Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2010

Mhe. Zitto ni mwanablogu

Picha
Pamoja na kutumia nyenzo za uandishi wa kiraia kama twitter, facebook na majamvi ya kijamii kama Jamiiforums nk, Mhe. Zitto Kabwe ni mwanablogu. Na blogu yake imesheheni elimu na maarifa ambayo tunayahitaji kwenye majikwaa haya ya kiraia. Ameitambulisha blogu yake siku chache zilizopita (tarehe 25 Mei) kwa maneno machache yafuatayo: "Ndugu msomaji, nimekuwa na blogu hapo kabla lakini sikuweza kuifanyi kazi kama invyostahili. Nimeamua kuanzisha blogu hii mpya ili liwe jukwaa la kujadiliana jinsi ya kuimarisha demokrasia nchini kwetu Tanzania, Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla. Karibu kwa maoni, ushauri na hata makatazo!" Bonyeza hapa kumsoma , halafu uone namna mwanasiasa huyu kijana alivyotofauti na wanasiasa wazee wasiojua kingine zaidi ya redio na magazeti ya kila wiki. Hawajui kwamba zama hizo zilishapita na hazitarudi tena. Karibu sana Mhe. Zitto.

Ni usalama wa Taifa au ni ubaguzi wa rangi?

Picha
Tuko ndani ya uwanja wa ndege wa Sao Paulo, Brazil. Ni usiku, tunangoja usafiri wa kwenda Dubai, kama lisaa limoja lijalo. Nimekamata kitabu changu nasoma. Ni kitabu cha rafiki yangu kanigawia nionje yaliyomo. Yeye naye kakaa zake kimya anasoma kitabu changu pia. Saa nyingine tunafunika vitabu, tunazungumza mawili matatu, tunaendelea kupekua pekua. Ni katika kuongoja tu usafiri. Faizul, Deo, Bijoy, na mimi jijini Sao Paulo. Picha: Dr Awab Mara wanatufuata watu wawili waliovaa kiraia. Mmoja kajazia, kajichora tatuu mkononi, kavaa viatu vinavyompyaya. Mtu wa mazoezi. Mwingine mdogo dogo tu, ila shida yake hasemi kiingereza. Kwa hiyo ni "mpole fulani hivi". Baunsa anatuonesha kitambulisho chake. Ni askari wa Kibrazil. "Ninaomba kuona hati yako ya kusafiria tafadhali?"askari bonge ananiambia, mwenzie akimsaidia kwa macho. Nilisita kidogo, nikijiuliza inakuwaje aje kwangu wakati nilikuwa na wasafiri wengine. Ndicho nilichomwuliza. Baada ya kudai kuwa anafanya ...

Blogu zakutanisha wanablogu...!

Picha
(picha mali ya Mtanga wa Mwananchi mimi) Habari za kukutana kwa wenzetu watano nilizipokea kwa furaha kubwa. Hii kwa hakika ni hatua kubwa na ya kupigiwa mfano. Bila shaka, kama wanavyofikiri wanablogu wengine, huu utakuwa mwanzo mzuri kwa wengine wetu tukukutana mmoja mmoja na hatimaye wote kwa wakati mmoja kama walivyofanya wenzetu hawa. Hongereni sana Mwananchi mimi , Hadubini , Mtambuzi , Lundunyasa na Chacha Wambura kwa kutuonyesha njia. Wapo watu wanadhani matumizi ya majina bandia yanawasaidia. Niliona mjadala fulani kwenye mtandao wa Jamii forums ambao kwa kweli ni vigumu wanachama wake kukutana kama walivyofanya wenzetu. Bonyeza hapa uone na utafakari. Tuachane na hao wasitaka kufahamika. Turudi kwa wenzetu waliweza kuutumia mtandao mpaka wakaweza kukutana siku ile. Hivi ndivyo Ndugu Fadhy anavyosimulia tukio hili: "Muda huu hapa hoteli ya Movenpick jijini Dar es Salaam. Tunamshukuru sana Mungu kwani leo tumeweza kukutana tena bloggers kama unavyotuona...

Ya Santiago na nguvu za Kiraia

Mkutano uliokusanya wanablogu, wanahabari, wanaharakati na wanateknolojia watokao katika nchi mbalimbali umemalizika. Siku mbili za mwanzo zilihudhuriwa na watu wa kada mbalimbali kutoka hapa Chile na sehemu nyinginezo ikiwa ni pamoja na Kampuni za google, Yahoo, You tube na wengineo. Kilichokuwa muhimu sana katika siku hizo mbili za mwanzo, ni kutizama mifano ya namna uandishi wa kiraia (mablogu, twita, facebook, simu nk) ulivyoweza kushika kasi katika nchi mbalimbali zinazoendelea. Unaweza kusoma muhtasari hapa kuona namna blogu zinavyoleta mageuzi nchini Madagaska kupitia jumuiya ya wanablogu iitwayo Foko . Nilizungumza na Lova Rakotomalala juzi na nilishangazwa na jinsi jamaa wanavyoweza kufanya mambo makubwa katika mazingira magumu yanayofanana na yetu. Madagaska wamekuwa mfano mzuri wa nguvu ya uandishi wa kiraia. Siku zile mbili za mkutano zilitupa ushahidi wa wazi wazi wa namna uandishi wa kiraia unavyopamba moto katika nchi zinazoendelea. Bofya hapa uone mifano mic...

Mkutano wa wanablogu Santiago

Picha
Nimepata fursa ya kukuhudhuria mkutano wa wanablogu wa jumuiya ya Global Voices unaofanyika kwenye Ukumbi wa Maktaba ya Taifa, Santiago Chile. Moja ya vivutio vya mkutano huo ni kukutana na mwanablogu wa kitanzania aishiye Australia Bw. Joe Nambiza Tungaraza na Njeri Wangari mwanablogu wa mashairi wa Kenya .