Jana nilikuwa nikitazama kipindi cha kiislamu kwenye televisheni ya Chaneli 10. Suala la mali katika ndoa za dini hiyo lilikuwa likijadiliwa. Kwamba Kiislam, mali katika ndoa si suala la wanandoa kwa pamoja. Kwamba mali anazoingia nazo mwanandoa kwenye ndoa, zinabaki kuwa zake mwenyewe. Na wakiachana, kila mmoja anaondoka na alichokuja nacho. Hata ndani ya ndoa, mali zinapatikana 'separately' kwa maana ya kwamba kila anachopata mwanandoa hicho ni haki yake yeye mwenyewe. Wakitengana, kila mtu anaondoka na vyake. Katika kufakari hayo, nilijaribu kumfikiria mwanamke na nafasi yake katika ndoa. Nikamwona kama kiumbe anayenyanyaswa na dini. Kwa nini? Wanaume wengi hutafuta mali kwanza ndio waoe, na hata wanapooa, huwaoa wanawake watakaowategemea wao. Katika hali hii nini salama ya mwanamke katika dini inayoruhusu talaka? Hizi si dalili za wazi za ukandamizaji wa jinsia ya kike?
Asante kwa kunikumbusha nitajaribu kuwa hewani
JibuFutaAhsante kwa taarifa hizi muhimu.
JibuFutaJe wadau wanakutana wapi? na je kutakuwa na matukio gani?
Tunakutania mtandaoni kubadilishana mawazo kaka
JibuFuta