Hakuna kujifunza bila kutofautiana kimawazo

Ni Jumapili nyingine njema. Hatuna budi kukumbushana kwamba siku ndo zinaenda hivyo. Siku ya tisa leo. Zinaenda. Bado siku chache tuelekee kwenye mwezi wa lala salama. Mwezi wenye sherehe nyingi kuliko utekelezaji wa mipango ya wanajamii. Siku zinakatika.

Kwangu Jumapili ni siku ya kupumzika kwa asilimia mia moja. Sababu ni kwamba katika siku sita za juma huwa ninabanwa kisawasawa na dunia. Kwa hiyo Jumapili kwangu ni siku ya kujisomea ninavyovitaka. Kulala. Stori. Kula. Alimuradi tu kufurahia mwisho wa juma.

Nimekuwa nikitafakari michango kadhaa ya wachangiaji wa blogu hii hasa kwenye makala za uwapo wa Mungu. Najua kila mtu anao mtazamo wake. Japo najua watu wengi hawajajaliwa kuweka wazi mawazo yao hasa inapokuja suala lenye utata kama hili. Nawashukuru waliomajasiri kujaribu kuchokoza mawazo ya wengine. Kuchokoza mawazo si kazi rahisi.

Nilikuwa napitia pitia niliyopata kuyaandika. Basi nikapata makala hii niliyoiandika miaka miwili iliyopita. Ilihusu biblia na imani zetu. Hiyo ilikuwa baada ya Da Vinci kuandika kile kitabu chake. Bofya hapa kuipitia uone tofauti za mawazo zinavyonogaga. Hakuna kujifunza kama wote mnasema kitu kinachofanana.

Basi. Nategemea kuandika mtazamo wangu kuhusu Mungu. Ni mtazamo. Niweke wazi kwamba ningependa kuthibitisha kisayansi kwamba Mungu yupo. Ujasiri huo ninao. Kwa sababu baada ya miaka kadhaa ya kusoma nadharia kadha wa kadha katika sayansi ya maumbile, nyingine zikijaribu kumkana Mungu wakati pasipokujijua kumbe zinamthibitisha Mungu huyuhuyo, naweza sasa kujituhumu kuwa na haki ya kutumia nadharia hizo za kisayansi kuthibitisha uwapo wa Mungu.

Najua kuna dini. Na mimi siamini katika dini. Hivyo sitatumia maelezo ya dini kujaribu kumthibitisha Mungu. Lakini cha maana kwa sasa ni kukuhabarisha tu kwamba Mungu lazima awepo kwa mujibu wa sayansi. Nitafafanua nipatapo wasaa. Usiende mbali.

Maoni

  1. angalia www.vilagrablas.blogspot.com
    kisha research and deduce..

    JibuFuta
  2. Imani yangu inanituma kuwa Mungu yupo ingawa sijamwona. Na kuhusu dini hii ni kila mtu anaamua kuanzisha dini na watu wengine wanaamini dini hiyo. Ni ubunifu tu wa watu. Mawazo yangu. acha wengine waseme.

    JibuFuta
  3. Ninaingoja kwa hamu makala yako ya kuthibitisha uwepo wa Mungu maana italeta changamoto kubwa sana kwa wasomaji.

    JibuFuta
  4. Kwa haraka haraka nimepitia blog yako nikaona, kunamengi ya kujifunza humu.
    Nitakapopata muda nitatulia na kuisoma kwa makini na ninaamini we have something in common.
    Naomba na wewe ukipata muda usisite kupitia ka blog kangu ka utambuzi ili tusaidiane mawazo katika kukaboresha.
    nitembelee kwenye:

    www.kaluse.blogspot.com

    JibuFuta
  5. Nuru hujajibu swali langu kwenye moja ya post hapo chini. Nasubiri jibu.

    Kasule napitia sasa hivi. Karibu sana kaka.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Uislamu ulianza lini?

Zijue Tabia Nne za Kiongozi Bora Kazini

Tabia za Mtoto wa Miaka 0 – 3 Kimahusiano na Kihisia