Madhara ya Kutoa Ushauri Kienyeji na Kuugeuza Unasihi kuwa Ushauri

Utamaduni wa (kutoa na kuomba) ushauri umejengeka kwenye misingi ya hekima ya wazee walioona mengi, uzoefu wa mtu mzima unaompa uhalali wa kutoa mwongozo wa kufuata kwa anayemzidi. Hata tunaposikia unasihi (counselling), aghalabu, mawazo yetu yanaenda kwenye taaluma ya kushauri watu na kuwaambia cha kufanya ili kutatua matatizo yanayowakabili. Wapo, tena wengi, wanaotafsiri ‘counselling’ kama ushauri. Counselling sio ushauri. Katika makala haya, ninajenga hoja kuwa kutoa ushauri ni jambo la hatari na kwamba linaweza kusababisha madhara makubwa kwa anayeshauriwa lakini pia hata anayeshauri. Kadhalika, ninalenga kuonesha, japo kwa ufupi kuwa hata kwenye unasihi msingi wa kwanza wa kuzingatia kwa mtoa huduma (aliyefuzu) ni kuepuka kabisa kutoa ushauri kwa mtu. Nakusudia kuonesha nini hasa huwa ni malengo ya unasihi. stefanamer/Getty Images Ushauri ni nini? Unaposema unamshauri mtu unakuwa na maana gani? Ushauri, kwa kifupi, ni maelekezo mahususi unayompa mtu, maamuz...