Jifunze Namna Bora ya Kumzawadia Mwanao
Watoto wanapenda zawadi. Namna watoto
wanavyochukulia zawadi inabadilika kulingana na umri. Katika umri mdogo, mtoto huchukulia
zawadi kama haki ya kupata kila akipendacho kwa wakati wowote. Mzazi anaporudi
nyumbani jioni, kwa mfano, watoto hutarajia pipi bila kufanya chochote.
Lakini kadri mtoto anapoendelea kukua, mtazamo wa
zawadi kama haki hupungua. Mtoto huanza kufikiria zawadi kama matokeo ya
kufanya kile kinachotarajiwa na mzazi. Mtoto anapofaulu mtihani, mathalani,
anatarajia kitu. Unapompa kile anachokitarajia, anajenga hamasa na motisha ya
kutia bidii zaidi masomoni.
Aidha, uzito wa zawadi kwa mtoto hutegemea na
wakati. Zipo nyakati ambazo zawadi hubeba maana zaidi kwa watoto kuliko wakati
mwingine. Kwa mfano, katika familia nyingi, msimu wa sikukuu unapokaribia watoto
hutarajia zawadi zaidi kuliko wakati mwingine wowote. Hawezi kuelewa pale
inapotokea mzazi anashindwa kutoa zawadi inayotarajiwa.
Katika mipaka ya makala haya, zawadi ni chochote
kile anachopewa mtoto kwa minajili ya kukuza uhusiano wake na mzazi na hata
kujenga motisha ya kuimarisha tabia njema. Pamoja na manufaa hayo ya zawadi, utoaji
holela wa zawadi unaweza kutengeneza matatizo ya kitabia.
Katika makala haya tunajadili mambo matano ya
kuzingatia unapomzawadia mwanao.
Fahamu
kipi ni zawadi kwa mwanao
Sio
kila kitu unachompa mtoto kinaweza kutafsirika kama zawadi kwake. Ili zawadi yako
iwe na maana, ni muhimu kumfahamu mtoto vizuri kujua mambo yepi anayapenda
zaidi. Kwa mfano, katika umri mdogo, watoto wengi hupenda vitu vitamu.
Unapowaletea pipi, keki, biskuti unakuwa umewaweza. Lakini wanapokua, wanajenga
matarajio mengine. Ni muhimu kuyaelewa.
Hakikisha
zawadi inaendana na kile anachokipenda mtoto. Kila mtoto ana mambo anayopenda
kuyafanya katika muda wake binafsi. Kama mwanao anapenda kuchora, kwa mfano,
inaleta maana kumletea zawadi ya rangi badala ya michezo ya kidijitali hata
kama kwako michezo hiyo inafurahisha zaidi.
Kadhalika,
uzito wa zawadi kwa mtoto pia hutegemea nyakati. Katika sherehe ya kuzaliwa,
kwa mfano, mtoto anakuwa na matarajio tofauti na yale anayokuwa nayo wakati
mwingine. Unapofanya kama anavyotarajia, ni rahisi kuchukulia kwa uzito na
hivyo akajisikia vizuri.
Ifanye
zawadi iwe adimu
Zawadi inayotolewa mara kwa mara inakuza matarajio.
Mtoto anapojua kuwa lazima atapata zawadi kila unaporudi nyumbani, hujenga
mazoea ya zawadi. Ili muendelee kuwa marafiki, utalazimika kuendelea kwenda na
zawadi kila siku.
Mazoea haya yanajenga tabia ya utegemezi wa zawadi.
Inapotokea umeshindwa kumpelekea zawadi kama alivyotarajia, uhusiano wenu
unaweza kuzorota. Katika mazingira haya, maana ya zawadi inapotea kwa sababu mtoto
anakuwa amejenga matarajio kwenye zawadi.
Sambamba na hilo, ni muhimu zawadi iwe ndogo. Hakuna
sababu ya kutoa zawadi kubwa itakayokugharimu pale itakapozoeleka. Zawadi ndogo
inayoambatana na uhusiano mzuri na mwanao, inaleta mantiki kuliko ukubwa wa
zawadi.
Kadhalika, badala ya kujenga mazoea ya kutoa zawadi
ya vitu, unaweza kuanzisha mazoea ya kutoa zawadi zisizonunulika. Kwa mfano,
unaweza kumpa mtoto pongezi za mdomo zinazoonesha kutambua kilichofanywa; kuwa
na wakati mzuri na mwanao nje na nyumbani; kumkumbatia kwa upendo; kumruhusu
kuwa na muda na rafiki zake na matendo kama hayo yanayoimarisha uhusiano wenu.
Ifahamike imetolewa kwa sababu gani
Lengo
la zawadi ni kukuza tabia inayotarajiwa. Unapompa mwanao zawadi kutambua tabia
njema aliyoionesha unamjengea ari ya kufanya vizuri zaidi. Hakikisha mwanao
anajua kwa nini umempa zawadi. Zawadi isiyojulikana ina malengo gani haiwezi
kumsaidia mtoto.
Kama
mwanao amefanya vizuri shuleni na unadhani anastahili motisha, mpe zawadi
inayoambatana na ufafanuzi. Kama mwanao ameonesha jitihada za kukuza tabia
fulani njema, mpe zawadi kwa maelezo.
Unapohakikisha
kuwa mwanao anafahamu kwa nini umempa zawadi, utamfanya awe na ari ya kuendelea
kuonesha tabia hiyo kwa matarajio ya kupata zawadi zaidi kwa wakati mwingine.
Iwe na manufaa kwa mtoto
Mpe
mtoto zawadi yenye manufaa na itakayomsaidia kujifunza. Kwa mfano, vifaa vya
shule kama kalamu, rangi za kuchorea, vitabu, vifaa vya michezo, madaftari, CD
za elimu vitakavyomsaidia kujenga uelewa na kukuza vipaji vyake.
Kadhalika,
fikiria kumpa mtoto kiasi kidogo cha fedha taslimu atakachowajibika kukitunza.
Ingawa jambo hili linahitaji kufanyika kwa tahadhari, lakini humsaidia mtoto
kujenga tabia ya kuwa na nidhamu ya fedha mapema.
Itoe wakati usiotarajiwa
Upo
ukweli wa kisayansi kuwa wakati tabia mpya inajengwa, unalazimika kuhakikisha
kuwa zaiwadi yako inatolewa kila mara tabia hiyo inapojitokeza. Kwa kufanya
hivyo, unajenga motisha inayosaidia kumsukuma mtoto kufanya kile
kinachotarajiwa.
Hata
hivyo, baada ya mtoto kujifunza tabia hiyo mpya, unahitaji kubadili utaratibu.
Ukiendelea kuitoa kila mtoto anapoonesha tabia hiyo, zawadi kujenga utegemezi.
Badala ya mtoto kujifunza tabia husika, anajifunza kungoja zawadi.
Inapokosekana, tabia iliyojengwa hupotea mara moja.
Ni
vizuri kuhakikisha kuwa zawadi haifahamiki itatolewa lini. Hakuna sababu ya
kumjengea mtoto mazoea ya kupata zawadi nyakati za sikukuu. Kama anahitaji
mavazi, mnunulie wakati mwingine wowote. Ukifanya hivyo, hutadaiwa zawadi
nyakati za sikukuu zinapowadia.
Fuatilia Jarida la Maarifa ndani ya gazeti la Mwananchi kwa makala kama hizi.
Shukrani kwa makala. Ni mada muhimu, na hapo ulipogusia suala la zawadi za manufaa, na ukataja vitabu na vifaa vingine vya elimu, umenikumbusha ujumbe niliowahi kuandika kuhusu vitabu kama zawadi ya siku kuu.
JibuFutaAsante sana Prof Mbele kwa kusisitiza umuhimu wa zawadi zinazojenga utamaduni wa kujifunza. Naamini ujumbe wako utawafikia wazazi wengi.
JibuFutathanks for your sharing. i think this article must be share to other people.
JibuFutaBest regards, http://galeriqq.com
TiketQQ*net Agen BandarQ Domino99 Bandar Poker Dan Bandar66
JibuFutaOnline Terbaik Di Asia
- Dengan Minimal Deposit : Rp 15.000,-
- Tersedia 8 Game Dalam 1 User ID
- Bonus Rollingan 0,5% Setiap 5 hari
- Bonus Referal 20% Seumur hidup
Nyetornya cukup sekali, nariknya berkali-kali
TiketQQ*net Agen Bandarq Domino99 Bandar Poker Dan Bandarq
Online Terbaik Di Asia
- Kontak Kami -
PIN BBM : Tiket99
WA : +855966348165
LINE : Tiketqq
Website : TIKETQQ
FB : TIKETQQ
Twitter : TIKETQQ
Agen Bandarq
JibuFutaAgen Poker
โปรโมชั่น pg slot รวมโปรสล็อต PG โปรโมชั่นดีๆสุดพิเศษและก็ร้อนแรงมาเสนอแนะสำหรับคุณ สำหรับสาวกสล็อตตัวจริงต้องห้ามพลาดกับโปรโมชั่นที่พวกเราเตรียมความพร้อมมายกให้คุณทุกวัน
JibuFuta