Udhaifu wa sayansi (1)
Haya tuendelee. Tunahitaji aya nyingi kufafanua dhana ya sayansi. Kwanza nijitete kwamba sina msamiati wa kutosha kukwepa maneno yanayoitwa ya kisayansi ila nitajaribu kadiri niwezavyo. Kwa uchache sana, na katika lugha rahisi zaidi, sayansi ni namna ya upatikanaji wa maarifa kwa njia ya utafiti. Utafiti hapa humaanisha majaribio ambayo hukusudiwa kuchunguza na hatimaye kuthibitisha ama kukanusha bashiri ya kisayansi. Sayansi hutumia mbinu katika kuchunguza dhana, ili kuongeza maarifa ama kurekebisha maarifa yaliyopo. Huanzia katika ukusanyaji wa ushahidi unaochunguzika, unaopimika, na wenye chanzo mahususi kinachokubaliana na ufahamu wa kawaida. ( Sina masamiati sahihi sana ). Ushahidi huo, ndio kile kinachoitwa data, ambazo hupatikana kwa majaribio ambapo bashiri hujengewa hoja ili kufanyika maelezo ya dhana iliyokuwa ikichunguzwa. Majaribio haya hupangiliwa kitaalamu kwa kutumia vibadiliko (variables) ili kuzijaribu bashiri za awali. Majaribio haya hufanyika katika ma...