Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2007

Kwa nini uko hivyo ulivyo?

Bila shaka umewahi kuonana na watu wenye aibu. Huenda na wewe unalo tatizo hilo la aibu. Au unamfahamu binadamu mwenye tatizo la mkono wa birika. Ama watu wenye mtazamo hasi tu katika kila kitu. Wenye kuwaza ubaya tu kwa watu wengine. Au pia inawezekana umewahi kuwaona watu wenye kupenda ngono utafikiri chakula na chai ya asubuhi. Na vijitabia vingi vingi hivi ambavyo hutokea hatuvipendi ila tunavyo. Ningependa tujadili chanzo cha tabia hizi na namna ya kuachana nazo. Ninajaribu kurahisisha maelezo ya kisaikolojia katika lugha nyepesi ili kuona namna ya kushughulikia matatizo-nafsi kwa namna rahisi zaidi. Ukweli ni kwamba kila mtu ni mwana-saikolojia. Hata kama wapo wanadhani kujua saikolojia ni mpaka ukasugue dawati darasani kwa miaka kadhaa lakini bado ukweli uko pale pale kwamba wewe ni mwana-saikolojia. Labda utadhani natania. Hebu fikiria, ni mara ngapi umeweza kubaini kuwa mtu fulani hana furaha ama ana huzuni ama amekasirika na kadhalika? Umejuaje? Unapoweza kujifunza kinachoen...