Bongo flava imevamiwa na wababaishaji
Siku hizi raia wanapambana na ufukara wao kwa mbinu nyingi.Zipo zilizo halali na hali kadhalika zipo zilizo haramu. Ndio maana utaona kuwa tatizo la ujambazi limekuwa likinona na kunenepa kila uchao. Watu wanatumia nguvu kunyanganya mali za wengine, mchana kweupe. Watu wanavunja nyumba za watu, wanachukua (iba) kila kilichomo mumo. Usije ukadhani kuwa wanapenda, ni mfumo unawalazimisha kutenda matendo hayo bila hiari. Ashakumu si matusi, afadhani ujambazi huu kuliko "ule mwingine" unaofanywa na wachache wanaodhani wana meno kuliko sisi kwa kutumia ile iitwayo demokrasia. Katika kukabiliana na ukata wa maisha, siku hizi kumeibuka kundi la vijana wengi wakilazimika kujiunga na miradi ya shughuli za usanii wa aina kadha wa kadha. Muziki mpya, maarufu kama Bongo flava, ukiwa ni moja wapo. Ni mradi usiodai gharama kubwa kama vile elimu ambayo siku hizi haipatikani kiurahisi. Kimsingi, hii ni njia halali ambayo faida zake si haba. Kwanza, ingawa haijawa ajira iliyorasmishwa, imekuw...