Mbinu za Kushinda Maswali ya Usaili wa Kazi - 2
Katika makala yaliyopita tuliona
maeneo manne muhimu ya kuzingatia unapoingia kwenye usaili. Kwamba pamoja na
maswali mengine, unaweza kuulizwa maswali kuhusu uzoefu wako wa kikazi huko
ulikotoka. Tuliona kuwa unapoulizwa maswali kama hayo, lengo ni kupima namna
unavyoweza kuwa mkweli.
Usikimbilie kumponda mwajiri wako wa
zamani kwa kutoa sababu za kutokuridhika na mshahara, migogoro ya kazi
uliyokuwa na mwajiri wako, kutokuelewana na wakubwa wako wa kazi au watu
uliokuwa unawasimia.Ukifanya hivyo utaonekana wewe ni mtu wa matatizo.
Badala yake, toa sababu chanya
zinazoleta picha ya mtu mkomavu kazini. Mfano, unaweza kuonesha kuwa uliacha
kazi uliyokuwa nayo kwa sababu ulipata fursa ya kutumia vipaji vyako vizuri
zaidi kwingineko, au kwamba kazi
uliyoipata ingekupa kukua kiujuzi zaidi.
Katika makala haya, tutatazama
maeneo mengine manne unayohitaji kujiandaa ili kushinda maswali utakayoulizwa
kwa mafanikio.
Matarajio yako kwa mwajiri
‘Unadhani tukulipe mshahara kiasi gani?’
Hili swali linatafuta kujua
vipaumbele vyako uwapo kazini. Ni kweli unatafuta kazi ili upate fedha uboreshe
maisha yako. Lakini kuonesha kuwa ari na kujituma kwako kazini kunategemea na
kiasi cha pesa unacholipwa ni kosa la kiufundi. Kosa hili linaweza kuwa kikwazo
cha kukupa kazi.
Unahitaji kuonesha ukomavu kwa
kuelewa kuwa taasisi bora [kama hiyo unayotaka ikuajiri] zina utaratibu rasmi
wa kuwalipa wafanyakazi wake. Mtu hulipwa kwa sifa alizonazo. Kwa uelewa huo,
utapata alama za ziada.
Hata hivyo, pamoja na majibu hayo
wapo wasaili wanaweza kukubana uwaambie matarajio yako. Fahamu kuwa kujadili
mshahara wa kazi ambayo bado hauna uhakika nayo, haiwezi kukusaidia.
Ikiwa utalazimika kutaja tarakimu,
inatarajiwa kuwa tayari utakuwa umeshafanya utafiti wa taasisi hiyo ikiwa ni
pamoja na viwango vya mishahara. Taja kiwango ambacho hakitaonesha huna
thamani, lakini pia usitaje kiwango kitakachoonesha kujikweza kupita kiasi.
Uelewa wa mambo na ujuzi wa kazi
Unaweza kuulizwa maswali yanayopima
uelewa wako wa kawaida kwa mambo yanayofahamika. Lakini pia unaweza kuulizwa
masuala ya moja kwa moja yanayohusiana na kazi unayoomba.
Wakati mwingine, baadhi ya wasaili
hutumia mtihani wa kuandika kujaribu kuthibitisha kama kweli una uwezo na ujuzi
uliouonesha kwenye wasifu wa kazi.
Maswali yanayoulizwa yanaweza kupima
moja kwa moja utaalam uliousomea darasani au namna unavyoweza kutatua
changamoto halisi za kazi. Jiandae ipasavyo kwenye maeneo muhimu.
Kilicho muhimu ni namna unavyoweza
kutafsiri nadharia zako katika mazingira ya kazi.
Kwa mfano, unaomba kazi ya uhasibu
msaili mmoja anakuuliza, ‘Chukulia ofisini kwako kumetokea wizi wa fedha.
Utachukua hatua gani?’ Au unaomba kazi inayohusika na utawala, ‘Chukulia kama
kiongozi umesikia wafanyakazi wa chini yako wana mpango wa kugoma. Utafanyaje?’
Hayo ni maswali ya uchokozi.
Usitumie muda mrefu kutafuta masuluhisho yasiyokuwepo. Jibu kwa ujasiri kuwa
hutarajii kuwa matatizo ya namna hiyo yatajitokeza. Lengo ni kuonesha una uwezo
wa kuikinga taasisi yako na changamoto kama hizo.
Malengo yako ya baadae
‘Unajiona ukifanya nini baada ya miaka 10 ijayo?’
‘Una malengo gani ndani ya miaka
mitano ijayo?’
Hapa unahitajika kuonesha ari ya
kukua kiujuzi na kiweledi. Ongelea mipango ya kujifunza zaidi kufikia kwenye
malengo makubwa yanayoendana na malengo mapana ya kitaasisi. Kuzungumzia
malengo yasiyoendana na kazi unayoomba kutakupunguzia alama.
‘Umeomba kazi kwingine?’
Wanahitaji kuwa na uhakika na maamuzi
yako. Ni kweli inawezekana utakuwa umeomba kazi maeneo mengine. Lakini
utaonekana mkomavu ukiweza kuonesha kuwa kazi hii unayosailiwa ndio chaguo la
kwanza.
‘Utafanya kazi na sisi kwa muda
gani?’
Hapa wanataka kujua kama wewe ni
mpitaji au la. Inawezekana kweli unaweza kuwa na mpango wa kufanya kazi kwa
muda mfupi na utafute njia nyingine.
Lakini kuonesha wazi kuwa unapita
wakati hata kazi hujapata si busara. Onesha ungependa kufanya kazi kwa muda
mrefu kadri utakavyohitajika.
‘Unaota kufanya kazi gani nzuri
baadae?’
Ukitaja kazi nyingine mbali na hiyo
unayoomba, unaleta wasiwasi kuwa hutaridhika na kazi unayoomba. Ongelea
mazingira ya kazi bila kutaja kazi mahususi. Mfano, kazi inayokufanya utumie
vipaji vyako na ujuzi ulionao. Kazi inayokufanya ukue kiujuzi na kiuzoefu.
‘Uko tayari kuanza kazi lini?’
Kama huna kazi, ukisema uko tayari kuanza kazi
mara moja inaonesha utayari ulionao. Lakini kama unabadilisha kazi, kuonesha
utahitaji muda mfupi wa kukamilisha taratibu za kukabidhi majukumu uliyonayo na
kuaga itakupa alama.
Fursa ya kuuliza swali
Kwa kawaida, baada ya kuulizwa
maswali mengi, kikao cha usaili
kitahitimishwa kwa kukukaribisha kuuliza swali. Kama tulivyosema, kila swali
lina maana. Unapoulizwa, ‘Je, una swali ungependa kuuliza?’ lengo ni kutaka
kujua ulivyo na ari ya kufanya kazi na taasisi hiyo.
Usipouliza swali lolote, maana yake
ama huna uelewa wa mambo mengi au huna ari ya kutosha. Uliza swali kuhusu
taasisi hiyo. Waliuze wanatarajia nini kwa mtu atakaye pata kazi hiyo.
Kadhalika, waweza kuulizia mambo yanayohusiana na fursa wanazoweza kutoa kukuza
ujuzi wako kama mfanyakazi wao.
Epuka kuuliza maswali ya kimaslahi.
Kuuliza, ‘Mnanilipa bei gani?’ ni kuonesha huna mtazamo mpana na kazi. Unaweza
hata usijibiwe au ukajibiwa jibu litakalokunyong’onyeza.
thanks for your sharing. i think this article must be share to other people.
JibuFutaGALERIQQ.COM
thanks for share :D
JibuFutaSitus BandarQ Terpercaya
Situs Poker Online Terpercaya
Situs Agen DominoQQ Online Terpercaya
Situs Poker Online
Situs Poker BandarQ Terpercaya
Yuk Buruan ikutan bermain di website http://sahabatpoker.poker
JibuFutaSekarang SAHABATPOKER Memiliki Game terbaru Dan Ternama loh...
=> Bonus Refferal 15%
=> Bonus Turn Over 0,5%
=> Minimal Depo 20.000
=> Minimal WD 20.000
=> 100% Member Asli
=> Pelayanan DP & WD 24 jam
=> Livechat Kami 24 Jam Online
=> Bisa Dimainkan Di Hp Android
=> Di Layani Dengan 5 Bank Terbaik
Ayo gabung sekarang juga hanya dengan
mengklick Poker Online
PIN BB : 2B13CFDA