Ni kweli, Fossils, mabaki ya viumbe wa kale ni ushahidi wa Evolution?
Msomaji mwenye historia ya elimu ya viumbe anaweza kuuliza: Uhusiano tunaouona baina ya viumbe (phylogenetic relationship) una maana gani? Kusema kweli, viumbe wanaonekana kuhusiana kwa karibu. Na uhusiano huo unaleta mawazo kuwa huenda kila kiumbe ametokana na mwenzie. Kwa mfano inavyoonekana, maisha hasa ya viumbe yalianzia baharini. Kwa maana hii, viumbe wa kwanza waliishi majini wakibadilika badilika na kuishia kufanya aina nyingine ya maisha yasiyotegemea maji, yaani maisha ya nchi kavu. Sasa katika kuangalia mlolongo huu, tunaambiwa viumbe walijikuta wakijiongezea “viungo” (adaptive features) vilivyowawezesha kukabiliana na aina vyingine ya maisha. Kwa ule mfano wetu wa samaki, ni kwamba baadhi ya samaki walianza kupoteza uwezo wao wa kupumua kwa kutegemea maji, na badala yake, wakaanza kuwa na vitu kama mapafu vilivyowasababisha kugeukia maisha nje ya maji. Baadae makoleo yao yaliyotumika kuogelea (fins) yakatengenezeka kuwa (miguu?) ili waweze kuishi vizuri nchi kavu. Na...