Rais mteule atumia mitandao ya kijamii kuwaomba raia kumchagulia Baraza la Mawaziri
KATIKA kuthibitisha kwamba kasi ya matumizi ya mitandao ya kijamii ni kubwa, hivi majuzi, Rais mpya wa Indonesia Mhe Joko Widodo (maarufu kama Jokowi) amewaomba watumiaji wa mtandao wa Facebook kumsaidia kuteua baraza lake la mawaziri kwa kupendekeza majina ya watu wanaoweza kushika wadhifa wa kuwa Mawaziri. Hatua hiyo, ni mwendelezo wa kile anachokiita mwenyewe 'kuongeza kwa ari ya kujitolea' miongoni mwa raia wa nchi hiyo, baada ya watu wengi kujitolea kumsaidia katika harakati zake za kuingia ikulu. Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Jokowo ametoa orodha ya nafasi 34 za Uwaziri , zenye majina matatu yanayopendekezwa kwa kila nafasi, huku kukiwa na nafasi ya nne wazi kwa wananchi kupendekeza wanayemtaka. Widodo anataapishwa ifikapo Oktoba 20, 2014 kuwa Rais. Joko Widodo (53) Gavana wa zamani wa Jakarta, amechaguliwa kuwa Rais wa Indonesia baada ya kumbwaga mpinzani wake Prabowo Subianto kwa asilimia 53 ya kura milioni 130 zilizopigwa tarahe 9 Julai, 2014. Kama ilivyo