Vijana wengi hawana elimu ya uraia?
Ninablog nikiwa Singida. Nimekuta harakati nyingi zinazohusiana na uchaguzi mkuu, utakaofanyika Desemba 14. Yupo Mhindi mmoja hapa anasumbua akili za watu kwa wingi wa hela alizonazo. Ukweli ni kwamba wananchi wa Singida wamekubali awe Mbunge wao si kwa sababu ya sera zake. Ni kwa sababu ya pesa! Hii ni ajbau maana ukimsiliza Mgombea huyu utashangaa kapita pitaje hadi kuteuliwa kuwa mpeperushaji wa bendera ya chama Kikongwe kama CCM? hajui kujieleza na akisimama anachokijua ni kutaja ahadi za miradi ya mamilioni atayoifanya akiwa Mbunge. Ni wazi, nimegundua, Vijana wengi wa MJi huu na mkoa kwa ujumla hawana elimu ya Uraia. Wengi wanafuata mkumbo na hawajuai umuhimu wao kushirikji katiuika masuala ya siasa. Utakuta wamejaa kijiweni wakilaumu kwa nini huyu bwana (Mhindi) kapitishwa na chama chake awe mgombea...wanalalamika sana. Ajabu ni kwamba ukiwauliza kama wamejiandikisha kupiga kura, watakwambia "hilo halihusiani na wala si muhimu...kura moja itaathiri nini?" Naam.Hiy...