Rafiki yangu wa ujanani...
Nasikitika mwezi huu umekuwa mzurimbaya. Kwanza nilivinjari miji kadhaa hapa nchini nikakutana na watu wa namna mbalimbali. Hiyo ilikuwa nzuri sana kwangu kwa mwezi huu. Hata hivyo, uzuri huo ukasababisha ubaya mwingine. Sikuweza kuwa mwandikaji mzuri. Hayo mawili. La tatu zuribaya, ni hili. Mara nyingine nimekuwa nikifuatilia mijadala mbalimbali kupitia simu ya kiganjani. Imenisaidia mara nyingi hasa nikiwa barabarani. Bahati nzuri juzi nikiwa kwenye usafiri wa daladala kuna 'tukio la mzunguko wa kiuchumi' lilitokea, simu yangu niliyoipenda sana, ikawa imependwa zaidi na mtumiaji mwingine nisiyemfahamu. Bila shaka inamsaidia huko alipo japo hakuniarifu wakati anaichukua, lakini inavyoonekana aliihitaji kuliko mimi. Akaondoka na majina ya watu wangu kwenye simu yangu ambao nsingependa kuwapoteza. Bahati nzuri wakati nakaribia kabisa kuipoteza simu hiyo, nilikuwa nimetoka tu kuwasiliana na rafiki yangu wa ujanani niliyepotezana naye kwa miaka kadhaa. Nilisoma naye madaras...