Long live JUMUWATA
Leo ni siku ya kuadhimisha maendeleo ya blogu Tanzania. Maadhimisho haya yalianza rasmi mwaka juzi, kwa makubaliano ya wanablogu wenyewe walipokutana kwa mkutano mkuu wa kwanza wa mtandaoni. Soma blogu hii hapa kwa maelezo zaidi.
Kusema kweli tuna kila sababu ya kufurahia kuanzishwa kwa jumuiya hii muhimu ya kutuunganisha. Siku hii haikupaswa kabisa kuwa hivi ilivyo leo. Kwamba kila mmoja anasherehekea kivyake vyake si jambo la kujivunia sana.
Kwa wanablogu wapya, ni vyema kufahamu kuwa tunayo jumuiya yetu yenye viongozi waliochaguliwa kwa kura. Angalia majina yao hapa.
Napenda kumpongeza sana Kitururu kwa kazi kubwa aliyoifanya akishirikiana na wenzake. Najua anayo majukumu mengi ya kufanya. Lakini bado hajasita kujitolea kwa faida ya wote. Yupo Da Mija mwamke wa shoka ambaye juhudi zake za kujitolea zimeipeleka mbele jumuiya yetu. Ndesanjo mzee wa kujikomboa. Majukumu nayo bila shaka yamembana. Historia inamkumbuka. Mwenyekiti wetu blogu yake haipatikani. Sijui kilichotokea.
Jambo moja ambalo ningependa tukumbushane miaka hii miwili baadae: Je, tufanyeje kuongeza mshikamano zaidi katika Jumuiya yetu?
Kila la heri unapokumbuka siku maendeleo ya blogu yalipowakutanisha watanzania kutoka pande mbalimbali za dunia kwa mara ya kwanza. Tarehe 18 Mwezi wa 11 miaka miwili iliyopita. Hakuna kulala.

Ni kweli kila la heri, bila hivi hatungefahamiana. Nimewafahamu watu wengi sana kwa kuanzisha blog yangu.
JibuFutaKaka Simon kazi nzuri sikujua kama ulikuwa na cheo.
Well, Well, Well! Tunajumuika na wakongwe kuadhimisha. Lakini pia kukumbusha yale mengi mema yanayoweza kufanywa na blog hizi kuikomboa jamii. Tukiacha kuzifanya kama sehemu za kulalamikia matatizo yetu na badala yake kuzifanya kama sehemu ya kuweka na kubuni suluhisho, basi tutakuwa tumefanya meeengi ya kuisaidia jamii na hapo tutatimiza lile walifanyalo wenzetu waliotanguliwa; kuzifanya BLOGS kuwa sehemu kuu ya jamii.
JibuFutaLive Long JUMUWATA
Najua JUMUWATA iko kimya kinamna na najua ina nafasi ya kufanya mengi . Na mpaka sasa naweza kukiri kuwa hakuna mchango wa jumuwata unaoonekana na labda ni mimi muhusika. Nitajitahidi kufanya kitu hata hicho kitu kikiwa ni ni kuwezesha viongozi wengine kufanya kazi wenye nafasi. Samahani nilio waangusha maka sasa . NAJISIKIA AIBU KAMA KATIBU!:-(
JibuFuta@ Yasinta, Umesema kweli.
JibuFuta@ Changamoto, Nakubaliana na wewe kwa asilimia zote.
@Simon kazi yako kama Katibu inaonekana. Tunakutia moyo kuifanya kazi hii kwa ari mpya zaidi. Tunajua ni ya kujitolea na inahitaji moyo kama wako kuifanya.