Utaratibu wa Kufuata Unapoachishwa Kazi
Sheria
ya ajira na mahusiano kazini Namba 6 ya mwaka 2004 inaainisha mazingira kadhaa
yanayoweza kusababisha mwajiriwa aachishwe kazi na mwajiri. Kwanza, kama
mwajiri amefuata masharti ya mkataba yanayohusiana na utaratibu wa kumwachisha
kazi. Kufuata masharti ya mkataba kunategemea kama aina ya mkataba. Pale ambapo
mkataba ni wa kudumu, mwajiri lazima awe na sababu halali za kuchukua hatua za
kusitisha mkataba kwa kufuata utaratibu.
Lakini
pia mwajiri anaweza kumwachisha kazi mfanyakazi kwa sababu ya mwenendo mbaya na
utovu wa nidhamu kazini. Makosa yanayoangukia kwenye utovu wa nidhamu ni pamoja
na kufanya vitendo vya dharau ya kubwa kwa viongozi wako kazini na utoro. Utoro
ni kutokuonekana kazini bila taarifa au kuchelewa kufika kazini kinyume na
mkataba wa kazi.
Aidha,
vitendo vinavyoonesha ukosefu wa maadili vinaweza kuchangia kukuondoa kazini.
Kwa mfano, kufanya udanganyifu mkubwa, kuharibu mali za mwajiri wako kwa
makusudi, kuhatarisha usalama wa watu wengine kwa makusudi, uzembe mkubwa
kazini na hata kumtukana, kumdhalilisha au
kumshambulia mfanyakazi mwenzako, mteja, msambazaji au mwanafamilia au mtu yeyote
anayehusiana na mwajiri.
Vyovyote
iwavyo, kuachishwa kazi si jambo jepesi. Mbali na athari za kiuchumi, kupoteza
kazi bila hiari yako kunaweza kukuathiri kisaikolojia. Athari hizo zinaweza
kuwa kubwa zaidi kama utakuwa na hisia kuwa utaratibu uliotumika kukuondoa
kazini haukuwa wa haki. Hisia kuwa hukutendewa haki na ukakosa namna ya kupata
haki yako zinaweza kukuumiza zaidi.
Ndio
kusema, ni busara kujiridhisha kuwa pamoja na yaliyotokea bado unapata haki
zako unazostahili. Makala haya yanaangazia mambo mawili ya kufanya unapopewa taarifa
rasmi za kusitishwa kwa ajira yako.
Kufuatwa kwa utaratibu
Pamoja
na utaratibu wa uachishwaji kazi ulioainishwa kisheria, inawezekana mwajiri kwa
kujiona anaweza kufanya lolote, akaamua kukuachisha kwa sababu zake binafsi. Mfano,
pengine mwajiri amesikia umeathirika na VVU/UKIMWI na kuamua kukufuta kazi kwa
visingizio vingine. Lakini pia inaweza kutokea pamoja na kuachishwa kazi kwa
makosa ambayo wewe mwenyewe unajua ni ya kweli, taratibu za kufanya hivyo
hazikufuatwa.
Kwa
hivyo, hatua ya kwanza baada ya kupewa taarifa rasmi kuwa umeachishwa kazi, ni
kujiridhisha kuwa ni kweli utaratibu halali wa kisheria umefuatwa katika
kukuachisha kazi. Hapa kuna mambo mawili. Kwanza, mwajiri analazimika
kuthibitisha kuwa kuna kosa limefanyika na lina uzito wa kutosha kuhalalisha
kuachisha kazi.
Jambo
la msingi ni kwamba hata kama umefanya kosa, mwajiri analazimika, kwa mujibu wa
sheria, kufanya juhudi za kurekebisha nidhamu yako kwa unasihi (ushauri) na
maonyo. Kuonywa kunalenga kukusaidia kuelewa kuwa unapofanya kosa kama hilo
unaweza kuchukuliwa hatua zaidi za kinidhamu. Ikumbukwe kuwa mwajiri analazimka
kuwafahamisha wafanyakazi sera za nidhamu katika eneo lake la kazi.
Kwa
mujibu wa Sheria hii, mfanyakazi anapofanya kosa na mwajiri akaona kuna haja ya
shauri kufanyika, basi mwajiri analazimika kumpatia hati ya mashtaka mfanyakazi
husika iliyoandikwa katika lugha ambayo mfanyakazi ataielewa. Kisha mfanyakazi
atapewa muda wa kutosha (si chini ya masaa 24) kuandaa utetezi. Katika
kutekeleza haki hii ya kusikilizwa, mfanyakazi anaweza kujitetea kwa msaada wa
vyama vya wafanyakazi au mfanyakazi mwenzake.
Shauri
hili litaendeshwa na wakili ambaye atakuwa hakushiriki kwenye mazingira
yaliyosababisha kesi. Mfanyakazi atakuwa na haki ya kujibu tuhuma na kuhoji
mashahidi watakaoitwa na mwajiri. Hata hivyo, mfanyakazi asipokuwepo bila
sababu, shauri lake litaendelea bila yeye kuwepo. Uamuzi ukishafanyika, ikiwa
ni pamoja na kuachishwa kazi, mfanyakazi atajulishwa kwa maandishi na kuelezwa
sababu za kuachishwa kazi.
Katika
mazingira ya kuachishwa kutokana na utendaji mbovu, utaratibu kama huo
utachuliwa isipokuwa hapa mwajiri atahitajika kumwezesha mfanyakazi kujifunza
kazi kabla ya kuchukua hatua zozote. Kadhalika, pale ambapo mfanyakazi
ameachishwa kazi kutoka na ugonjwa au ameonekana hawezi tena kudumu kazi zake
shauri ya ugonjwa, mwajiri atahitaji kuongozwa na maoni ya daktari.
Haki unazostahili
Mfanyakazi
aliyeachishwa kazi ana haki ya kulipwa kiinua mgongo cha mshahara wa siku 7 kwa
kila mwaka kamili wa kuwa katika ajira mfululizo kwa mwajiri huyo kwa miaka
isiyozidi 10. Mshahara wa siku unaweza kukokotolewa kwa kugawanya mshahara wa
mwezi kwa kila siku.
Hata
hivyo ikiwa mfanyakazi aliachishwa kabla ya kuisha mwaka wa kwanza wa ajira,
aliachishwa kihalali kwa sababu ya mwenendo mbaya, kukosa uwezo, kutokuhitajika
au amekataa kazi mbadala aliyopangiwa basi hatastahili malipo ya kiinua mgongo.
Pia,
akiba ya mfanyakazi kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii haitaguswa na mwajiri kwa
sababu zozote. Katika mazingira ambayo mfanyakazi ameachishwa kazi akiwa na
mkopo benki, itategemea na makubaliano yaliyofikiwa kati yake na benki. Kwa
mfano, ikiwa mwajiri ndiye mdhamini wa mfanyakazi benki, kwa maana ya
mfanyakazi kutumia mshahara wake kama dhamana, ni jukumu la mwajiri kuwasiliana
na benki kuhusiana na deni litakaloachwa.
Haki
nyingine unazostahili ni cheti cha utendaji kazi chini ya mwajiriwa anayekufuta
kazi, posho ya usafiri kwenda mahali ulikotoka kwa mujibu wa mkataba na
mwajiri.
Usuluhishi
Katika
mazingira ambayo unaamini hujatendewa haki kwa maana kutokuridhishwa na
utaratibu uliotumika kukufuta kazi, una nafasi ya kupata msaada kwenye tume ya
usuluhishi wa migogoro ya kazi. Maamuzi ya tume hiyo yataongozwa na kanuni za
taasisi za kazi za mwaka 2007 zinazolenga kulinda maslahi ya pande zote.
Hata
hivyo, wakati ukishughulikia mgogoro huo kisheria, hupaswi kulazimisha
kuendelea na kazi hata kama unaamini ulionewa.

Ikiwa nimefanya kazi ndani ya miezi mitatu, na nimesaini mkataba wa mwaka, ila kwenye mkataba kuna kipengele cha majaribio ya miezi mitatu. Je, mwajiri akinisimamisha kazi, haki zangu zikoje kwenye malipo?
JibuFutaNaomba jibu please. Asante.
Yusuph
FutaIkiwa nimefanya kazi miaka mitatu na sina mkataba wowote,,je ni haki kisheria?
JibuFutaMartin
FutaJe ni harali kufanyishwa kazi au kuajiliwa Na kampini zaidi ya miaka miwili bila mkataba?
JibuFutaShaban
FutaSauda
FutaJe nikiwa nimefanyisha kazi na raiya wakigeni zaidi ya miaka mili sina mkataba nna kiinuwa mgongo apo kaniachisha kazi kwakunishuku kwamba nimemuibia police ikasibitsha sikafanya wizi huo
JibuFutaNapenda kuuliza kwamba he unapokua umepunguzwa kazi ukapewa notice ya yakupungwa Nazi na malipo ya kinua mgongo yatakiwa kutolewa ndani ya Siku ngapi
JibuFutaJe unapofanyishwa kazi na kampuni baada ya miaka miwili haijakupatia mkataba.na ikakupatia mkataba baada ya hapo ikakufukuza kazi.swali langu ni kuhusu mafao unatakiwa kupata kuanzia pale mkataba wako unapoanzia au ni kuanzia pale ulipoanzia kazi pamoja na kwamba walichelewa kukupatia mkataba wao? Naomba majibu 0766367032.
JibuFutaKwa karibu mwaka mmoja, mume wangu aliniacha mimi na watoto wetu wawili. Aliacha kujali, akaacha kupiga simu, na akaondoka kabisa. Nilikuwa nimevunjika moyo, nimechanganyikiwa, na karibu kupoteza tumaini. Kisha siku moja, rafiki yangu aliniambia kuhusu Dkt. Dawn, mtu wa kiroho aliyepewa kipawa na ulimwengu ili kuwasaidia watu kurejesha upendo na amani.
JibuFutaMwanzoni, nilikuwa na shaka, lakini kitu kuhusu maneno yake kilinipa amani. Aliniambia haswa kilichokuwa kibaya na kwamba mtu alikuwa ametupa uchawi mkali kututenganisha. Aliandaa kazi maalum ya kiroho na uchawi wa kuungana tena kwa ajili yangu - na ndani ya siku chache, mume wangu alinipigia simu ghafla, akilia na kuomba msamaha.
Tangu wakati huo, maisha yangu hayajawahi kuwa sawa. Ndoa yetu sasa ni tamu na yenye furaha zaidi duniani. Tunapendana zaidi kuliko hapo awali, na nyumba yetu imejaa vicheko na baraka.
Lakini sio hivyo tu - Dkt. Dawn pia alisaidia kuondoa bahati mbaya na nishati hasi iliyozunguka familia yetu. Tangu wakati huo, kila kitu kimekuwa laini: amani nyumbani kwetu, maendeleo ya kifedha, afya njema, na furaha safi.
Ninashukuru ulimwengu kila siku kwa kuniongoza kwa Dkt. Dawn. Kwa kweli ni mtu mwenye nguvu na mwanga wa kimungu. Ikiwa unapitia hali yoyote - huzuni, bahati mbaya, au kuchanganyikiwa - usikate tamaa. Mfikie na uache ulimwengu ufanye kazi kupitia yeye ili kubadilisha hadithi yako, kama vile alivyobadilisha yangu.
Wasiliana naye kwenye WhatsApp: +2349046229159
dawnacuna314@gmail.com
Uchawi wa mapenzi wa Dkt. Dawn hufanya maajabu kweli.
JibuFutaNiliwasiliana na Dkt. Dawn wakati uhusiano wangu ulipovunjika kabisa. Mpenzi wangu wa zamani alikuwa ameniacha na kunizuia kwenye mitandao yote ya kijamii. Nilivunjika moyo na kupoteza tumaini. Baada ya kushauriana na Dkt. Dawn, kila kitu kilibadilika. Mpenzi wangu wa zamani alirudi peke yake, akaomba msamaha kwa dhati, na akaomba msamaha. Leo, tunaishi pamoja kwa furaha, na hata tuna mtoto.
Maneno hayatoshi kuelezea jinsi ninavyoshukuru. Kutokana na uzoefu wangu, naweza kusema kwa ujasiri kwamba Dkt. Dawn ni halisi, anayetegemewa, na mwenye nguvu. Ikiwa unakabiliwa na hali yoyote ngumu maishani mwako hivi sasa, Dkt. Dawn anaweza kukusaidia.
ANAWEZA KUKUSAIDIA KWA MATATIZO YAFUATAYO:
Kurudisha ndoa na mahusiano yaliyovunjika
Kuvutia mafanikio na ukuaji katika biashara
Matatizo ya uanaume, utasa, na ukosefu wa watoto
Kurejesha mali zilizoibiwa au zilizopotea
Kurudisha kazi zilizopotea au fursa za kazi
Kinga dhidi ya uchawi na macho mabaya
Hirizi za mvuto
Kutatua migogoro ya ardhi na mali
Kuwafanya wapenzi kutimiza ahadi zao
Kushinda kesi mahakamani, na mengine mengi
Huu si ulaghai — ni ushuhuda kutoka kwa uzoefu.
Kwa maelezo zaidi, wasiliana naye moja kwa moja kwenye WhatsApp. +2349046229159
dawnacuna314@gmail.com