Self-Esteem: Ni muhimu kwa mwanao
Ninaanza na kukupa hitimisho: Mzazi anayo nafasi muhimu sana ya kumfanya mwanae ajenge fikra-chanya kuhusu maisha yake mwenyewe zitakazomfanya ajiamini. Na mzazi huyohuyo asipokuwa mwangalifu, anaweza kumsababishia mwanae fikra-hasi na hivyo kumfanya ajione duni. Kujenga fikra chanya kwa mwanao si kazi rahisi sana. Ni kazi ngumu inayodai muda wa kutosha wa mahusiano ya karibu kati ya mzazi na mwanae. Kazi hii haifanywi na wazazi wengi ambao huzaa pasipo kuhesabu gharama za uzazi husika. Hii ni kwa sababu kitendo kinachosababisha uzazi huwa hakihesabiki kama kazi. Kitendo hicho hufanyika katika mazingira ya starehe ya tamaa ya mwili kiasi kwamba wapenzi wengi huwa hawafikiri zaidi ya tamaa hiyo. Kwa maana nyingine, inaweza kukubalika nikisema kuzaa si kazi. Ndio maana hata wahenga walilonga: Kuzaa si kazi, kazi ni kulea. Kila mmoja wetu anaweza kuzaa akipenda. Ndio maana unawafahamu wasichana wadogo walioshika mimba bila kupenda. Hii ina maana kwamba kila binadamu asiye na hitilafu ya ...