Ukitaka Kujifunza Waruhusu Watu Waone Usichokiona
UKIFUATILIA mazungumzo ya wa-Tanzania
wengi kwenye mitandao ya kijamii, unaweza kuona namna watu wanavyojinasibu
kujua. Mijadala mingi imejaa ‘ujuaji’ unaofanya watu wajigambe, wadhihaki wengine,
watukane na wakati mwingine, kadri ya mamlaka yao, watake kulazimisha kile
wanachokiona wao ndio kiwe ukweli usiopingika.
Katika makala haya, ninajaribu
kuonesha kuwa ili tujenge jamii ya watu wastaabu wanaoheshimiana lazima tuwe
tayari kujifunza hata katika mazingira ambayo tunaamini tunajua.
Labda utaniuliza, una maana
gani unaposema ‘ujuaji’? Je, kujua ni jambo baya? Nikujibu kabla sijafika
mbali. Kujua si jambo baya. Kimsingi ili mwanadamu akabiliane na mazingira yake
na awe salama, analazimika kujua mambo kadha wa kadha. Mwanadamu anahitaji
kujua wapi anaweza kupata mahitaji yake, nani ni rafiki yake, nani ni adui
yake, wapi kuna dalili za hatari na mambo kama hayo ambayo ni msingi wa usalama
wake.
Aidha, tunafahamu pia kuwa
mbali na kutaka kujua ili kujihakikishia usalama wetu wa kimwili, maarifa
yanatuhakikishia usalama wa kisaikolojia. Chukulia pale unapogundua umekosea.
Unajisikiaje? Hatupendi kuwa wajinga (wasiojua) ndio maana tunapohisi kuna
jambo hatulijui tunajisikia vibaya. Hata pale tunapopata taarifa sahihi
zinazothibitisha kuwa tulikuwa tumekosea, bado tunakuwa wagumu kukubali makosa
yetu. Maana yake kujua ni hitaji muhimu la kisaikolojia alilonalo mwanadamu.
Shida inakuja pale tunapofikiri
tuko sahihi na wengine wote wenye mtazamo tofauti na ule tulionao hawako
sahihi. Mawazo kama haya ndiyo ninayoyaita ujuaji. Ujuaji ni ile tabia ya mtu
kutaka kuonekana ana ufahamu wa mambo hata kama wakati mwingine yeye mwenyewe
anajua hujui.
Mtazamo kama huu ni dalili za
upungufu mkubwa wa uelewa. Kwanza, ni kutokana na ukweli kuwa binadamu pamoja
na kupenda kufahamu mambo mengi, bado tunafahamu mambo machache mno. Lakini
pia, ufahamu wetu kwa asili una tabia ya kutudanganya bila sisi kujua
tumedanganyika. Nikupe mfano rahisi.
Ukitazama picha hii hapa
pembeni, kwa haraka haraka unaweza kudhani unaona sura ya kijana wa ki-Hindi anayetazama
kushoto na nywele zake ndefu amezitimua kwa nyuma. Unachokiona ni kitu sahihi. Hata
hivyo, huo si mtazamo pekee kwa picha hiyo.
Ingawa ni kweli umeona uso wa
kijana wa ki-Hindi, bado unaweza kuona kitu kingine ukiwa tayari na kuufungua
ufahamu wako. Tazama kwa makini kuona kama unaweza kumwona mtu mfupi jamii ya
Waeskimo aliyegeukia ubao akiandika kitu kwa mkono wa kulia.
Tazama kwa makini.
Nikusaidie kumwona. Uso wa yule kijana wa ki-Hindi sasa utazame kama kichwa cha
mtu huyu mfupi aliyejifunika koti lenye manyoya mithili ya koti la ‘Father
Christmas’, shingo ya kijana wa ki-Hindi sasa itazame kama miguu ya mtu huyu
mfupi, na nywele za kijana wa ki-Hindi sasa zitazame kama ubao wa kuandikia.
Je, umemwona? Kama bado, tazama kwa bidii.
Huu ni mfano unaoweza
kutusaidia kuelewa namna gani jambo lile lile linaweza kuwa na tafsiri zaidi ya
moja kutegemea na kile tunachokitarajia au kutaka kukiona. Ndivyo ilivyo katika
maisha. Suala hilo hilo unaloamini liko vile unavyojua linaweza kuwa tafsiri
tofauti ikiwa tu utafungua milango ya kujifunza zaidi.
Unapojadiliana na watu,
usilazimishe kuwa sahihi hata kama unaamini uko sahihi. Kile unachokiona ni kwa
mujibu wa taarifa ulizonazo na imani uliyonayo tayari. Wengine unaofikiri
hawako sahihi nao wanaweza kuwa na taarifa tofauti na zile ulizonazo wewe. Ukilazimisha
waone kile tu unachokiona wewe unakosea.
Kama nilivyotangulia kusema,
tunalazimisha kuwa sahihi kuliko wenzetu kwa sababu tunafikiri bila kuwa sahihi
hatuwezi kuwa na heshima. Tunatumia ‘ujuaji’ kama silaha ya kulinda heshima
zetu. Lakini je, huwezi kuwa sahihi na mwenzako pia akawa sahihi? Hatuwezi kuwavumilia
wenzetu kwa kuona kile tusichokiona?
Nikirudi kwenye picha niliyoitumia
kwenye makala haya. Hakuna mtu anayeweza kudai kuwa kile anachokiona yeye
ndicho sahihi zaidi kuliko wanachokiona wengine. Mazingira tuliyokulia, mambo
tuliyozea kuyasikia yanaweza kufanya ikawa rahisi zaidi kuona kichwa cha kijana
wa ki-Hindi anayetazama kulia. Lakini hiyo haifanyi wanaomwona kijana mfupi wa
ki-Eskimo wasiwe sahihi.
Lugha sahihi tunayoweza
kuitumia ni kwamba wanaomwona kijana wa ki-Hindi wako sahihi, lakini pia
wanaomwona kijana mfupi wa ki-Eskimo nao wako sahihi. Hakuna walio sahihi
kuliko wengine hata kama hawaoni kile wanachokiona wengine.
Siku nyingine unapojadiliana na
wenzako masuala yoyote yale iwe ni imani/dini, siasa, utamaduni, taaluma
zingatia kuwa unachokiona wewe sicho wanachokiona wenzako. Taarifa ulizonazo
wewe, sizo alizonazo mwenzako. Upande unaoona kuwa ndio sahihi, kwa wengine ni
upande usiosahihi. Ukizingatia hilo, hutalazimisha kuwa sahihi wakati wote na
hivyo utakuwa mwepesi kuvumilia mawazo tofauti na yale uliyonayo.
Changamoto ya kizazi kinachojua kama kinajua kumbe hakijui kinachotakiwa kujua ni kupinga kile kinachotakiwa kujua kwa wanaojua.
JibuFutaHivyo kufanya wanaojua kutokuwa na nafasi kwenye fahamu zao.
Najifunza mengi kwako
Mwalimu wangu.
Nakubali kuwa siwezi kuwa sahihi wakati wote. Lakini Mwl, yako mambo ambayo ni dhahiri kama ilivyo "2+2=4" na wala hayahitaji mijadala. Lakini mtu kwa makusudi kabisa pengine kwa sababu ya nguvu fulani aliyonayo hutaka kufanya" 2+2=3"
FutaHapo ndipo shida huanza. Hawa, wana matatizo. Sio kwamba hawajui, la hasha, wanajua ila wanajifanya hawajui.
Titanium Straightener: A Perfect Combination Of The Best Batteries
JibuFutaIn its price of titanium simplest form, the tibia straightener is an active gr5 titanium form of titanium fidget spinner the naturally active micro touch hair trimmer Thiibean tooth comb, the thiibean titanium banger tooth comb and the