Je, kuna mungu?

Hakuna mjadala kwamba kila jamii inaamini katika Mungu. Hata kama tafsiri hasa ya mungu huyo hutofautiana kutoka jamii moja hadi nyingine, lakini ukweli unabaki kuwa kila jamii inaamini katika mungu.

Ningependa tujipe nafasi ya kujadili dhana ya Mungu katika jamii kwa mtazamo usio wa kigomvi wala kulazimishia majibu kwa kutumia imani tulizonazo. Najua dini zetu zilituzuia kujiuliza maswali ya msingi kama haya. Zinatulazimisha kuamini hata kama hatuelewi. Na tunapojaribu kufanya hivyo, tunaambiwa, tunakufuru.

Siamini kuwa kujadili jambo kwa nia ya kulielewa ni kukufuru. Tunaishi katika kizazi kinachotaka ushahidi zaidi kuliko imani. Kwa hiyo hapa ninayo maswali ya kuuliza:

1. Je, Mungu yupo?

2. Na kama yupo, nini kinatufanya tuamini hivyo?

3. Je, ni kweli kwamba sayansi inamkana mungu?

Nadhani kujielewa ni pamoja na kupata majibu ya maswali haya kwa ufasaha.

Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo ya Kuzingatia Unapoandika Wasifu wa Kazi (Curriculum Vitae)

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Haiba ni nini?

Tabia za Mtoto wa Miaka 0 – 3 Kimahusiano na Kihisia