Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba, 2005

Bongo flava imevamiwa na wababaishaji

Siku hizi raia wanapambana na ufukara wao kwa mbinu nyingi.Zipo zilizo halali na hali kadhalika zipo zilizo haramu. Ndio maana utaona kuwa tatizo la ujambazi limekuwa likinona na kunenepa kila uchao. Watu wanatumia nguvu kunyanganya mali za wengine, mchana kweupe. Watu wanavunja nyumba za watu, wanachukua (iba) kila kilichomo mumo. Usije ukadhani kuwa wanapenda, ni mfumo unawalazimisha kutenda matendo hayo bila hiari. Ashakumu si matusi, afadhani ujambazi huu kuliko "ule mwingine" unaofanywa na wachache wanaodhani wana meno kuliko sisi kwa kutumia ile iitwayo demokrasia. Katika kukabiliana na ukata wa maisha, siku hizi kumeibuka kundi la vijana wengi wakilazimika kujiunga na miradi ya shughuli za usanii wa aina kadha wa kadha. Muziki mpya, maarufu kama Bongo flava, ukiwa ni moja wapo. Ni mradi usiodai gharama kubwa kama vile elimu ambayo siku hizi haipatikani kiurahisi. Kimsingi, hii ni njia halali ambayo faida zake si haba. Kwanza, ingawa haijawa ajira iliyorasmishwa, imekuw...

Sauti ya Umma inapomtaka Baraba...

Najua wengi hawasadiki mafundisho ya kitabu kiitwacho biblia. Mniwie radhi, nikirejee kidogo. Katika kitabu cha Mathayo 27:15-26 kuna tukio ambalo linasadifu suala la demokrasia ya enzi hizi. Hapa kuna fundisho la jinsi ambavyo demokrasia ya watu inaweza kuchezewa kama wapendavyo waungwana wachache wenye nafasi ya kufanya hivyo. Katika Uyahudi hiyo, wakati wa Pasaka, Pontio Pilato, Mkuu wa Dola ya Rumi katika Uyahudi , alikuwa na utaratibu wa kumfungua mfungwa mmoja wakati wa Pasaka (Mat. 27:15). Lakini Pilato ili kufanya hivyo inasemekana ilimpasa kupata ridha ya wananchi wa Uyahudi ile, ili amweke huru mmoja wa wafungwa kwa mujibu wa katiba yao. Basi, ilitokea katika Pasaka mmoja Yesu Mnazareti akawa amekamatwa kwa kosa la kuwakosoa watawala kwa kutangaza mambo ambayo hayakupendeza machoni pao. Nafikiri Yesu alikuwa tishio kwa watawala hao. Kukamatwa kwa Yesu kulikuja baada ya Yuda Iskariote kugawiwa takrima ya nguvu (Ni kama fulana siku za leo) iliyomshawishi kusahau mafundisho yote...

Ni kweli, tusiwategemee wanasiasa!

Jamani ninasikitika siwezi kublog mara kwa mara maana kidogo shule inanibana. Hata hivyo, huwa najitahidi kujua kuna nini kinaendela katika mtandao. Kwa kifupi, ninafuatilia sana soga za wanablogu (saaaanaa!)hata kama sitoi mawazo moja kwa moja kulingana na muda na masuala fulani ya shilingi. Namshukuru Mungu, ninakaribia kuwa huru, nitaonekana kila inapobidi. Mimi ni mpenzi wa safu ya Gumzo la wiki katika Mwananchi Jumapili. Pamoja na ukata mkali unaotukabili sisi tulio "wa kusoma", sikumbuki ni Juma lipi lilipita bila kulipitia kujua lina gumzo gani. Ni gazeti la kusoma ingawa ndio hivyo vijana wengi hatuonekani kupendelea magazeti siriaz, kama alivyobaini Padri Karugendo katika Rai toleo fulani. Juma lililopita kulikuwa na hoja nzito kwamba tusilogwe kuwategemea wanasiasa kutuletea maendeleo binafsi. Mwandishi alifanikiwa kunishawishi kwa hoja kwamba kuendelea kunahitaji mikakati na juhudi binafsi zaidi, kuliko kulia lia tukiwategemea wanasiasa wasiotabirika! Somo h...