Kuanza Kupotea kwa Desturi ya Ukaribu wa Kifamilia Kunavyoathiri Malezi
Malezi
katika mazingira yetu ya ki-Afrika ni suala nyeti. Kwa kutambua umuhimu wa
malezi katika kujenga jamii yenye ustawi, wa-Afrika tumekuwa na desturi ya kuelekeza
nguvu zetu nyingi katika malezi ya wanetu. Kwa mfano, tangu mtoto anazaliwa, ilikuwa
ni lazima alale kitanda kimoja na wazazi wake kwa muda unaozidi miaka miwili. Mtoto
mchanga hakuachwa alale kwenye kitanda chake mapema kwa sababu za msingi
zilizokubalika katika jamii zetu.
Aidha, mtoto daima alikulia mikononi mwa watu wazima aliowafahamu vyema. Watu hawa ama aliishi nao kwenye boma la wazazi wake au walitoka miongoni mwa jamaa inayomzunguka. Muda mwingi mtoto alibebwa mgongoni kwa mama yake au dada zake. Desturi ya kubeba watoto mgongoni ilifanya suala la ukuaji wa mtoto kufuatiliwa kwa karibu sana na imethibitika kisayansi kusaidia kujenga muunganiko wa kihisia kati ya mzazi na mtoto. Jambo hili, hata hivyo, halieleweki kwa wageni wa bara hili wanaodhani ni aina nyinine ya udhalilishaji wa mtoto.
Mama akiwa amembeba mwanae. Picha: CORBIS |
Wakati
wa jioni, familia zilikuwa na desturi ya watoto kukaa na wazazi wao kijinsia.
Baba aliota moto na watoto wa kiume akiwasimulia mambo mbalimbali ya kimaisha.
Kadhalika, mama naye alifanya kazi za jikoni kwa ushirikiano wa karibu na
watoto wa kike.
Chakula kilipokuwa tayari kililiwa kwa ushirikiano. Muda wa chakula ulifahamika, na kwa kweli, kila mtoto aliwajibika kuwepo kupata chakula. Kwa kuwa chombo kilichotumika kulia chakula mara nyingi kilikuwa kimoja basi kila mmoja katika familia alilamizika kula kwa ushirikiano na wenzake.
Chakula kilipokuwa tayari kililiwa kwa ushirikiano. Muda wa chakula ulifahamika, na kwa kweli, kila mtoto aliwajibika kuwepo kupata chakula. Kwa kuwa chombo kilichotumika kulia chakula mara nyingi kilikuwa kimoja basi kila mmoja katika familia alilamizika kula kwa ushirikiano na wenzake.
Desturi
hii ya kukaa karibu na watoto na kufanya mambo mengi kwa pamoja iliwasaidia
wazazi kuwafundisha watoto maarifa na ujuzi wa aina mbalimbali. Vile vile,
ukaribu huu ulikuza uhusiano wa karibu wa kifamilia. Kadhalika, karibu huu uliwahakikishia
watoto usalama wao. Kisaikolojia walijua hawana wasiwasi kwa sababu baba na
mama wapo na wangepigana na yeyote anayetishia usalama wao. Watoto
waliwategemea wazazi wao.
Upo
ushahidi wa kiutafiti kwamba
kutegemewa kwa mzazi ni nguzo kuu ya malezi. Kwamba mtoto huiga mengi wa mzazi
ikiwa anaamini mzazi huyo ni wa kutegemewa na yuko upande wake. Hali hii ilimfanya
mtoto asiwe na wasiwasi na usalama wake pale yalipojitokeza mazingira ya kutengana
kimwili na kwa hivyo wazazi kwa kweli hawakulazimika kuwa na watoto muda wote.
Kama tutakavyoona katika mfululizo huu, hali hii ya mtoto kumwamini na
kujisikia salama mikononi mwa mzazi inategemea sana uwepo endelevu wa mzazi kimwili
na kihisia tangu siku za mwanzo za maisha ya mtoto.
Hata
hivyo, kadri mwanadamu anavyozidi ‘kuendelea’ na ‘kustaarabika’, ndivyo desturi
hii ya kupatikana kwa wazazi nyumbani inavyozidi kukosa umaarufu. Kwa mfano, ipo
dhana inajengeka katika jamii kwamba maendeleo halisi ni vitu. Matokeo ya imani
hii ni kutufanya tutumie muda mwingi ‘kuhusiana na vitu’ zaidi kwa gharama ya
mahusiano na ustawi wa familia zetu.
Kadhalika,
zipo changamoto nyingine za kijamii zinazotishia desturi ya familia. Kuna
masuala kama kazi/ajira zinazowatenganisha wazazi na familia, misukosuko ya
kimahusiano inayozaa talaka na/ama kulazimisha malezi ya mzazi mmoja, ujio wa shule
za bweni kwa watoto wadogo pamoja na matatizo kadha wa kadha yanayofanya watoto
wadogo wakue katika mazingira magumu yasiyo na uangalizi mzuri. Haya tutayaangalia
wakati wake ukifika.
Kwa
hiyo, ili kukabiliana na changamoto hizi mpya, upo umuhimu mkubwa wa kujadili
tafiti zilizochunguza athari za mazingira haya mapya ya kimalezi ambayo kwa
kiasi kikubwa hayakuwepo huko nyuma. Kwa mhutasari, tunaweza kutaja suala kuu linalojitokeza
kwa haraka. Kwamba uhusiano kati ya mzazi na mtoto unaathiri mahusiano ya mtoto
huyo na watu wengine.
Inaendelea
Twita: @bwaya
Nimeipenda mno hii...maana siku hizi desturi zetu zinaharibiwa sana..ahsante kaka Bwaya
JibuFutaAsante sana Yasinta kwa kuisoma. Tupo pamoja
JibuFutaarticle nzuri sana.......
JibuFuta