Naam. Idadi ya wanablogu inaongezeka. Na kila mwanablogu anakuja na mtazamao mpya. Hebu mtembelee Koero uone. Kama utakavyoona, ujio wa watu kama hawa ni wa muhimu sana. Karibu sana Koero tujadiliane.
Labda naweza kuwa nakosea, lakini nadhani ile dhana kuwa hatupendi kufikiria inaanza kuondoka polepole. Labda sasa ni kwamba hatupendi kuchangia fikra zetu lakini nalo litaondoka. Ule mtazamo wa kila mwenye blog aje na picha sasa unaanza kupoteza ukweli na sasa watu wanaanza kufikirisha wasomaji zaidi. Lakini pia twahitaji taswira kwa hiyo wenye kufikirisha kama Koero karibuni saaana na wenye taswira pia mwakaribishwa maana mwatusaidia "kusindikiza" tafakuri zetu. Karibu Koero na wenye nia ya hivyo
(picha kutoka Mawazoni bila ruhusa) Ningependa kumwomba mheshimiwa Katibu Mtendaji wa JUMUWATA ruhusa ya kuuliza swali hili. Tumefikia wapi na ile Jumuiya ya Wanablogu Tanzania? Mnaonaje tukifanya mjadala wa wazi kuhusu 'ufufuaji' wa jumuiya yetu? Jamani yasijeyakawa yale ya mwaka elfu tisa mia sabini na saba.
WANAUME wengi wanaamini wanawake, kwa kawaida, ‘wanapenda hela.’ Kwamba ukiweza kumhakikishia mwanamke 'uhakika wa kiuchumi' unakuwa umemaliza. Ingawa hatuwezi kupuuza ukweli kuwa uhakika wa 'kiuchumi' ni moja wapo ya mahitaji ya mwanamke, lakini si sahihi kuamini kuwa moyo wa mwanamke unaweza kuthamanishwa kwa fedha. Fikra hizi walizonazo wanaume [kuwa anachokihitaji mwanamke ni fedha] zimeleta matatizo mengi katika mahusiano na ndoa. Kwa mfano, wapo wanaume ambao baada ya kuhakikisha wenzi wao wamepata mahitaji ya msingi, basi wanawatelekeza kihisia. Hali hii husababisha upweke mkubwa kwa wanawake hawa wanaojikuta hawana mtu wa karibu kuwasikiliza isipokuwa vitu.
YAMEKUWEPO madai kwamba Uislam ulianza tangu kuumbwa kwa dunia. Na wapo watu wanaotuaminisha hayo. Ukweli ni kwamba Uislam ulianzishwa na Nabii Muhammad mwaka 622 BK huko Arabia. Kabla yake, dini zilizokuwepo zilikuwa ni Uyuda ambayo ni dini rasmi ya Wayahudi (Judaism) na Ukristo ambayo ni dini ya mataifa wasio Wayahudi ulioanza miaka kadhaa baada ya Yesu kuwa ameondoka mwaka 33BK. Yesu mwenyewe hakuanzisha Ukristo. Alisali katika misikiti ya Wayahudi. Masinagogi. Maelezo haya yana msingi wa kistoria na sio propaganda za kidini. Ndio ni propaganda kwa sababu dini zote zimekuwa na tabia ya kuonyesha kwamba zenyewe ndizo za kweli kuliko dini nyinginezo hata ikibidi kwa kuichezea historia. Na ni bahati mbaya kwamba Dini zimekuwa na tabia ya kufanana ya kuzima uwezo wa waumini wake kuhoji lolote kwa kuwajengea hofu ya kujitafutia laana. Qur’an inatupa maelezo yanayokinzana kuhusu lini hasa Uislamu ulianza. Baadhi ya mistari katika kitabu hicho zinadai kwamba ‘nabii’ Muhammad ndiye ...
Ukitazama picha hii kwa makini, unaweza kubaini utata fulani wa kimaamuzi. Ukiitazama kwa haraka haraka, huwezi kuuona utata huo na hivyo huwezi kukubaliana na mtazamaji mwingine atakayedai kuuona utata usiouona wewe. Sasa itazame kwa makini kadiri unavyoweza halafu ujiridhishe kwamba unachokiona ndicho kinachopaswa kuonwa. Heri ya mwezi mpya.
Kuna wakati unaweza kufikiri unaigiza msimamo na kejeli kwa maumivu ya mtu, unakuwa na maoni yasiyo na haya kwa mateso ya wenzako ukijua unawafurahisha watu fulani lakini hayo maigizo ya kukosa huruma kwa mwenzako yana uwezekano wa kugeuka tabia kweli na ukawa mtu katili kweli kweli. Michezo, dini na siasa visikuchochee kujiona una haki ya kubeza masaibu wanayopitia wenzako kwa sababu mdogo mdogo mizaha hugeuka ukweli. Mwaka 1971, Philip Zimbardo, mshunuzi na mwalimu wa Chuo Kikuu cha Stanford, alifanya utafiti maarufu kama #StanfordPrisonExperiment akilenga kuchunguza nguvu ya mazingira kwenye tabia. Utafiti ulivyofanyika Zimbardo alitengeneza gereza la kuigiza hapo chuoni likiwa na seli, mahali mfungwa angekaa mwenyewe, mahali pa wanyarapa kuishi, mahali wafungwa wangetoka na kuteswa na wanyapara. Washiriki walifanyiwa mchujo wa haiba kuona kama ni watu wenye utimamu wa tabia na hisia. Kwa njia ya nasibu (random assignment) wanafunzi...
Katika makala haya, tunatazama kwa ufupi makuzi ya mtoto mwenye umri wa siku moja mpaka miezi 36. Tutaangalia mambo ya msingi yanayonesha ukuaji wa mtoto unavyoendelea katika maeneo makubwa manne; 1) ukuaji wa kimwili 2) kiakili 3) kimahusino na watu wengine na mwisho 4) kihisia. Kwa kawaida maeneo haya manne yanategemeana ili kumwezesha mtoto kukua kwa ujumla. Kwa mfano ili mtoto akue kimwili, anahitaji ukuaji wa akili ipasavyo ambayo nayo itaathiri namna anavyomudu hisia zake na hivyo kuhusiana na watu wengine. Kwa hiyo ni sawa tukisema hakuna ukuaji wa eneo moja usiotegemea eneo jingine.
Mkesha wa kuukaribisha mwezi mpya ndio huu. Kesho tutauanza mwezi mpya kwa siku iitwayo 'ya wajinga'. Masuala ya kuangazia kidogo: Ni kwa kiasi gani umepoteza muda mwingi pasi na sababu ya msingi? Soga. Stori zisizojenga. Kuwakatisha tamaa watu. Mabishano. Na kadhalika. Na kadhalika. Umesafiri kilomita ngapi mwezi huu? Hebu fikiria, kama ungeamua kuzitumia kilomita hizo kusoma, ungesoma vitabu vingapi? Kwa mwezi Machi, umeweza kusoma vitabu vingapi? Ni fedha kiasi gani umetumia kununua vitabu? Utasema hela hazitoshi. Hivi unajua ni shi'ngapi umeteketeza kwa kukwangulia vocha mwezi huu? Umekwangua vocha kusaidia kusambaza 'text messages' za mizaha! Umeona ulivyo na fedha? Haya. Hima na tuanze kuzitumia hizo hizo vitabuni mwezi huu! Na tusome. Mwezi Aprili uwe ni wa kusoma.
Haswa! Koero kaja kakamilika. Tunakukaribisha kwa mikono yote. Kazi yako ni nzuri sana.
JibuFutaLabda naweza kuwa nakosea, lakini nadhani ile dhana kuwa hatupendi kufikiria inaanza kuondoka polepole. Labda sasa ni kwamba hatupendi kuchangia fikra zetu lakini nalo litaondoka. Ule mtazamo wa kila mwenye blog aje na picha sasa unaanza kupoteza ukweli na sasa watu wanaanza kufikirisha wasomaji zaidi. Lakini pia twahitaji taswira kwa hiyo wenye kufikirisha kama Koero karibuni saaana na wenye taswira pia mwakaribishwa maana mwatusaidia "kusindikiza" tafakuri zetu.
JibuFutaKaribu Koero na wenye nia ya hivyo
waama kweli kabisa
JibuFuta