Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2011

Kuwa mwenye furaha ni uamuzi wako mwenyewe!

Picha
Ni mara ngapi umewahi kukutana na mtu aliyekukwaza kiasi cha kumtupa katika kapu la “watu wa hovyo” wasiostahili heshima kama binadamu? Umewahi kupatwa na tukio ambalo lilibadili kabisa mtazamo wako kuhusu maisha, watu na maisha kwa ujumla? Kwa nini watu kukata tamaa? Umewahi kuwaza kwa nini kinachomkwaza huyu si lazima kimkwaze yule? Umewahi kuonana na mtu anayeshangaa inakuwaje “huyu bwana achukue uamuzi wa ajabu namna ile” wakati kilichotokea kinachukuliwa na wengi kuwa “ni jambo la kawaida”? Natamani ukimaliza kusoma hapa uelewe kwamba sehemu kubwa ya matatizo tunayokabiliana nayo kama binadamu kila siku, tunayasababisha wenyewe. Na kwa yale tusiyo naudhibiti nayo, tunaweza kubadili mtazamo wetu kwayo, na hilo linaloonekana kuwa tatizo ama likawa si tatizo au likabadilika kuwa changamoto. Wengi wetu tunapokumbana na vikwazo (ambavyo mara nyingi huwa ni watu, vile mambo yalivyo na matukio yanayokuwa katika namna tusiyoitegemea) hujenga mawazo kwamba vitu hivyo vi vibaya. Mato...

Wanablogu wanasemaje kuhusu utaratibu wa "Kutuzwa"?

Picha
Tangazo lilianzia hapa kwamba kuna mwuungwana -japo hakuwa anafahamika jina lake wala mahali aliko- kapata wazo la kutunuku kazi za wanablogu. Huenda hili bado halijulikani kwa wanablogu wengi kama ilivyokuwa kwangu kabla ya kusoma posti ya mwanablogu matata, Bw. Mubelwa Bandio juma lililopita. Blogu ya mwandaaji wa Tuzo hizo inajinadi kwa maneno haya: "...Our wish is to help bloggers to success, beat the odd and push past their limitation. We believe bloggers can play an important role keeping their places, villages, towns, cities or countries visible. Tanzanian Blog Awards is another opportunity to showcase your blog to the world and get some free traffic and subscribers..." Pamoja na kupongeza wazo hilo (la kuandaa tuzo kwa wanablogu), Mubelwa Bandio alionyesha wasiwasi wake ikiwa zoezi hilo litafanyika katika mazingira ambamo masuala ya msingi kuhusu blogu hayajafanyiwa kazi. Kwamba blogu zinaeleweka vyema kwa wadau (wateuzi na wateuliwa), hilo lilimtia mashak...