre Karugendo mara zote ameonyesha wazi kuwa Padre anayetaka mabadiliko. Mara zote amejitahidi kuwa yeye zaidi kuliko 'kuigiliza' misimamo asiyoiamini yeye. Si mara moja nimesoma akitofautiana na wakuu wake wa dini kwe...

Baada ya migomo mwaka jana...

Heri ya mwaka mpya. Bila shaka ulipata fursa nzuri ya kuupokea mwaka huu popote ulikokuwamo. Naamini si tu kwamba uliupokea mwaka kwa madebe na fataki, lakini pia ulipata fursa ya kuyaandika malengo na matarajio yako kwa mwaka huu tena. Kama hujafanya hivyo bado, hima, naufanye hivyo sasa. Ningependa kuamini kuwa mwaka huu utakuwa wa kasi kubwa kwa blogu zetu. Naamimi mwaka huu wanablogu watakuwa pamoja zaidi kuliko ulivyokuwa mwaka jana. Naamini mwaka huu tutakuwa na mijadala tofauti tofauti zaidi kuliko ulivyokuwa mwaka jana. Wenye kujadili siasa watafanya kwa ufanisi zaidi. Wenye kamera zao watazitumia kwa ufanisi zaidi. Wenye kujadili mambo ya kijamii watafanya hivyo kwa moyo zaidi. Wale wa mambo ya falsafa na kila aina ya maarifa watafanya hivyo kwa bidii zaidi. Almuradi kila eneo, naamini kuwa litapata wabobezi. Ili kulifanya jukwaa la blogu kuheshimika zaidi. Blogu ziwe ukumbi muafaka kwa kila mwenye wazo na maarifa ya kuwashirikisha wengine. Mwaka uliopita ulichukua sura ya...