Usawa wa viumbe mbele za Mungu uko wapi?

TURUDI kwenye ule mjadala wetu wa suala la Mungu ambalo bado ninalitafutia wakati mzuri zaidi. Kuna changamoto ndogo nadhani itastahili kutazamwa. Nayo inahusu usawa wa viumbe mbele za Mungu wao.

Tunaamini kwamba Mungu alituumba sisi wanadamu pamoja na viumbe wengine mfano mimea pamoja na aina nyingine za wanyama. Na inavyoonekana, mbingu iko kwa ajili ya sisi wanadamu zaidi. Sasa hoja ni kwamba nafasi ya hawa viumbe wengine iko wapi katika ufalme wa mungu? Kwa sababu hatuelezwi wazi kuwa viumbe wengine watafaidikaje na umilele tunaoutarajia (sisi wanadamu) ambao tu viumbe kama wao.

Jibu la haraka haraka ambalo mtu anaweza kulitoa kama majibu ni kwamba viumbe wengine hawana upeo/utashi wa kutambua. Lakini jibu hili nadhani haliwezi kuwa sahihi. Kwa sababu hebu tuchukulie mfano ng'ombe anapopelekwa machinjioni. Anapofikishwa pale, kiumbe huyu huonekana kupatwa na mfadhaiko mkubwa kiasi cha kuweza hata kubomoa uzio ushahidi kwamba anajua kinachoendelea. Kwamba kuna kundi la viumbe wenzake wanataka kumtoa roho!

Kwa maana hii tunaweza kuhisi kwamba hata mimea nayo ina namna yake ya kukabiliana na dhahama kama hizi za "kuuawa" na viumbe wenzao. Pengine hatujaweza kutambua inavyowasilisha hisia zao kwa viumbe wengine.

Na zaidi inaeleweka kwamba viumbe wengine hawatendi dhambi. Kama binadamu wenye dhambi ndio wanaohukumiwa kuikosa mbingu, kwa nini wanyama "watakatifu" wasipewe haki ya kuurithi ufalme wa Mungu wao?

Usawa wa viumbe wote mbele za Mungu uko wapi? Je, ni kweli kuwa binadamu amependelewa kuliko wengine? Kwa kipi hasa, maana ni yeye ndiye anayeongoza kuiharibu dunia kwa kutumia utashi wake. Ameharibu mfumo wa asili uliokuwepo kwa kujidai kuwa anaitawala dunia. Ni yeye huyo huyo anayeongoza kuwanyanyasa viumbe wengine kwa kiburi kuwa eti ndiye mtawala. Ni yeye huyu huyu binadamu ambaye anaongoza kwa kumwasi Mungu kiasi cha kumfanya mungu awaadhibu na viumbe wengine wasio na hatia.

Je, ni kweli binadamu wanaupendeleo zaidi mbele za Mungu?

Maoni

  1. Mi si mtaalamu wa theolojia lakini ninayo imani, nadhani si haba.
    Nianzeje? Kwa kusema kuwa binadamu amepewa upendeleo wa dhahiri kutoka kwa Muumba.
    Binadamu, kadri Mungu alivyoumba ulimwengu, alimwumba kwa namna tofauti na viumbe wengine.
    Kwanza, alimuumba kwa mfano wake. Alimwumba kwa kuufinyanga udongo ilhali viumbe wengine waliumbwa kwa kutamka.
    Lakini pia, Mungu aliumba wanadamu na kuwapa utashi. Akawapa mamlaka juu ya viumbe wengine wote. Hivyo ni halali kwa binadamu kuyatawala mazingira.
    Na hii inathibitishwa pia na theolojia kuhusu kiyama ya wafu. Haiwagusi viumbe wengine isipokuwa binadamu.
    Nadhani nao ni ushahidi tosha wa kiimani kuwa binadamu ni bora zaidi ya viumbe wengine.
    Naomba niweke tuo hapa.

    JibuFuta
  2. Hii mada inahitaji tafakuri.
    Niliwahi kuambiwa kuwa hata wale Makaburu wa Afrika ya Kusini walikuwa wantumia Biblia katika kuhalalisha siasa zao za kibaguzi.
    Walikuwa wanatumia, vifungu gani katika maandiko, sijui, labda anayefahamu zaidi atujuze.
    Mimi bado nina mashaka sana na kitu kinachoitwa Dini, ndio sababu nimeamua kubaki neutral, Yaani sifungamani na upande wowote.
    Naomba msiniulize sababu.
    Jamani nimechoka kudanganywa!!!!!

    JibuFuta
  3. haya mambo bwana, kwani kunamnyama gani alishirikishwa katika kuandika maandiko tunayoyaamini? si binadamu tu? zamani Mzungu alikuwa karibu na mungu kuliko mwafrika siku hizi hapana. nani anayepima na kujua jinsi binadamu alivyokuwa na akili kuliko wanyama wengine? uliwahi kusikia mnyama gani anakubali kwamba binadamu ana akili zaidi? si binadamu mwenyewe anajitapa tu na kujipaisha?

    je ni kweli binadamu ana akili na yuko karbu na Mungu? sikubaliani na hilo. ndio maana kuna Mungu wa Israel na waarabu harafu sisi tunadhani ni Mungu wetu pia. ndio maana tunaamini kwamba tanzania ni nchi ya Mungu wakati kimaumbile hakuna tanzania, bali kuna sehemu kubwa ya ardhi iitwayo afrika. Tanzania ni himaya ya kikoloni.

    ndiyo maana watu wanaomjua Mungu kama maaskofu nk kuliko wengine,hii inadhihirisha ukweli kwamba sisi kama binadamu ndiyo tunaomuumba mungu na sio kinyume chake kwani kumbu kumbu zote tunafundishwa na kuamulishwa tuzifute na sio kuzijua automatikale kwa hiyo ili kujua kama kuna mungu wa wanadamu ni lazima uambiwe/ufundishwa na binadamu mwenzio na sio Mungu!

    ndiyo maana biblia inasema yesu ni mwana wa mungu wa kipekee wa kiume, wakati bwaya, kaluse, Mtanga, kamala Nk ni wanae pia.

    Mungu mwenye upendeleo harafua ana upendo mwingi na hasira hapo hapo! mimi sijui niseme nini jamani, labda nikae kimya kwanza, haiingiii akilini, hii inabidi huiamini bila kulazimika kufikiri kwanza ili hudhiirishe ujinga wako wa kutokufikiri

    udogoni tuliimbishwa nyimbo za natamani kwenda yerusalem, ni kadhani mji huu uko mbinguni, kumbe ni duniani tena kwenye vita vya ajabu, nikaogopa kupatamani tena

    naishia hapa

    JibuFuta
  4. Ukisoma kitabu cha Ufunuo wa Yohana katika biblia, utaona wazi kwamba mbingu ina milango kumia na miwili watakayoitumia yale makabila kumi na mawili ya Israel kuingilia (kila kabila wa mlango wake).

    Sasa sisi akina kayumba tutaingilia mlango upi mbinguni?

    JibuFuta
  5. Ukisoma kitabu cha Ufunuo wa Yohana katika biblia, utaona wazi kwamba mbingu ina milango kumia na miwili watakayoitumia yale makabila kumi na mawili ya Israel kuingilia (kila kabila wa mlango wake).

    Sasa sisi akina kayumba tutaingilia mlango upi mbinguni?

    JibuFuta
  6. Yaliyoandikwa ktk bibilia ni historia kama zilivyo historia ktk vitabu vingine hususani vile vinavyoelezea maisha ya mababu zetu wa zamani.Sielewi ni kwa nini tumebase sana upande huu mmoja na kuudharau upande wa pili wa historia ya mababu zetu.Tukizingatia kwamba dini ilikuwa miongoni mwa mbinu zilizotumiwa na wakoloni ktk kutimiza azma yao ya kutukandamiza na kutudhalilisha sisi pamoja na utamaduni wetu tuliokuwa nao na kupelekea sisi kujidharau na kudharau utaratibu wetu wa maisha(utamaduni wetu).
    Historia iliyo ktk vitabu vya dini inawaelezea walewale waliotukandamiza huku waziwazi ikionekana mwafrika kutokupewa nafasi kabisa ktk vitabu hivi vya dini.Najaribu kujiuliza hali ya sasa ingekuwaje kama wazee wetu wasingepokea mafundisho haya ya dini za kigeni na kubaki na utaratibu wao wa dini?Kama Mungu ni wa wote basi mbona hizi dini za kigeni zilianzia huko kwa wenzetu?Kuna swali jingine la kujiuliza,kabla ya kuja kwa dini za kigeni,mababu zetu walikuwa wakiabudu kwa namna yao,je walikuwa wakifahamu kuwa kuna Mungu anayezungumziwa kwenye vitabu vya dini? Acha tu! Hii mada! Njia panda! Msaada!

    JibuFuta
  7. Hili swala hapa naona linatazamwa kwa jicho la baadhi ya dini. Kuna waliokua katika dini ziwakatazazo hata kukanyaga panzi kutokana na imani kuwa labda Simon maisha yaliyopita alikuwa mjusi.Mtu atokaye katika imani ambazo si za kikristo huwa ana jicho tofauti sana katika swala.

    Binadamu mara nyingi anatatizo la kujiweka yeye mbele ndio maana hata UJAMAA wa NYERERE ulushindikana. Kwa wengi labda USAWA mbele za Mungu ni mimi kwanza halafu ndio wewe. Na kwa dini zifuatazo vitabu fulani , kuna msitari unaweza ukakufariji ukijipendelea wewe kuliko senene.

    JibuFuta
  8. IKO WAZI, TUMEPENDELEWA NA KUPEWA FREE WILL AMBAYO HAKUPEWA YEYOTE KATIKA VIUMBE. VIUMBE WENGINE NI KWA FAIDA YETU, CHAKULA N.K. LA SIVYO TUNGEKUFA WOOTE.

    USAWA UNAOZUNGUMZWA NI ULE WA BAINA WATU TUU.

    NA HIYO FREE WILL NDO MTIHANI WETU, TUKIITUMIA VIBAYA: JAHANAM, TUKIITUMIA VIZURI: PEPONI.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Pay $900? I quit blogging

Haiba ni nini?

Heri ya mwezi mpya!