Tuiamini sayansi? Au ni ghiliba tu?
MIONGONI mwa maeneo ambavyo sayansi imekuwa ikijihusisha nayo, elimu ya viumbe ni mojawapo. Unapozungumzia viumbe unalazimika kuanzia na uhai wenyewe, Uhai ulitokea wapi? Tunaambiwa baharini mahala ambapo viini urithi viitwavyo DNA vinaaminika kutokea kirahisi rahisi. Bahari nayo ilitokea wapi, tunajibiwa utafiti bado unaendelea, tuvute subira. Dunia yenyewe ilitokea wapi, hapo nako tunaambiwa wanaotaka kufanya Shahada ya uzamifu, wazame. Hapo hatujauliza ulimwengu uliobaki (universe). Jambo moja ni wazi. Kuwa katika sayansi, mambo yanapokuwa magumu, rufaa huwa: TUNGOJE, maarifa hukua taratibu! Lakini ni ukweli kwamba kauli hii ni kichaka kile kile cha kukimbiwa maelezo. Tukiachana na asili ya uhai, sayansi inajaribu “kupendekeza” nadharia ya utokeaji wa idai tofauti tofauti ya viumbe tulivyonavyo leo. Mahala pa kuanzia ni kwamba inavyoonekana viumbe vyote vinavyo asili moja (common ancestry). Asili hiyo ilibadilika na kufanya viumbe kwa wingi tuuonao leo. Msingi hapa ni...