Je, kuna Mungu? - Mchango wa Kamala

Haya. Nashukuru kwa michango ya wasomaji kuhusu hoja ya uwapo wa Mungu. Ufuatao ni mchango wa Kamala mwanablogu machachari anayepatikana hapa.

Yeye anasema: " Kwa vyovyote kuna nguvu inayoendesha haya mambo, kuna nguvu ambayo ni ya ajabu katika hufanyaji kazi wake.

nguvu hii wakristo huuita Mungu na waislamu huiita Allah, kila mtu hujiona yuko sahihi lakini wanasayansi ndio basi kwani wao huiita Nguvu tu kama ilivyo. siku zote wanasayansi hukataa kuwepo kwa mtu anayeitwa Mungu lakini hukubali kuwepo kwa nguvu na wanasema kuwa nguvu haiwezi kubadirishwa wala kuharibiwa na wala kupindishwa!

uwepo wa nguvu unaonekana tu wenyewe, biblia inasema tumeumbwa kwa mfano wa Mungu kwa hiyo basi na sisi ni nguvu au Roho kama ilivyo hiyo Mungu.

sisi kama binadamu mawazo yetu, maneno (kauli) yetu, yananguvu kuliko tunavyofikiri na hubadirisha na kutupangia maisha yetu. kwamfano, Tanzania sio nchi masikini na wala watanzania sio masikini bali ni nguvu ya Hoja ya watu fulani na sisi kuipokea na kukubali ndivyovinatufanya kuonekana masikini - Nguvu hizo!

Dini nyingi huamini kwamba nguvu hiyo (Mungu) inahasira na inachukia baadhi ya watu wanaofanya kinyume na maneno ambayo kimsingi ni mapendekezo ya watu waliopita, hii sio kweli!

nguvu hii ipo na inapenda kila mtu na kila kitu na haihitaji chochote kutoka kwa yeyote isipokuwa ipo kupenda na kupenda tu.

iko sawa na umeme wa pale Mtera, ukifika mtera huwezi kuona umeme kwa macho na hukuna aliyewahi kuuona umeme japo tunautumia kila siku. wala mtera haijui hasi na chanya, mpaka short ikitokea na kudhuru, yenyewe haijui! inajua kuendelea kuwepo! muifuate mtera na kuileta kwa nguzo mijini msiifate, yote sawa ila nyie msioifuata mdo mmnaopoteza! (mtalala gizani etc)

nguvu hii ufikiwa kwa upendo kwani asili yake ni upendo usiowamasharti wala wa kulipiza! hufikiwa kwa sayansi ya Roho (science of the soul)

wanasayansi wetu wanasema hakuna mungu na hii ni kweli kwani Mungu hawezi kupatikana kwa majaribio ya kisayansi, bali kwa majaribio ya sayansi ya roho na hapa ninamaanisha "tahajudi/taamuli-meditation! ambayo hutumika kutuunganisha na Nguvu kuu kama zifanyavyo nguzo na nyaya kwa kuunganisha Nyumba zetu, miji yetu viwanda vyetu nk na chanzo cha umeme yaani mtera..."

Maoni

  1. Asante Kamala kwa kuonyesha uhusiano uliopo kati ya ulimwengu usioonekana na ulimwengu mwingine uonekanao kama namna ya kueleza dhana ya Mungu.
    Hata hivyo kuna mambo yanajitokeza. Kama vile, inakuwaje unafahamu kuwa nguvu hiyo ina upendo? Na sayansi ya roho unayoizungumzia ni ipi?

    Ulisema:
    " nguvu hii hufikiwa kwa upendo kwani asili yake ni upendo usiowamasharti wala wa kulipiza! hufikiwa kwa sayansi ya Roho..."

    JibuFuta
  2. nasema nguvu hiyo inaupendo kwa sababu; ni kwa kuwa na upendo tu ndipo tunaweza kuifikia, kuitumia na kufurahia katika maisha yetu hata kama hatujui kuwa kuna nguvu hiyo.

    nikisema upendo hii ni dhana pana pia. kumbuka kupenda ni kukubali au kupokea kama mambo yalivyo au yawavyo au uwezo wetu wa kupokea matokeo ya matendo/mawazo yetu au ya maumbile.

    kuna watu wazuri wa kulalamika na kulialia tu. mf. mvua ikinyesha analalamikia matope, baridi, utelezi n.k, jua likiwaka analalamikia Joto, kuumia macho n.k ni vigumu kwa watu hawa wasiopenda hali hizi mbili muhimu za hewa kuifurahia nguvu kwani hawana upendo wa matokeo ya kazi ya maumbile (nguvu).

    waafrika wanaouchukia uafrika wao, wanajichukia wenyewe na hivyo wataichukia Nguvu kuu au matokeo ya kazi ya nguvu hiyo! hawawezi kufurahia nguvu hii.

    waoga wanaokataa kufa na kuogopa kwamba watachomwa moto siku moja wakifa, bila kujua kuwa kufa ni kuuvua tu mwili! hawataifurahia nguvu hii pia.

    kimsingi nasema inajidhihirisha kwa upendo kwani ni kwa kupokea na kukubali kila hali (matokeo) kama inavyokuwa bila kinyongo na lawama ndipo tutaifurahia nguvu hii kwani kupokea na kukubali hali (matokeo) ni msingi mzuri wa kuchukua hatua mpya na nzuri kwani utakuwa na uhuru wa kuchagua kutokana na matokeo-- na utapenda!

    2. sayansi ya Roho ni ile hali ya kuulewa undani wako na kuufurahia. Dini nyingi husingizia kuelimisha juu ya sayansi hii lakini bado.
    kuilewa sayansi ya roho ni hatua nzuri ya kuelekea kuilisha roho na kuipatia chakula chake.

    wengi tunasahau kuwa tuna roho na tunaishi kwa kufuata matakwa ya miili na akili mwisho wa yote ni kuteseka kwani vitu vya nje yako haviwezi kamwe kukupa furaha na amani, isipokuwa vya ndani yako-Roho.

    Sayansi ya Roho ni pana na ngumu kueleweka, lakini wengi wanaangahika kuitafuta na kuishia kupotea/kupotezwa.

    kimsingi sayansi ya roho inatuwezesha kuishi vizuri kwa amani upendo na furaha na kutuonyesha kwamba sote kiroho ni kitu kimoja isipokuwa kimwili ni tofauti! ni roho ndio inayoweza kutufanya tuache upuuzi wa kudhani kuwa kuna waliobora kuliko wengine.

    tusiisahau roho jamani, tuipe kipaumbele na kuipa chakula chake!

    ukiishi Kiroho hautakula au kunywa vyakula hovyo bali utakula kwa sababu. Hautaongea na kutukana hovyo bali utaongea kwa sababu... kila kitu utafanya kwa sababu au lengo/malengo na hivyo utaishi maisha yenye malengo (the purpose driven life)

    JibuFuta
  3. Sina lakusema zaid yakusukuru kutokana na somo lako.

    Nimejifunza kwa somo.
    Nimefurah kwa swali alouliza ndugu yangu hapo.
    Na nimejifunza pia kwa majibu ulotoa.

    Asante sana

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Haiba ni nini?

Uislamu ulianza lini?