Unaweza kuwa mzazi bora zaidi kwa kujifunza kwa wazazi wako

NI UKWELI kwamba katika suala la malezi, hakuna kitu unachoweza kukiita 'the obvious'. Hakuna uzoefu. Na tunahitaji kujifunza kwa wengine. Ndivyo anavyofanya mzazi mmoja nchini Panama, Joel Silva Díaz, anayeandika uzoefu wake wa kimalezi katika blogu yake. Lengo lake ni kushirikisha wasomaje wake kile anachodhani kinaweza kuwasaida watu wenye kiu ya kujifunza.

Anasema, 
Sikumbuki kuwa na mazungumzo ya zaidi ya mistari mitano na baba yangu. Ni miaka kumi na zaidi imepita. Kwa matukio ya hapa na pale kati yangu na baba yangu, naweza kusema tu ni kwamba angalau nilikuwa na baba.
[...]
Na hicho ndicho ninachotaka kukifanya vizuri zaidi, nataka kuwa baba anayefanya bila hata kutambua, nataka kuwakumbatia, kuwabusu, kuwapa fursa bora za kufanya maamuzi bora na kuwasaidia wanapokuwa hawajafanya chema, sichelewi kuwonyesha upendo na kuwajali, hata kama kuna nyakati naweza kweli kuwafinya.
[...]
Kama mzazi, nisingependa  niwe mtu wa kuwachungulia wanangu kila baada ya majuma mawili. Nataka kuwepo...ninataka watoto wangu wawe na angalau kumbukumbu moja nzuri akilini mwao, kwamba baba yao aliwapenda.

Joel Silva Diaz anatuonyesha namna tunavyoweza kujifunza kuwa wazazi kwa kutazama namna wazazi wetu walivyotulea. Kile tunachovutiwa na malezi yao, kituhamasishe kukifanya kwa watoto wetu. Kile ambacho tunadhani tulikikosa kwa wazazi wetu, tukifanye kwa wanetu. Vingi ambavyo wazazi wetu wanaweza kuwa hawakuvifanya kwetu, si kwa sababu hawakupenda bali tu kwa sababu hawakujua the better way. Hakuna mzazi asiyependa kufanya chema for the best interest of the child. Hakuna.

Unaweza kusoma zaidi hapa, na kumfuatilia Diaz kwenye mtandao wa Twita.

Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Haiba ni nini?

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Uislamu ulianza lini?