Mwaka wa malengo mahususi ndio huu

Mwaka unaishia leo. Watu wengi watakwambia jitathmini. Kuona wapi ulikosea. Wapi ulilikoroga. Wapi ulifanya vizuri na mambo kama hayo.

Binafsi sioni sababu yoyote ya kufanya hivyo. Sioni sababu ya kufanya hicho kinachoitwa tathmini ya mwaka. Sababu ni kwamba hata kama ungegundua wapi ulikoharibu, huna unachoweza kufanya zaidi za kujiumiza moyo. Utaumia moyo, na historia itabaki pale pale. Maana historia ilikwisha kuandikwa. Kama ulishindwa mwaka huu, hesabu ni upepo umepita.

Hata kama ungegundua wapi ulifanya vizuri, ukweli ni kwamba hayo wameshapita. Yaache yaende. Hakuna haja ya kulewa sifa zisizoweza kukusaidia leo. Siafa za jana zinabaki kuwa za jana. Huna sababu ya kuangalia nyuma. Historia haiwezi kukusaidia. Una sababu ya kuiacha ipite vile ilivyokuwa.

Nionavyo mimi, huu ni wakati wa kutazama mbele. Kuwa na malengo. Usipojua unakokwenda, utaishia kokote. Wafanyakazi waangalie namna watakavoboresha utendaji wao wa kazi. Wanafunzi wajiangalie watakavyoweza kusoma kwa bidii. Wazazi, namna watakavyowalea watoto kwa ufanisi zaidi. Mafisadi, namna watakavyoiba kwa makini zaidi.

Katika kufanya hivyo, tukumbuke kuwa namna tunavyofikiri huathiri uhalisia wa mambo. Tukianza kufikiri kushindwa kabla hata hatujaanza, ni hakika yake tutashindwa. Tukianza kuhisi kukwama, ni hakika tutakwama sana. Busara ni kuona kuwa mwaka unaoanza utakuwa wa mafanikio kwako. Kwa kila unachotia mkono wako kukitenda, ona/fanya kama suala la kushindwa halipo. Maana hutoshindwa, mpaka uamini akili mwako kwamba umeshindwa. Kila kitu kinaanzia akilini kumbuka.

Wengi wetu hatufikii malengo yetu pengine ni kwa sababu ya malengo hayo kutokuwa mahususi (specific). Hayapimiki. Hayaeleweki. Ni ya jumla jumla. Malengo yanayoelea elea.

Mtu anakwambia, "..mwaka huu lazima nifanikiwe...!".
Unamwuliza, "...unataka ufanikiweje?"
"...sina lugha nzuri sana ila nataka kufanikiwa, naona kufanikiwa yaani...".
"...katika eneo lipi sasa?..."
"...maeneo yote. Yote nifanikiwe...".
Ukimwuliza lini, anakwambia, "..ah, wakati wowote bwana...lazima nitoboe!"

Mipango ya jinsi hii ni ndoto na huwa haitekelezeki. Na hata kama "utafanikiwa" hatuwezi kujua, maana hatukupanga. Twapaswa kuwa na malengo yanayopimika. Malengo ya Yenye muda mahususi kuyatekeleza. Ni kwa namna hiyo tutaweza kuyakagua kila wakati kuona tunavyoyafikia. Tumia kitabu cha kumbukumbu za kila siku. Kama huna kinunue leo. Tukianzia hapa, suala la kutunza muda halitakuwa mgogoro. Tutaweza kuukomboa wakati. Na mwaka utakuwa wa mafanikio.

Heri ya mwaka mpya.

Maoni

  1. Ndugu yangu,kila mwaka mpya unapofika huwa nawakumbuka wale rafiki zangu wanaopiga madebe na kuchoma matairi usiku.Ukiwauliza wengi wao kuhusu mafanikio ya 2008 au matarajio ya 2009 hawana jibu.Lakini katika dunia ya sasa huwezi kumlaumu mtu kushangilia kumaliza mwaka,huku mafisadi huku magonjwa huku vimbunga,majambazi,nk.Nadhani njia nzuri ya kusherehekea mwaka mpya ni kanisani au msikitini,au faragha kutafakari na kutafakuri mwaka huu umeishaje na ujao utaishaje.

    Ndugu yangu Bwaya,nakutakia kila la heri katika 2009.Tuzidi kuwa sote katika libeneke la ku-blog.Tuna nafasi muhimu (japo haijatambulika sana) katika kuwasemea wasioweza kusikika.Happy New Year,Bwaya.

    JibuFuta
    Majibu
    1. I 'm so glad you could come across this site ,
      and we hope to establish good relations with you.
      greetings from me ( OBAT KUAT )


      obat pembesar penis

      jual vimax

      obat kuat viagra

      jual kondom

      Futa
  2. Heshima kwako Kaka Evarist na asante kwa yote. Napitia na kusoma na kuelimika na kuerevuka kila niangaliapo kitokeacho ughaibuni. Kaka Bwaya naamini umemaliza. Lakini niseme tena kuwa "taswira tujengayo vichwani mwetu ndiyo ituongozayo katika maisha yetu halisi". Natujenge taswira njema, zenye mafanikio, zenye upendo, heshima, amani na utu na pia kukua katika kila imani tuliyopo (maana zote zahimiza upendo na umoja) kisha tutendee kazi mipango yetu myema.
    Tutafika tukishajielewa.
    Heri ya mwaka

    JibuFuta
  3. Nawatakieni Heri ya Mwaka Mpya bloggers wote.
    Na wasomaji wetu.
    One love.

    JibuFuta
  4. salam. thanks your comment. you can translate my post to your language by Google translate in my blog.

    JibuFuta
  5. Habari kaka Bwaya

    Nakutakia heri ya mwaka mpya wa 2009.
    Naomba tuendelee kushirikiana kama mwaka uliopita.

    JibuFuta
  6. Nimkujw akuwasalimia tu HAMJAMBO JAMBO? heri ya mwaka mpya

    JibuFuta
  7. tusiishi jana na wala tusiiogope kesho,tuishi maisha tuliyonayo sasa.

    JibuFuta
  8. Nawatakia wote kila lililojema kwa mwaka huu tuliouanza. Tuendeleze kusudi lile lile kwa nia ile ile.

    JibuFuta

Chapisha Maoni

Zilisomwa zaidi wiki hii...

Maana ya Saikolojia na Nafasi Yake Katika Jamii -1

Mambo Yanayoweza Kugusa Moyo wa Mwanamke-1

Tumia Mbinu Hizi Kuelewa Unachokisoma -3

Haiba ni nini?

Ukuaji wa Kiakili na Kimwili kwa Mtoto wa Miaka 0 – 3

Uislamu ulianza lini?