Ninapoahirisha mafanikio yangu kwa "kukwepa" kuamua
Mambo mengi yenye matokeo mazuri, si rahisi kuyafanya. Hasa ikiwa utekelezaji wake unadai utashi, “usilolazimishwa” na mamlaka iliyo nje na mtu mwenyewe. Ugumu wa mambo haya, ni zile zinazoonekana kuwa gharama za papo kwa hapo, zinazoweza kutukwaza tukate tama ya kufanya yale tuyapendayo. Matokeo ya haya yote, ni kujikuta tukiishi maisha yasiyo na utimilifu. Maisha yasiyo yetu. Pengine uliwahi kusoma maneno ya mtu mmoja aitwaye Albert Gray yanayosema: The successful person has the habit of doing things failures don’t like to do. They don’t like doing them either necessarily. But their disliking is subordinated to the strength of their purpose. Nukuu hii imekuwa na maana tofauti kwangu. Kwamba kile ninachokiona kwamba kana kwamba hakivutii kukifanya, ndicho chaweza kufanyika utimilifu wa ninachokikusudia. Mambo gani ambayo unajua ni ya muhimu yafanyike lakini unayaahirisha? Ni mangapi mazuri unayakosa kwa kule tu kukwepa kulipia gharama ya kuyatekeleza hayo unayoyaona kuwa ni ...