Singida: Here I come

Niko Singida. Baada ya kufika niliona ingefaa kupata huduma ya intaneti cafe. La haula! Nakutana na picha za ngono. Nahisi jamaa aliyekuwa akitumia kompyuta hii ndio kazi kubwa iliyomleta hapa. Uzuri, kama kweli ni uzuri, kompyuta za hapa zimewekewa uzio. Privacy. Unafanya kile unapenda bila hofu ya kuichunguliwa. Waswahili ukiwapa uhuru, ndo umeharibu kabisa.

Jamaa aliyeondoka hapa ni mtu na heshima zake. Tai. Suti na vitu kama hivyo. Mtu na ofisi yake bila shaka. Sitaki kuamini kwamba ndicho alichokuwa anakifanya hapa. Ni lini net zitatumika kwa mambo ya maana, hilo ndilo twapaswa kujiuliza. Vijana wanajazana net siku hizi. Usifikiri (wengi wao) wanafanya vya maana. Ngono ndugu msomaji.

Hivi hata nilitaka kuandika nini hata nimeshahau. Kwa nini ngono? Labda anajifunza lakini. Tuchukulie anajifunza. Sasa kujifunza kupi kwa picha za mnato wajameni? Mjadala hapa. Au tuwashauri wenye net waondoe uhuru? No. Hilo sio jibu. Siku hizi kuna simu. Watu "wanafaidi" mambo haya wakiwa vyumbani mwao. Kama huamini chukua simu ya kijana, mwenye kiwango kizuri tu cha elimu, halafu peruzi. Si ajabu ukakutana na "makarabrasha" kamili yaliyosheheni picha za ngono. Kwa nini hali iko hivi? Majibu tunayo wenyewe.

Nilichotaka kusema, ndugu msomaji, singida kuko poa kabisa. Kesho ni siku kuu naambiwa. Binafsi mimi siku hii inanitia mashaka sana. Kwanza chanzo chake. Pili namna inavyosherekewa.

Mwaka jana niliandika kuhusu Krismasi. Kwangu mimi, kusherekea siku hii bila kwanza kumpa kipaumbele mwenye sherehe, hakumpi tija. Unafikirije ndugu msomaji.

HNimepotea njia tena. Nilipokuwa nikisafiri kuja hapa, nilikuwa nikisoma kitabu cha mwandishi nimpendaye sana, Norman Vincent Peale, kiitwacho "The positive way to change your life". Nilikinunua Christian Bookshop, Mtaa wa Mkwepu. Ukipenda vitabu vya Non-fiction nenda pale. Huyu bwana anazunguzia mambo ya utambuzi. Kwa hiyo Kaluse fanya fanya uwasome na wenzako.

Haya. Kwa leo niishie hapa. Ntakupa mawili matatu kutoka hapa kwetu Singida. Ujue kabisa: Home is best. Nyumbani bwana asikwambie mtu. Poa.

Maoni

  1. Nimekusoma Mzee, Ahsante kwa habari za Singida na mawili matatu uliyotumegea uliyokutana na yo katika hiyo Cafe, nadhani habari hiyo inaweza kuanzisha mjadala mpya si unajua wanblog hawapendi kitu kipite hivi hivi.
    Kuhusu hicho kitabu cha utambuzi nitakitafuta ili nimsome huyo jamaa, kwani huenda nikapanua wigo wangu wa utambuzi.
    Tunaomba usisahau kutuletea zawadi za huko Singida.

    JibuFuta
  2. Haya mambo mkuu acha kabisa. nikupe stori moa ua??? sema mbona uanchekacheka? nikwambie kitu????
    Poa ni hivi, mwaka 2006 niliwahi kufanya mazoezi ya utangazaji redio fulani kule kwetu tena ya dini mkuu {dada Yasinta anaijua sana}. Sasa kwakuwa pia nilikabidhiwa jukumu la kutafsiri pia habari za kimataifa kwa ajili ya taarifa ya habri na michezo, kwahiyo nilikuwa natumia sna kompyuta kuliko kukaa studio. Mmmmmmm mwanawane kila nikifika nakuta amefunguliwa lakini aliyefungua alikuwa akicheki ngono, sijui inakuwaje hapo. SWALI yule jamaa aliyeanzisha blogu ya UTAMU vipi, unaona mkuu tulivyo? nakumbuka ulisema kwamba watu wa maana sisi ndiyo tunaoangalia vitu visvyo na maana ni kweli kabisa. Swali hivi ilikuwaje hadi tukafikia hapa? nyongeza; ilikuwaje hata wanawake wakaanza kuvaa nguo za kubana mata**** hadi chu*** zionekane? Nini kitafuata baada ya kuvaa hivyo au kuangalia picha hizo??? aaaah naacha mkuu topiki ngumu hii maliza mwenyewe au tumwite kaka Simon,dada Yasinta, Mzee wa changamoto na Kalama wamesme nao.

    JibuFuta
  3. nilisahau kuna dada mmoja alikuwa akinishangaa sana kila mara nikija nikigundua mtu kaangalia picha hizo! akaniuliza inakuwaje nanuna? nikamwambia sifurahishwi na mwenendo huo? Duh alinishangaa sana akasema hanielewi, lakini nikamwambia kwanini upo Argentina kusoma?[maana alikuwa likizo anasoma Argentina, aliwahi kuwa mtangazaji hapo mwaka huo). hakunielewa,lakini nilimwambia ugnetumia muda wako kuangalia kila siku picha za ngono usingekwenda Argentina kusaka MASTERS, wala kufanya saveyi katika latin amerika. Duuh kumbe alikuwa katika uatafiti kuhusu hili suala. Ila sijui huko alikokafikia wapi na utafiti wa suala hilo. Eeeeh naaacha nimechok macho yanauma

    JibuFuta
  4. Kaka Bwaya, mimi ni mgeni, nimepita hapa kujitambulisha naipenda sana kazi yako. karibu kwenye kijiwe changu, unisaidie kuiboresha.

    ni mimi Koero Mkundi

    JibuFuta
  5. Bwaya Bwaya Bwaya!! Nijaalie za Singida Mkuu. Haya Man, nakumbuka msanii mmoja wa Reggae aitwaye Nasio Fontaine alitufananisha binadamu na "apple". Akasema na hapa namnukuu kuwa "though the apple looks rosy on the outside, yet Jah know that it is rotten on the inside" na akaendelea kuwaasa walio walio nje ya apple kuwa "though the apple. looks good, don't get tempted" Nakati ya sentensi zake zooote alizoimba kwenye albamu zake nne nilizonazo, napenda iliyo ndani ya wimbo huu akisema "YOU LOOKING GOOD FROM AFAR, BUT YOU'RE FAR FROM LOOKING GOOD". Sasa mtazamo wa huyo jamaa wa Suti na tai, nadhifu kwelikweli tena na "heshima" yake wala usidhani unaeleza kilicho ndani ya ubongo wake. Wengine mwonekano wa juu ni kuficha "kamasi" zilizochukua nafasi ya ubongo. Sidhani kama nina tatizo na hawa waangaliao picha za utupu, si zipo bwana na wana-enjoy, ninalowaza ni kinachofuata baada ya hapo. Yaani kuangalia filamu za vita kama hakukufanyi uwe mgomvi kunaiathiri vipi jamii? Ama kuangalia madubwana yako ukaondoka hapo na ari mpya, kasi mpya na nguvu mpya ya kuijenga taifa kungeiathiri vipi jamii? Nasema kama hawa watu wanatumia hii kama njia ya kuamsha mizuka yao ya kazi basi zijengazo taifa (kama watu wanavyokunya kahawa wakiwa na usingizi) basi waendelee kivyaovya, lakini najua huu si ukweli. Wana-charge hisia mbovu wakatafute wa kumunyana nao tena wakati mwingine kwa simu za kazi na kutoroka kazi kwenda gesti bubu.
    Eeeee, nami naacha kama Marcus ama Kitururu. Nakumbuka aliyesema SERIKALI YA MTU NI KICHWA CHAKE kwa hiyo na kila mtu ajiongoze kwa style yake (ilmradi haiathiri jamii). Kwani hawa tunaowasema watasema sisi ni wabinafsi? Kwamba tunapenda dunia ipende tupendayo sisi? Lol. Basi kama hawawezi kubadilika na wafanye kwa siri, wafunge wakishamaliza kisha wasiharibu kazi kwa fikra hizo.
    Blessings

    JibuFuta
  6. Mpangala, kumbe jamaa inawezekana alikuwa kwenye utafiti? Najaribu kutafakari aina ya utafiti kwa kutumia picha za utupu. Elimu bwana!


    Mzee Changamoto,

    Je, maadili ni suala la kibinafsi ama kijamii?

    Koero karibu sana. Nimefurahi kupata mgeni mpya. Karibu tena na tena. Nitakutembelea hivi punde kujifunza kwako.

    JibuFuta
  7. hata mimi nilianza kutembelea ngono kabla ya kujua kuwa kuna google, blog, web na vitu lukuki. web za ngono zilinibadilisha kweli

    JibuFuta
  8. Kamala,

    Ngono ziliwezaje kukubadilisha?

    JibuFuta
  9. baada ya kuzitembelea kwa wingi, cjui itu gani kilinijia nikaona kuna google na kuanza kusearch vtu vya kitanzania na baadaye vya kimasomo na maarifa mbali mbali ya dunia nikaishia kuwa na blog na sasa naingia kufungua website yangu.

    nilianza kwa kutumia email nikangia ngono na sasa nazidi kukua

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Haiba ni nini?

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Uislamu ulianza lini?