Tofauti ya Magharibi na Kusini

Natafakari tofauti hasa iliyopo kati ya mataifa ya magharibi na kusini. Wakati Zimbabwe kura zinapigwa na mwezi unakatika ndo matokeo yafahamike...wakati Kenya inachukua majuma kadhaa...wakati Bongo unaelewa mwenyewe...Marikani imechukua masaa kadhaa matokeo yamejulikana. Na si tu masaa hayo, lakini mshindwa anatoa kauli ya moja kwa moja kwamba aliyeshinda kashinda. Anampongeza.

Mimi sielewi. Hivi tofauti hii inatokana na nini? Umasikini? Uroho? Ujambazi? Ama ni ujinga flani mukichwa? Sielewi. Hivi sisi ndugu zangu tumepungukiwa nini hasa? Mwenyezi Mungu alitunyima nini sisi wanadamu wa dunia ya sita?

Kuna haja ya kujielewa. Ipo haja hiyo.

Maoni

  1. Hii yote ni kutokana na uongozi mbaya na kudanganya wananchi na kupata pesa bure RUSWA. Tuchukue Zimbabwe kwa nini wapige kura mara mbili na ubishi mwingi. Haya ni maoni na mtazamo wangu

    JibuFuta
  2. Mimi naamini ndivyo tulivyo (miafrika)hata mpinzani ukimpa nchi akiingia ikulu tu kutoka kazi hadi muuane.

    Kazi kwelikweli

    JibuFuta
  3. ni ujinga, upuuzi na uroho miongoni mwa wapuuzi wachache wanaodhani kuwa wao ndio wa kuongoza tu na lazima wakae madarakani. wanadhani bila wao nchi haiwezi kuongozwa wakati siku inakuja ambapo wao watakufa na nchi zitaendelea kuwepo/

    JibuFuta
  4. Sasa huu upuuzi unatokea wapi? Mpaka muuane ndo mbadilishane madaraka? Wapi liliko tatizo?

    JibuFuta
  5. mifumo yetu na hasa ya elimu kwamba hatusomi kwa malengo na wala hatuna malengo, tunafanya vitu kiubishi na kiubabe ubabe tu.
    waulize viongozi wetu wanamalengo gani na wanayatekeleza vp, utaduwaa. rejea sera za CCm kwenye kampeni za 2005, na kinachofanyika leo, utaona ujuha fulani usioingia akilini, hapo liko tatizo kwa wapigana wapigiwa kura

    JibuFuta
  6. Kamala asante kwa michamngo yako na samahani kama maswali yanakuwa mengi. Lakini najaribu kujiuliza kwa nini basi mfumo wetu uwe duni? Kwamba hatusomi kwa malengo. Sawa. Lakini kwa nini inakuwa hivyo? Kwamba wapiga kura wana tatizo, hilo halina ubishi. Sasa kwa nini wawe hivyo walivyo?

    Umagharibini wamejaliwa nini tusichonacho sisi? Si tu binadamu sawa? Sasa kwa nini katika mambo ya msingi kama haya tofauti zinakuwa bayana? SIjui kama nimejieleza kikamilifu.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?