Tuache ubabaishaji, tubadilike
Nchi yetu inarudi nyuma kwa kasi. Zipo sababu nyingi. Moja wapo ninayoiona ni ubabishaji uliokithiri. Ile hali ya kushindwa kufanya mambo kama yanavyopaswa yawe, na kule kuchukulia mambo kirahisirahisi pasipo uwiano wa ukubwa wa suala na majibu yake. ( Asomaye na afahamu) Angalia siasa. Tizama wataalamu wetu. Madaktari. Wahandisi. Waalimu. Waandishi. Wote. Ubabaishaji. Ubabaishaji kila kona. Watu wanajitia kujua kila kitu. Inakuwa kama nchi hii haina wajinga. Ni kama nchi hii ina watu wanaojua kila aina ya kitu. Nchi ya wajuaji. Watu hatutaki kukubali ukweli wa kibinadamu kuwa ufahamu wetu una ukomo na hivyo hatuwezi kujua kila kitu. Ndio maana wetu hatukubali ukweli kuwa tu wajinga. Uliza kila mtu swali lolote, unapewa majibu. Ni kama kila mmoja ana majibu ya kila swali. Hakuna anayeomba "excuse" kwamba hapo bwana nimegota sijui. Ninanchotaka kusema mchana wa leo ni kwamba hatuwezi kuendelea endapo tabia ya kuamini kwamba tunajua kila kitu haitaondoka. Hatuwezi kuendel...