Heri ya mwezi mpya!
Mwezi wa tano ndio huu. Tarehe mbili leo. Kama ulikuwa hujapanga cha kufanya mwezi huu, ndugu, hujachelewa. ( Si unajua haipendezi kufanya chochote bila kupanga?) Tabia ya kusubiri mwisho wa mwaka ndio tuanze kufikiri kupanga mipango mingi ya mwaka mzima ( ambayo hata hivyo haitekelezeki) si nzuri sana. Nakukumbusha mipango yako ya mwaka huu: Ulipanga kufanya nini mwaka huu? Je, umefikia walau nusu ya mipango yako? Una mikakati gani na mwezi huu wa tano? Nusu ya mwaka ndo inayoyoma! Nakukumbusha kutafakari upya mambo yako mwaka huu, uone wapi umefanikiwa na wapi unahitaji kujipanga vyema zaidi. Nakukumbusha kutafakari changamoto ulizokumbana nazo katika sehemu ya kwanza ya mwaka huu, na ufikiri namna ya kukabiliana nazo vizuri zaidi kwa nusu iliyobaki. Na unapofanya hivyo, usiache kupitia hapa kuanzia juma hili kwa ajili ya vipande vya saikolojia na falsafa za kutafakari pamoja namna ya kujielewa. Niwatakieni wanablogu wote heri ya mwezi mpya wenye mafanikio (pamoja na uki